Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa
yuko Ulaya, nchini Ujerumani kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, kuanzia Novemba
7, mwaka huu, katika mji wa Bensheim, Makao Makuu ya Shirika la Kimataifa la
Kimataifa la CBMI Mshirika mkuu wa Taasisi ya CCBRT ambayo yeye Dkt. Slaa ni
mwanzilishi na Mwenyekiti wake.
Ni kwamba CCBRT kwa ajili ya
kuboresha huduma zake, ipo kwenye mpango mkubwa wa upanuzi, kwa kuanzia
na
Baobab Hospital, mother and Child
yenye vitanda 200 itakayokuwa na huduma zote za kisasa,
Ujenzi wa Private Clinic ambayo
unaweza kuanza wakati wowote, na; Staff Housing na Hostel. Kutakuwa na jumla ya majengo sita
hivi yenye ghorofa nne kila moja. Mambo hayo yote yanakisiwa kugharimu
zaidi ya Euro 150 million.
Hivyo Bodi ya CCBRT na Bodi ya CBMI
watakuwa na mkutano wa siku mbili katika mji wa Bensheim, dk 45 kutoka jiji la
Frankfurt, Ujerumani.
Lengo kuu la mkutano huo ni
pamoja na kupitia mikataba mbalimbali ya pande hizo mbili na kutengeneza mpango
mkakati wa pamoja katika upanuzi huo mkubwa ambao unalenga kubadilisha sura ya
huduma kwa mama na mtoto katika jiji la Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment