Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, February 14, 2014

Kesi ya Zitto yapigwa kalenda

      KESI iliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) ya kupinga kujadili uanachama wake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeahirishwa hadi Aprili mosi. Kesi hiyo iliahirishwa jana na Naibu Msajili, William Mutaki, kutokana na Jaji John Utamwa anayesikiliza shauri hilo lililopo Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kutokuwepo. Zitto kupitia kwa wakili wake, Albert Msando, aliiomba mahakama itoe zuio hilo la muda hadi kesi yake ya msingi namba 1/2014 aliyoifungua itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
       Hata hivyo, CHADEMA kupitia kwa mawakili wake, Tundu Lissu na Peter Kibatala, walipinga maombi hayo wakidai kuwa hayajakidhi vigezo vya kupewa zuio la muda wanaloliomba. Zitto alifungua kesi siku moja kabla ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CC) kuanza vikao vyake ambavyo vilikuwa vijadili utetezi wa tuhuma zake za kuendesha mkakati wa siri wa kusaliti chama, akiomba mahakama izuie suala la uanachama wake lisijadiliwe hadi kesi yake isikilizwe.
Tanzania Daima

No comments: