Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, March 17, 2014

Green Guard; Mtu akiikataa CCM achomwa Kisu?

Na Bryceson Mathias

MBINU za kuteka, kutesa na kuua raia, hivi karibuni zilileta tafrani Katika Kampeni za kumpata Mbunge wa Jimbo la Kalenga Katibu wa Vijana wa CHADEMA Tawi la Ikuwilo mkoani Iringa, Kata ya Luhota, Richard Mawata (33) kujeruhiwa kwa kuchomwa kisu kifuani na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM usiku.

Kama ni kweli Green Guards wa CCM wamefikia hatua ya kufanya unyama wa namna hii basi ni dhahiri wameshindwa kufanya ushawishi kwa wapiga kura jukwaani, badala yake wamebaki na mbinu hii chafu, hii ni mbaya na haikubaliki mbele ya jamii,

Swali langu kwa Serikali, CCM wakikosa uungwaji mkono na wananchi adhabu na Mshahara wake achomwe kisu, atekwe ateswe na kuua raia kama ilivyokuwa kwa Mawata wa Kalenga ilivyomtokea baada ya Mama yake mzazi wa kiongozi huyo wa Bavicha kujiunga na chadema.

Imebainika kwamba, baada ya CHADEMA kuvuta hisia za watu Kalenga kiasi cha Viongozi  muhimu wa CCM kujiunga kwa wapinzani hao, inadaiwa Vijana wa Green Guard walielekezwa kutoa vitisho vya unyama huo ili watu waogope kuujiunga na Chadema au vyama pinzani.

Sisi wa habari tunaona iwapo CCM ambao ndio wanatakiwa waviagize vyombo vya Ulinzi na Usala nchini kuhakikisha vinalinda Usalama wa Raia na Mali zao, halafu ndio hao hao vijana wao wanateka watu, kuwatesa kwa nia ya kuwaua, huo ni unyama na aibu kubwa kwa CCM..

Tunasema CCM watatuhumiwa na tukio hilo kwa sababu, ni baada ya masaa machache mama wa Mwnyekiti wa Bavicha (Mama Mwenda), alipojiunga na  chadema, ndipo mtoto wake alitekwa na Green Guards sita na kuchomwa kisu karibu kabisa na moyo, ikiwa kama kisasi.

Aibu nyingine ambayo sisi tunaiona si kwa Serikali na CCM peke yake, bali ni kwa Jeshi la Polisi hasa RPC wa Mkoa wa Iringa na Maamanda wa vituo vyake, ambao kwa siku za nyuma wamepakwa matope kwa mauaji ya Mwandishi wa Channel Daudi Mwangosi, na matukio mbalimbali dhidi ya Chadema.

Msajili wa Vyama naye anatakiwa kutupiwa Lawama kubwa kutokana na kukithiri na mwendelezo wa vitendo vya Utekaji uteswaji na vifo vinavyoendelea kuwepo vikidaiwa kufanywa na Vikundi vya ulinzi vya Vyama vya Siasa.

Kwa nini tunataka atupiwe lawama; ni kutokana na kunyamazia kimya vitendo hivyo viendelee katika jamii nyakati za chaguzi ndogo na kubwa, hali ambayo inaonesha Msajili hana au hawezi kuvichukulia hatua vyama hivyo, jambo linaloonekana anashindwa kuwajibika kikamilifu kukomesha matukio hayo.

Hata hivyo kuna taarifa za kuridhisha kwa Jeshi la Polisi ambapo inadaiwa wamekwisha wakamata baadhi ya watuhumiwa, ambapo tunahoji je watachukuliwa hatua au itakuwa kama ilivyo siku zote funika Kombe mwanaharamu apite?

Mbinu ya kuwaogofya wananchi kujiamulia itikadi wanazoziamini zitawasaidia, ni ya kiintejensia kamwe haiwezi kufanywa na Mtu wa kawaidia bali mwenye mafunzo ya kijeshi na yanayoongozwa na mtu mkomavu, alipata mafunzo nje ya nchi!.

Ni swali letu pia kwa Msajili wa Vyama Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Je kwa Demokrasia tuliyonayo, mwananchi hana haki ya kujiunga na Chama chochote? Je wafanyakazi ni lazima wawe wanachama wa CCM? Na Je hivi mtu asipoiunga mkono CCM adhabu yake ni kutekwa, kuteswa na kucharangwa mapanga?

No comments: