Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, February 20, 2013

MNYIKA: SERIKALI INAWAUZIA KESI WALIMU



MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amesema serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inawauzia kesi walimu wa shule za msingi nchini kwa kuwaeleza wazazi na walezi kuwa elimu ya ngazi hiyo inatolewa bure huku ikiwa haitimizi wajibu huo ipasavyo. Mnyika alitoa kauli hiyo jijini Dar es Saalam juzi alipokaribishwa kuhudhuria mkutano wa hadhara wa wakazi wa Mtaa wa Kanuni uliokuwa na lengo la kuzungumzia kero mbalimbali zinazowakabili. Alisema mara nyingi Waziri wa Elimu anapokuwa bungeni akiulizwa maswali husimama na kusema elimu ya msingi ni bure kwa kuwa Watanzania wanakatwa kodi zinazotumika kupeleka mahitaji ya msingi katika shule zote. “Mnaniambia wengine mnatozwa hadi sh 70,000; mimi ninawaambia serikali ya CCM katika hilo imewauzieni kofia ya polisi kwa kuwa hawatekelezi jukumu lao ipasavyo,” alisema Mnyika.

Aliwataka wakazi wa jimbo la Ubungo kutowafumbia macho walimu watakaowatoza fedha ya kuwaandikisha wanafunzi au kuwalazimisha kutoa michango bila kuwa na kikao cha makubaliano baina ya wazazi na kamati ya shule. Akizungumzia malalamiko ya wakazi wa Mtaa wa Kanuni kuhusu kujengewa barabara kwa kiwango cha lami, Mnyika alisema wananchi wanapaswa waitunze barabara iliyopo kwa kuzuia magari makubwa yasipite wakati mchakato wa kuboresha ukiendelea. Kuhusu madai ya wakazi wa Mtaa wa Kanuni juu ya matumizi ya sh milioni tano zilizotolewa na mfuko wa jimbo kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu ambayo walidai haikutumiwa ipasavyo, Mnyika alisema atafuatilia kujua fedha hizo zimetumika vipi na kwa nini mradi wa kivuko cha mtaa wa Kanuni uko chini ya kiwango

Source: Khamis, A. ( February 20, 2013). Serikali inawauzia kesi walimu. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: