Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea na Operesheni Pamoja Daima katika
mikoa mbalimbali nchini. Kyela.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka madereva wa pikipiki
zinazobeba abiria maarufu kama `Bodaboda’ kuacha kumuunga mkono Waziri Mkuu
Mstaafu, Edward Lowassa. Akihutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Siasa ulioko mjini Kyela,
Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia chama hicho, Joseph Mbilinyi aliwashauri watu wa
bodaboda kupokea misaada ya kiongozi lakini ikifika uchaguzi waichague Chadema. Sugu,
ambaye alikuwa amefuatana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa ikiwa sehemu ya Operesheni
Pamoja Daima ya chama hicho, alisema kuwa Lowassa anatafuta kuungwa mkono na
makundi mbalimbali ili kufanikisha malengo yake ya urais.
“Lowassa
katika siku za karibuni amekuwa akitoa misaada mingi kanisani sasa amehamia
kwenye bodaboda,” alisema Sugu huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu
uliofurika kwenye mkutano huo. Sugu
alisema kuwa bodaboda wanapaswa kuachana na Lowassa kwani ni mwanachama wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho hakina msaada kwao. “Akiachana
na CCM, akaamua kwenda chama kingine basi mnaweza kumuunga mkono ila akibaki
CCM achaneni naye,” alisema Sugu wakati akimzungumzia Lowassa, ambaye hivi
karibuni alishiriki katika bonanza lililoandaliwa na Bodaboda jijini Dar es
Salaam. Mapema Dk
Slaa na Mchungaji Msigwa waliendesha operesheni hiyo kwa kupaa kwa helikopta
jana asubuhi hadi wilaya za Ludewa, Makete, Rungwe na Kyela huku wakiwekea
mkazo masuala ya matatizo ya ufisadi, matumizi mabaya ya rasilimali na vita
dhidi ya ujangili.
Lissu
avishukia vyombo vya dola
Viongozi
walioshambulia jukwaa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chadema kwa upande wa
Zanzibar, Said Issa Mohamed, Mkurugenzi wa Uenezi wa chama hicho, John Mnyika,
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema. Mnyika
ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, aliwashutumu viongozi wa Serikali kuwa wamekuwa
wakitumia vibaya rasilimali za nchi na kusababisha Watanzania kuendelea kuwa
masikini, huku wachache wakinufaika. Naye Lema
alizungumzia juu ya timuatimua iliyowakumba viongozi kadhaa wa chama hicho
akiwataka wananchi waamini kuwa Chadema ni makini na kamwe hakitawavumilia
wasaliti.
Source: Kaminyoge R., Matowo R., & Mussa M. (Jan. 2014). CHADEMA: Bodaboda achaneni na Lowassa. Kwela, Moshi, na Mpanda: Retrieved from Tanzania Daima

No comments:
Post a Comment