Dr. Slaa akiwa na Gavana wa Alabama 2013 |
Katibu Mkuu wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa ameondoka nchini jana
(Jumamosi Aprili 11, 2015) kuelekea nchini Marekani ambako atakuwa na ziara ya
kikazi ya siku tisa. Dk. Slaa katika safari hiyo ameambatana na mkewe Josephine
Mushumbusi.
Ziara hii ya siku tisa ni mwaliko
wa Gavana wa Jimbo la Indiana Mike Pence pamoja na taasisi mbalimbali za nchini
humo ikiwemo vyuo vikuu kutokana na kutambua mchango wa kisiasa na kijamii wa
Dr Slaa na Chadema katika maendeleo ya bara la Afrika na kipekee nchini
Tanzania. Ziara hiyo itamwezesha Dk. Slaa kushiriki mijadala mbalimbali
inayohusu uwekezaji, elimu na uongozi iliyoandaliwa kwa ajili yake ambayo lengo
lake kuu ni kuitangaza Tanzania kwa ukamilifu wake.
Kwa malengo hayo, Dk Slaa
atafanya mihadhara (Public Lectures) kwenye vyuo vikuu vya Purdue, Indianapolis
na Marion. Sanjari na mihadhara hiyo, Dk Slaa atakua na vikao vya mashauriano
na baadhi ya Maprofesa waadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali kwa lengo la
kubadilishana uzoefu juu ya masuala ya kisiasa na maendeleo na kijamii na
ushiriki wa Chadema katika siasa za Kimataifa.
Zaidi, ziara hii itamkutanisha
pia Katibu Mkuu na viongozi na watendaji wakuu wa kiserikali na makampuni mbalimbali
pamoja na taasisi kubwa za uwekezaji kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika
masuala ya uchumi na uwekezeji Barani Afrika na kwa kipekee Tanzania.
Imetolewa na:
Deogratias Munishi
Kurugenzi ya Mambo ya
Nje
No comments:
Post a Comment