Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, November 11, 2013

Wanafunzi 200 wasoma darasa moja

     SHULE ya Msingi Kongowe wilayani Kibaha, Pwani, inakabiliwa na uhaba wa madarasa jambo linalosababisha wanafunzi 200 kukaa katika darasa moja. Akielezea changamoto za shule hiyo wakati wa kukabidhiwa mabati 40 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Beatus Lingumbuka, alisema shule hiyo kwa sasa inahitaji vyumba nane vya madarasa, ili kukabiliana na changamoto hiyo. “Halmashauri inatujengea chumba kimoja na wananchi wanajenga vyumba viwili, hapa inahitajika msaada zaidi, kwani katika halmashauri ya mji wetu wa Kibaha hakuna shule yenye mlundikano mkubwa wa wanafunzi kama hii,” alisema. Alimshukuru meneja wa TRA kwa kuwasaidia mabati hayo na kofia za kujengea ambazo zitasaidia kuezeka vyumba vya madarasa vinavyojengwa na wananchi na kuwezesha wanafunzi kuvitumia.

      Meneja wa TRA mkoani Pwani, Highness Chacky, alisema wametoa msaada huo baada ya kupata taarifa ya changamoto ya shule hiyo na kuamua kutumia Wiki ya Mlipakodi kufikisha msaada huo. Mbali na msaada huo, vifaa tiba pia vilitolewa katika Wilaya ya Mkuranga, na Shule ya Msingi Kiluvya ilisaidiwa ukarabati wa darasa lililoezuliwa na mvua. Katika hatua nyingine, gazeti la Tanzania Daima na Radio Clouds walipata vyeti kutokana na kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo mkoani Pwani. Pia washindi watatu kutoka kila wilaya walipata vyeti kutokana na kutokuwa wasumbufu katika zoezi la kulipa kodi.

Source: Mkireri j. (Nov. 2013).Wanafunzi 200 wasoma darasa moja. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: