Jenerali Ulimwengu aliandika hivi, tarehe 24 februari 1995 ".....hatuna budi kukataa juhudi za kudhalilisha elimu ya wanetu. Hatuna budi kutambua kwamba iwapo tutakubali ziwepo tofauti katika viwango vya elimu vinavyotolewa kwa makundi tofauti tutakuwa tunakubali kupanda mbegu za mfarakano mkubwa huko mbele ya safari." - Raia ya Jenerali (wenye elimu watatawala)
Jenerali kaandika hivi leo "......tukishindwa kulielewa hili, kama ambavyo naona tunashindwa, basi tuelewe kwamba hatujengi Taifa moja. Iwapo tumekubali kwamba kila anayeweza ana hiari ya kuwafundisha wanawe kadiri anavyojua, basi tuelewe kwamba tunajenga mataifa mengi ndani ya nchi moja na tutambue kwamba iko siku mataifa haya hayataiva ndani ya chungu kimoja"
Nukuu ya kwanza nilikuwa Kidato cha Nne shule ya Sekondari Kibohehe wilayani Hai. Nukuu ya pili nimemaliza masomo na shahada za uzamivu na kupewa dhamana ya Ubunge na Uongozi wa Kitaifa katika chama changu. Lakini ukali na mantiki ya maneno ya 1995 na ya 2013 ni sawa kabisa. Tayari tuna mataifa mawili ndani ya nchi moja, Taifa la Masikini na Taifa la Matajiri (wenye uwezo). Masikini wana shule zao na Matajiri wa Shule zao. Masikini wengi tumewadanganya eti watoto wao wamesoma mpaka kidato cha nne.Tunaficha uchafu chini ya kapeti hata kwenye Elimu
Source: Zitto Kabwe Facebook wall. Follow Zitto on Facebook, click here, Zitto Kabwe
No comments:
Post a Comment