Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeahirisha kutoa uamuzi wa ombi la kufutiwa shtaka la pili katika kesi kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi a na kufanya mikusanyiko isivyo halali kwa lengo la kwenda Ikulu inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na wenzake wanane wafuasi wa chama hicho. Mbali na Mdee, washtakiwa wengine ni Rose Moshi (45), Renina Peter, Anna Linjewile (48), Mwanne Kassim (32), Sophia Fangel (28), Edward Julius (25), Martha Mtiko (27) na Beatu Mmari (35).
Hakimu Kaluyenda alisema kesi hiyo ilitakiwa kutolewa uamuzi mdogo juu ya ombi la wakili wa utetezi, Peter Kibatala, ambaye aliiomba mahakama kufuta shtaka la pili kwamba washtakiwa hao walikusanyika kwa lengo la kutaka kwenda Ofisi ya Rais Jakaya huku akidai shtaka hilo lina mapungufu kisheria,kwani halikuainisha vifungu vya kisheria. Hata hivyo, upande wa mashtaka ulidai kuwa hakuna madhara yoyote endapo vifungu hivyo havikuanishwa. Hakimu Kaluyenda alihairisha kesi hiyo hadi Januari 13, mwaka huu kutokana na kutokamilisha utoaji wa uamuzi wa ombi la wakili Kibatala.
IPPMEDIA/Nipashe
No comments:
Post a Comment