MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Mbowe, amesema hawako tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itumie
daftari la wapiga kura Jimbo la Kalenga lililochakachuliwa wakidai kwamba
limefanyiwa marekebisho mwaka 2014. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja
vya Mwembetogwa mjini Iringa, Mbowe alisema kama NEC watatumia daftari hilo
watakuwa wamesababisha vurugu na hawatakuwa tayari.
“CHADEMA hatuko tayari kutumia daftari la wapiga kura la Jimbo
la Kalenga lililofanyiwa marekebisho mwaka 2014… kama watalitumia kitanuka
maana hatutakubali,” alisema. Msimamo wa CHADEMA ni kwamba litumike daftari la wapiga kura la
kudumu la mwaka 2010 ambalo halina marekebisho yoyote kwa kuwa watu waliokufa
eneo husika wanawafahamu.
Mloswe D./Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment