Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na Mbunge
wa Ubungo, John Mnyika amesema rasimu ya pili ya Katiba haijazingatia masuala
ya msingi kuhusu haki ya wananchi kumiliki na kunufaika na rasilimali za
nchi.
Mnyika alisema hayo kupitia taarifa aliyoitoa kwenye vyombo vya habari
na kuongeza kuwa hatua hiyo imekuwa kinyume na mapendekezo aliyoyatoa bungeni
na mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, juu ya haki za wananchi kuhusu
umiliki wa rasilimali.
Mnyika alisema alipendekeza Katiba mpya iweke ibara
mahususi ya haki za wananchi kumiliki rasilimali ikiwamo ardhi, madini, gesi,
mafuta, maji, misitu na maliasili nyingine.
Kadhalika, alisema wananchi
wakipewa haki ya kumiliki na kuwekewa mazingira ya Kikatiba ya kunufaika na
rasilimali zao, mianya ya mikataba mibovu, ufisadi na matumizi mabaya ya
rasilimali itazibwa.
“Natambua kwamba katika sura hiyo hiyo ya nne
sehemu ya pili inayohusu wajibu na mamlaka za nchi ibara ya 51 ya ulinzi
wa mali za umma, imetoa wajibu wa raia kulinda rasilimali na maliasili,
hivyo, wadau wanapaswa kuendelea kujadili suala hili kwa maslahi ya
uchumi wa nchi na wananchi wenyewe.”
Ippmedia/Nipashe
No comments:
Post a Comment