Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, September 6, 2014

JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA-TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA KUTOKA CCT

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) inachukua fursa hii kuvishukuru vyombo mbalimbali vya habari kwa jinsi ambavyo vimekuwa vikitoa taarifa mbalimbali kuhusu kazi na matamko ya CCT. 
Kuhusiana na mchakato wa kuandikwa kwa Katiba mpya, CCT inaamini kuwa suala hili ni la MARIDHIANO na sio la ubabe wa kikundi au chama fulani cha siasa.-Kama ambavyo ilitangazwa na Mhe. Rais Januari 2014 kuwa Taasisi mbalimbali zipeleke mapendekezo ya wajumbe wanaoweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, CCT ilipeleka mapendekezo ya wajumbe tisa na kati ya hao Mhe. Rais alimteua mjumbe mmoja tu ambaye ni Bibi Esther Msambazi.
Mjumbe huyu aliyeteuliwa ni Mkristo wa kawaida (lay Christian) na wala si Kiongozi wa Dhehebu lolote la Wanachama wa CCT na pia hata sio Mzee wa Kanisa analotoka bali Mkristo mwaminifu wa kawaida. Huyu ndiye mwakilishi wa CCT kwenye Bunge Maalum la Katiba. Viongozi wengine wa Dini ya Kikristo (Maaskofu na Wachungaji) waliopo katika Bunge hilo HAWAKUTUMWA NA CCT na wala CCT haina taarifa ni vipi walichaguliwa kuwa wajumbe wa Bunge hilo Maalum.

Aidha, pia Jukwaa la Wakristo Tanzania haliwatambui Viongozi hao kwani Jukwaa hilo linaundwa na Taasisi za TEC, CCT, PCT na SDA. Kutokana na misingi ya imani ya taasisi hizi kwa umoja wake, Viongozi wakishakubaliana jambo fulani kwa pamoja na kwa umoja wao wanalisimamia na kulitekeleza. NDIYO YAO NI NDIYO NA HAPANA NI HAPANA kwa kuwa hawana ndimi mbili na wala hawatumikii Mabwana wawili. 

Kwa mantiki hiyo, CCT ikiwa mmoja wa taasisi zinazounda Jukwaa la Kikristo Tanzania inaendelea kusisitiza kuwa msimamo wa viongozi wa dini kama ulivyotolewa na Jukwaa la Kikristo Tanzania kuhusiana na Maoni waliyopeleka kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Wananchi chini ya Uenyekiti wa Mhe. Jaji Mstaafu Warioba na Matamko waliyotoa ni sahihi na itaendelea kuyasimamia na kuyasambaza hadi yamfikie kila Mkristo ili wananchi wa Tanzania wapate Katiba wanayoitaka.

Aidha, Viongozi hao wa Jukwaa la Wakristo Tanzania haliwezi kutafuta maoni ya Viongozi wa Dini walioko katika Bunge Maalum la Katiba kwa sababu hawawatambui kama wawakilishi wa taasisi zao na hivyo kukataa kwa nguvu zote yale ambayo viongozi hao waliopo Bungeni watakuwa wakiyasema. Mwisho kabisa tunawaomba viongozi hao wajiulize, “hivi sisi tumetumwa na tunamwakilisha nani humu Bungeni?
Imetolewa September 05, 2014 Na JUMUIYA YA KIKRISTO

No comments: