TAARIFA KWA UMMA/WADAUTAREHE 15
OKTOBA 2013
MKUTANO WA BARAZA LA UONGOZI LA KANDA YA KASKAZINI NA WADAU WA
CHADEMA WAPENDA MABADILIKO NA UHURU WA KWELI.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini kinapenda
kuwatangazia na kuujulisha umma na wadau wote kutoka mikoa ya Tanga,
Kilimanjaro, Manyara na Arusha kuwa tarehe 25 hadi 27 Oktoba 2013 katika JIJI
la Arusha yalipo makao makuu ya chama kwa kanda, kuwa kutafanyika mkutano wa
Baraza la Uongozi la Kanda tarehe 25 Oktoba, ambalo litajumuisha viongozi wa mikoa na mabaraza ya chama ngazi ya
mikoa kutoka kanda ya kaskazini, Wabunge wote kutoka mikoa ya kanda ya
kaskazini, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri zilizopo chini ya CHADEMA kutoka
kanda ya Kaskazini na wajumbe wa kamati kuu wanaoishi ndani ya kanda ya
kaskazini.
Sambamba na mkutano huu wa baraza la uongozi, tarehe 26 na 27
Oktoba, utafanyika mkutano wa wadau wote wa chama na wapenda mabadiliko ya
kweli kutoka kanda ya kaskazini. Wadau hawa ni pamoja na wanasheria wote,
wachumi, wahasibu, wahandisi, wahadhiri wa vyuo na waalimu, wanahabari,
wafanyabiashara, viongozi wa dini na makundi yote maalumu na ya kitaaluma, wote
wanaalikwa kushiriki katika mkutano huu ambao una lengo la kutoa fursa kwao
kama watanzania wakiwa kama wadau wa kweli waweze kuitumikia nchi yao kupitia
CHADEMA.
Katika mkutano huu wadau watapata fursa ya kushirikishwa katika
nafasi za kimaamuzi na kiutendaji za kanda kwa lengo la kuijenga na kuiimarisha
CHADEMA ambayo imekuwa na imeendelea kuwa tumaini kwa Watanzania kwa wakati huu
wa uhitaji mkubwa wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.
Mkutano huu utafunguliwa na pia kuhudhuriwa Mwenyekiti wa CHAMA
Taifa Mhe Freeman Mbowe (MB) ambaye pia ni mbunge kutoka Kanda ya Kaskazini.
MAWASILIANO yote yafanyike kupitia kwa MRATIBU - KANDA
Ofisi ya KANDA – ARUSHA –
Ngarenaro: NHC Nyumba Na. 8. S.L.P. 12525, Arusha, Tanzania. Simu: +255 784 343 275, Email: chademakaskazini@gmail.com Tovuti: www.chadema.or.tz
Wadau wote mnakaribishwa sana kuhudhuria mkutano huu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ushiriki kwenye mkutano huu tafadhali tumia mawasiliano kwa njia zifuatazo:
Simu: +255 758 976 260
+255 656 557 586
+255 755 282 878
Barua pepe: chademakaskazini@gmail.com / golugwa@gmail.com
Imetolewa leo tarehe 15 Oktoba 2013
Amani S. Golugwa
KATIBU – KANDA YA KASKAZINI
No comments:
Post a Comment