Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, November 16, 2014

MWANA-DIASPORA, LIBERATUS MWANG'OMBE "LIBE", ATOA "INSPIRATIONAL SPEECH" KWA FORM FOUR

Hotuba ikiendelea
Akiongea na watahiniwa wa kidato cha nne siku mbili kabla ya mtihani wa Taifa 2014,  shule ya secondary Montfort iliyopo Rujewa, Mbarali, Mwana-diaspora kutoka Washington, D. C., Marekani,  Liberatus Mwang'ombe "Libe" alianza kwa kusema, Montfort ni shule aliyo soma na anajisikia faraja akiyaona mazingira yale.  Aliendelea kwa kusema, maamuzi ya mwisho ya kila binadamu yapo chini ya himaya yake.  Alisema "huwezi kutegemea mtu baki au mwingine aongoze au arutubishe maisha yako, ni wewe binafsi unaweza kufanya tofauti kwenye maisha yako na kila binadamu ni kiongozi.  Pia alisema anaamini kuwa kila binadamu ana ndoto zake kwenye maisha; alisema; "ni muhimu kujiwekea malengo ya ndoto zenu. Malengo ambayo yanatimilika, malengo ya kiuhalisia na malengo yenye muda maalumu." Aliendelea na kusema, "ndoto bila malengo itaendelea kuwa ndoto na kutimilizwa kwake kutaendelea kuwa ni ndoto tu."  Mwisho Ndg. Libe aliwaomba wanafunzi hao wasimuangushe kwa kuweka malengo kwenye ndoto zao na kuhakikisha wanazitimiliza.

 Mbali ya maongezi Ndg. Liberatus alichangia miundombinu ya elimu kwa wanafunzi hao
Moja ya wanafunzi akimshukuru Liberatus kwa kukumbuka alipotoka
Juu na chini Libe akiendelea kubadirishana mawazo na wanafunzi




Kwa habari zaidi za Liberatus Bagasa Mwang'ombe, BOFYA HAPA

Source:SwahilivillaBlog

No comments: