Dr. Slaa si mtu mwenye maneno mengi, ni mtulivu
na mkimya kiasi chake, lakini akipanda jukwaani na kuanza kulishambulia huku na
kule huwezi kuamini kinachotoka ubongoni mwake. Kimya kingi kina mshindo.
Wengi hawamfahamu Dr. Slaa vilivyo, wengi
wanamwona sasa baada ya kuingia bungeni na sasa katika majukwaa ya siasa,
ukweli ni mtu mbunifu, mpenda maendeleo na mwenye kujitoa kwa ajili ya wengine
bila kujibakiza. Ufahamu wangu wa huyu Dr. Slaa ni wa muda mrefu, lakini wengi
wetu wanachukulia mambo ya juu juu tu bila kujua undani na utendaji uliotukuka
wa mtu huyu.
Machache kati ya mengi kuhusu Dr Slaa kabla ya
kuwa mwanasiasa, kuwa Mwanasiasa na hatimaye kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, ana
mlolongo wa mambo mengi ambayo yanaonyesha ubunifu wa hali ya juu, na pia
mwepesi kuwaelewa vijana na kuendana nao tofauti na watu wengine wa kizazi
chake.
Pamoja na kuwa mwanachama wa CCM, baada ya
kuombwa na Wanakaratu agombee ubunge kule baada ya kuchoshwa na mbunge aliyekuwepo
wakati huo, CCM iliendelea na mizengwe ile ile kama iliyotokea juzi pale Dodoma
kuwaengua watu wanaofaa kwa uongozi. Wanakaratu wakiamua hawataki longolongo,
wakamsihi kwamba wameamua awe mbunge wao na wakamwomba achague chama kingine
agombee kwani hawamtaki kabisa mbunge aliyepo. Kwa ridhaa ya wananchi akaamua
kujitoa CCM na kujitosa kujiunga na Chadema ili agombee ubunge kuridhia matakwa
ya wanakaratu.
Kabla ya kuwa mwanasiasa
kuna mengi ya maendeleo ambayo wengi tunayaona
huku tusijua kama Dr. Slaa ndiye aliyebuni na kuyaendesha kama ifuatavyo.
1. Dr. Slaa ndiye amekuwa wa
kwanza Tanzania kuagiza big truck for load and unload makontena bandari ya Dar
es Salaam wakati akiwa Katibu Mkuu TEC. Ilikuwa ni miaka ya 1980th, hakukuwa
hata kampuni au watu binafsi waliothubutu kufanya hivyo. Truck hilo lilikuwa na
crane za kupakia na kupakua bila taabu kokote linalokifkishwa container na kwa
truck hilo. Baadaye makampuni yakabembeleza wauziwe gari ile, ndipo Barala La
maaskofu likawauzia.
2. Kwa mara ya kwanza baraza la
Maaskofu Tanzania lilipoanza kuwa na matumizi ya computer ikiwepo ofisi yake Dr
Slaa kama katibu Mkuu, na taasisi za upashanaji habari ambazo zilikuwa chini ya
uongozi wake ikiwa ni pamoja na:
◦ Gazeti la kiongozi kuanza kutumia mfumo wa computer katika idara ya
set up
◦ TMP (Tanganyika Mission Press) Kipalapala idara ya uchapishaji
(printing) wakitumia Apple computers.
◦ TMP Book deparment Tabora mjini) idara ya maduka ya vitabu na
usambazaji vitabu wakitumia Apple computers
◦ TAPRI idara ya tungo za mawasiliano vitabu TEC iliyokuwa na ofisi zake
Seiminari kuu Kipalapala Tabora.
NB.
Wakati huo chuo pekee cha mawasiliano
(journalism) Tanzania kilikuwa ni Nyegezi-Mwanza pekee kilichokuwa kikiongozwa
na AMECA (Balaza la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati kimoja kikiwa
Kitwe - Zambia, cha Nyegezi kiliendeshwa na TEC Dr. Slaa akiwa msimamizi mkuu
kama Katibu Mkuu.
Dr. Slaa atakumbukwa sana kwa makubwa aliyofanya
kujenga na kuikuza TEC
1. Makao makuu ya Baraza la
Maaskofu Tanzania (TEC) tunayoona siku hizi ni matunda ya ubunifu wa Dr. Slaa
alipokuwa Katibu Mkuu pale. Jengo la awali ni lile lililo upande wa mbele
zinapotumika ofisi siku hizi ambapo yalikuwa madarasa ya shule ya sekondari ya
Masisita Tanzania, ambayo baadaye ilihamishiwa Bigwa Morogoro kupisha kiwanja
hicho kuwa makao ya Maaskofu Katoliki Tanzania, awali yalikuwa pale ofisi za
St. Joseph, Dar es Salaam. TEC aliyoikuta DR. Slaa ilikuwa na jengo hilo la
madarasa na jengo lilolokuwa la utawala wa shule. Dr. akabuni majengo ambayo
tunayoana sasa, hata kama hayakukamilika yote waliofuata walikamilisha kazi
alioyoianza.
2. Kaone maendeleo na majengo
katika jimbo la Mbulu ni jitihada za Dr. Slaa na Fr. Narda ambao kwa pamoja
walifanya makubwa.
3. Kaangalie jimboni kwake
huduma za kijamii ambazo amezifanya, utachoka mwenyewe kiasi ambacho CCM
imekimbiwa kabisa huko sababu utendaji wa Slaa huko na CCM ni sawa na
kulinganisha mlima na kichuguu.
4. Dr. Slaa kwa tunaomfahamu ni
mwanamapinduzi na mpenda maendeleo, na pengine mengi alikuwa anayafanya
yakaonekana mapya mno kwani alikuwa anaona mbali kuliko hawa wakubwa wake, ila
sipendi kuliongelea sana hilo.
Chadema yaimarika baada ya Dr. Slaa kuwa mgombea
urasi uchaguzi Mkuu uliopita.
Siyo siri Chadema hakikuwa na nguvu tunayoona
sasa hivi licha ya kuwa na sera nzuri, lakini leo tunaona nguvu ya Chadema
inayoogopewa mno na CCM ni kutokana na Chadema katika dakika za majeruhi kuamua
kumwangukia Dr. Slaa agombee urasi ambao Samweli Sitta aliingia mitini baada ya
makubaliano nao. Tangu hapo Chadema imekuwa na nguvu ya ajabu.
Je, vijana hao waliokuwemo ndani ya Chadema kabla
ya Dr. Slaa kugombea Urais kwa nini hawakuipaisha juu Chadema kama sasa? Baada
ya Dr. Slaa kuipaisha Chadema juu sasa tunakuja na kauli mbiu ya kubeza makubwa
yaliyofanywa na hawa mnaowaita kizazi cha kabla ya uhuru. Hapana tuwe
waungwana, pamoja na kila mmoja kuwa na haki za kugombea nafasi tusigeuze uhuru
huo kuwabeza hawa ambao wametufikisha tulipo, na bado tunahitaji mchango wa
ushauri, uongozi, hekima na busara zao. Uongozi bora ni kuchanganya mapya na ya
kale kwani viatu vya zamani vyaijua njia.
Ubunifu wa Chadema viongozi wakiwa mojawapo
waliozaliwa kabla ya Uhuru Dr Slaa na Kamanda Mbowe:
◦ Dr. Slaa ndiye mbunge ambaye baada ya kuingia bungeni alianza
kuchangamcha kwa kuichambua serikali na kasoro zake kitu ambacho katika mabunge
yaliyotangulia wabunge walikuwa ni rubber stamp ya serikali.
◦ Chadema wakiwemo hao unaoona walizaliwa kabla ya uhuru wamebuni mapya
katika shughuli na kampeni za uchaguzi Tanzania kuwa zenye mvuto kuanzia
mkuktano wa ufunguzi wa kampeni uchaguzi Mkuu uliopita ulifanyika Kidongo
Chekundu baada ya Dr. Slaa kushusha makumbora mazitomazito kuituhumu serikali,
watendaji wa serikali na CCM, tuhuma ambazo CCM wanazidi kubabaika kuwanyoshea
kidole wahusika kisha kuwakumbatia tena hivi karibuni kule Dodoma.
◦ Mkutano wa Kidongo chekundu Dar es Salaam ndio ulioanza kutufungua
macho na masikio Watanzania na kuanza kujifunza elimu ya uraia ambayo tulikuwa
tunazibwa na CCM tusiijue.
◦ Dr. Slaa ndiye aliyetufunza na kutufunua kwamba raia wanayo nguvu ya
kuiadabisha serikali haki zao za msingi zinapokiukwa kwa kauli mbiu ya nguvu ya
umma (peoples power).
◦ Utumiaji wa chopper kufikia maeneo magumu kufikika kwa magari na
kurahisisha kazi ya kampeni, CCM wakaiga.
◦ Kuwa na magari yanayotumika kama majukwaa ya mikutano badala ya
kupoteza gharama na muda kujenga majukwaa yatakayotumika kwa dakika chache.
Ilani ya Uchaguzi Chadema ndiyo inayotumika na
yenye uzito sasa hivi:
◦ Fukuto la Katiba mpya linaloendelea sasa nchini ni uzao wa ilani ya
Chadema na ilani ya Dr Slaa kwamba kinachofuata baada ya Uchaguzi mkuu ndani ya
siku 10
◦ Kikwete kufanya mabadiliko ya barala la mawaziri mara kadhaa ni
kutokana na shinikizo la wabunge wa Chadema bungeni.
◦ Serikali kubana matumizi ya ziada ili kuokoa pesa za walipa kodi
Kuna mengi tu wachangiaji wengine watachangia, ni
dhana potovu kuwa na fikra za aina hiyo na kuwabeza wabunifu wa mengi,
waliongoza nchi hii, wenye kuturithisha mengi kwa uzoefu na busara zao na
walioongoza nchi hii hadi kuwa na utulivu wa aina yake. Leo vijana mnaowasema
yanayojilia ni amani kusambaratika na mauaji ambayo ilikuwa hadithi za
kusimuliwa kutoka nchi nyingine, leo serikali ya CCM inayoongozwa na Rais kijana
kuliko Rais mwingine aliyemtangulia imetwishwa na aibu kubwa ya kitaifa na
kimataifa ya mauaji ya raia wasio na hatia.
Kuna nchi ambazo ni kielelezo cha vijana ambao
mimi ningewaita watoto kukabidhiwa madaraka ya kuongozia nchi na kusababisha
maafa makubwa kwa nchi husika kama Liberia, Ujerumani chini ya Hittler, na
kinachoendela huko Zaire ya sintofahamu. Vijana achaneni na uroho wa madaraka, vema kubaki
watumishi na watendaji wazuri serikalini na vyamani kujifunza mbinu za uongozi
na kupata uzoefu katika kuongoza nchi.
Kuongoza nchi hakuna shule wala kitabu cha
kusomea au chuo. Hekima na busara ya mtu ndio kielelezo cha fanaka katika
kuongoza nchi.
◦ Vijana wana papara,
◦ wanataka njia ya mkato,
◦ pagumu wanataka kulazimisha bila busara wala kutumia akili
◦ Vijana wanalipuka kama moto wa gas
◦ mambo yakigeuka magumu ni mabavu hutumika.
Imeandikwa na Candid Scope

No comments:
Post a Comment