Serikali imetakiwa kutatua matatizo ya wakulima nchini Tanzania kwa kuwatafutia masoko ya uhakika ya mazao ili kuepuka malalamiko yao kila kona ya nchi. Hayo yalisemwa wilayani Sikonge, mkoani Tabora na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku nne ya ‘operesheni Delete CCM’ (ODC). Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kuwahamasisha wananchi kujitokeza na kujiandikisha kwa wingi na kuchagua upinzani katika chaguzi wa serikali za mitaa na kuikataa Katiba iliyopendekezwa.
“Wakulima wa tumbaku wanalia, wakulima wa mpuga wanalia, wakulima wa kahawa wanalia huku serikali ikitoa vibali kwa wafanyabiashara wakubwa kuagiza bidhaa kutoka nje badala ya kuwatafutia wakulima wao mazao ya uhakika,” alisema Mbowe
Nipashe
No comments:
Post a Comment