Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, January 16, 2014

BREAKING NEWS: Wana CCM 70 watimkia Chadema-Mvomero

KATIKA hali inayoonesha Umakini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kusimamia maamuzi yake ya kuachana na ajenda za Wasaliti ili kisitoke kwenye hoja muhimu, sasa kimejikita kwenye mikakati mizito ya 2014, ambapo wiki hii wanachama 70 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamejiunga na CHADEMA.

Wanachama hao wa CCM ni wale wa  Kijiji cha Kisala Mvomero, ambako Ng’ombe zaidi ya 15 walikatwa Miguu ya mbele na ya nyuma na Mapanga na Wakulima na Vibutu, na wa Kijiji cha Kigugu kulikotokea Mauaji, wafugaji na wakulima Sita kufa.

Katika Mashambulizi ya Madiwani Wanne wa Chadema Kata zao kwenye mabano, Dunstan Mwendi (Gairo Mjini), Luanda Zengwe (Nyandira), Luka Mwakambaya (Mtibwa) na Juliana Petro Dunstan Mwendi (Viti Maalum) yaliyofanywa Kigugu, Wanachma 20 wa CCM, walitimkia Chadema.

Mkutano uliofanyika Kijiji cha Kisala na Madiwani, Mwakambaya, Petro na Mgombea wa Udiwani Kata ya Sungaji  2010, Jairos Msigwa na Mwenyekiti wa Kata ya Sungaji Mvomero, Musa Kombo, Wanachama wa CCM 50 walihamia Chadema.

Katika Mikutano yote hiyo, viongozi wa Chadema, walifungua Mashina na Ofisi za Chadema, na kuwataka wananchi waachane na Propaganda za CCM za kukifanyia Usaliti chama chao badala ya kuwatatulia Kero, hivyo wakipe ridhaa Chadema 2014.

“Wakati CCM kimeacha kushughulikia Sera Mbovu za Wakulima na Wafugaji na badala yake kueneza Usaliti ndani ya Chadema, tumejikita kutatua kero zenu na maazimio ya ajenda sita za chama, ikiwa ni pamoja na bei ya Umeme inayowanyonya na kuwaumiza, na Katiba”.alisema Msigwa.

 “Tuko  madiwani 5 Tarafa ya Turiani, na wote tuna wananchi na Wafanyakazi wanaodhulumiwa haki zao za Malipo  ya Miwa na mishahara, lakini ninayehangaika na kupambani kugombea haki zenu ni mimi tu, wenzangu wametulia, ichagueni chadema”. Alisema Mwakambaya.

Wanawake Msiwe na Woga kudai haki yenu, fahamuni kuwa wakati wa kila manyanyaso ya Mapigano ya Wafugaji na Wakulima, Njaa, na dhuluma za Mishahara, Athari za Kubomolewa Nyumba na kuhamisha na hata gharama ya Umeme, waathirika wakubwa ni akina Mama na Watoto, ichagueni chadema” alisema Petro.


Bryceson Mathias
Mvomero

No comments: