Kuna Wachina wamekamatwa na Shehena
Kubwa ya Meno ya tembo Bandarini Dar es Salaam na sasa wamechukuliwa kisiri na
"watu flani" ambao hawataki habari hii ijulikane.
Ilikuwa ni meli
ya kijeshi ya China ambayo ilikuwa imeegesha gati namba 3 baada ya kuwa nchini
katika shughuli za kawaida za ushirikiano katika kudhibiti maharamia (Pirates).
Katika kuuficha mzigo kwa kudai magari yamebeba chakula ndipo wakashtukiwa.
Chanzo chetu
kinatufahamisha kuwa Wametiwa pingu na wanajeshi wa JWTZ na TISS na wamepelekwa
Ukonga na msafara wa magari mawili yakiongozwa na pikipiki za Polisi.
Hata walipo
tuna chanzo chetu ambacho kitaendelea kutujuza kinachojiri.
Namna yoyote ya
kuzima huu ujangili italeta balaa kubwa si kwa vyombo vya dola tu bali hata
kuitia doa serikali kwa ujumla. Msifiche, waanike ili waueleze umma nani yupo
nyuma yao!
KUTOKA CHANZO CHETU -
WAJARIBU KUHONGA 25 MILLION, WAKUTWA NA TANZANITE PIA!:
Sakata la Wachina na kukutwa na Nyara za
Serikali limeendelea kuchukua sura mpya ambapo Wachina wawili walifika
bandarini wakitaka kuwasailimia ndugu zao ambao ni Wanajeshi.
Walipofika getini, kwakuwa tayari wanajeshi
wa JWTZ waliishaimarisha ulinzi baada ya tukio la jana yake (usiku wa kuamkia
leo) na meno ya tembo. Wanajeshi walitaka kuwakagua Wachina hao wakagoma na
ndipo wakapekuliwa kwa lazima na kukutwa na madini aina ya Tanzanite. Wakaitwa
maofisa wa Nishati na Madini na polisi wakawachukua!
Tukio la awali lilikuwa la jana Jumatatu saa
3 usiku wa kuamkia Jumanne (leo) ambapo gari moja binafsi likisindikizwa na
gari la Polisi na mtu mmoja mwenye sare za Polisi lilifika katika lango la
bandari eneo la geti namba 2 wakielekea geti namba 3 iliko meli ya kijeshi ya
Kichina yenye wanajeshi takribani 600.
Katika gari la kiraia kulikuwa na Wachina
watatu; wawili wanajeshi na mmoja raia na dereva Mtanzania.
WACHINA walitaka kuwapa walinzi rushwa ya sh
milioni 25 baada ya walinzi kukuta kuna vipande 81 vya meno ya tembo.
Walinzi waligoma na kulazimisha kulikagua
gari. Kuona hivyo gari la Polisi na mtu aliyevaa sare za polisi wakatoweka na
wale wanajeshi wawili wa Kichina wakatoweka na kukimbilia katika meli yao ya
kijeshi na kujichanganya na wenzao.
Ndipo walinzi walipowasiliana na wanajeshi na
Polisi na wakaja wanajeshi na maofisa Usalama wa Taifa wa Tanzania ambao
waliwachukua Mchina na dereva Mtanzania na kuondoka nao.
Tunaendelea kufuatilia zaidi kuwafahamisha
kinachojiri
No comments:
Post a Comment