Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, September 25, 2015

BREAKING NEWS: KIJANA KUTOKA DIASPORA, USA, AENDELEA KUWA TISHIO MBIO ZA UBUNGE


 Juu na chini akiwa Ubaruku. Chini anachukua maswali baada ya mkutano

Ni Liberatus Mwang’ombe “ Libe”, au kama watu wa Mbarali wanavyo muita “Mnyamwezi” aliye wahi kukaaa DMV (DC, Maryland na Virginia) ameendelea kuwa gumzo kwenye mbio za Ubunge jimboni Mbarali.  Mwang’ombe amekuwa akivunja rekodi kwa kila mkutano anao fanya; amekuwa anakusanya watu wengi sana kuliko kipindi chochote cha ubunge jimboni Mbarali

Uwezo wa Mwang’ombe kutoa hotuba za umoja, ushirikiano na bila kuweka uchama imekuwa chachu na kigezo cha kuwavuta wana Mbarali wengi.   Zaidi, Mwang’ombe amekuwa akiongea na watu wa kila aina hadi wa CCM ambao ndio mahasimu wake kisiasa: amekuwa akiwafuata CCM na kuwapa mikono kitendo ambacho kimekuwa kikiwashangaza watu wengi.  Kumekuwa na kasumba ya watu wa CCM na CHADEMA kuto kusalimiana na kuogopana kipindi cha kampeni; tofauti na Mh. Mwang’ombe ambaye amekuwa akipita hadi kuwasalimia watu wa CCM hata kama yeye ni CHADEMA.
 
Alipewa uchifu siku ya ufunguzi
Watu wa kila pande ya jimbo la Mbarali wamekuwa wakizungumza kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya Mh. Mwang’ombe; huku wengine wakisukuma gari lake baada ya mikutano, wengine wakimzuia barabarani hadi ashuke ili wamuone, wengine wakitaka atembee nao barabarani kuonyesha umoja na mshikamano.

Liberatus Mwang’ombe anaomba msaada kwa waTanzania wote, diaspora na waliopo nchini, wamsaidie kufanikisha harakati za kwenda DODOMA. 

Mh. Mwang’ombe anaomba michango ya kifedha ambayo inaweza tumwa kupitia WAVE-App,  M-Pesa number  +255 752 494 409

Au kama una mchango na huna WAVE-App wasiliana na

Rehema 301 367 9711
Jabil         240 604 0574

Lukresia 240 593 5973



Kwa picha zaidi endelea kurasa ya pili










No comments: