Nchi za Umoja wa Ulaya (European Union - EU) zikiongozwa na Ujerumani wanafanya uchunguzi wa kufungiwa kwa magazeti nchini ili kuweza kupata uhakika na kushauri serikali pale panapofaa. Hatua hiyo inafanywa ili kujenga uhusiano na jamii kuhusu utata uliopo wa kuona baadhi ya magazeti kufungiwa, likiwamo gazeti la kila wiki la MwanaHALISI.
Hayo yalisemwa na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania alipokuwa akizungumza na wanahabari kuhusu Maadhimisho ya miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ya Radio Deutsche Welle (DW) yatakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Alisema uhuru kwa vyombo vya habari katika nchi unasaidia katika maendeleo ya nchi na jamii husika huku ikikuza demokrasia na waandishi wa habari wakifuata misingi ya taaluma yao.
Source: Wavuti (February 21, 2013). Kifungo cha MwanaHalisi:EU kuchunguza, kuishauri serikali. Retrieved from Wavuti
No comments:
Post a Comment