Akielekea
ukingoni mwa safari yake, Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa ameacha
historia nchini Marekani kwa kuonyesha kukubalika kwa kiwango kikubwa miongoni
mwa viongozi wa ngazi mbali mbali nchini humo. Kutokana na msimamo wake dhidi
ya ufisadi, busara, sera zake na chama chake, Dr. Slaa ameidhiirisha siyo umma
wa Kitanzania na Kimarekani, bali dunia kwa ujumla ya kwamba ni kiongozi ambaye
yuko Tayari kuliokoa taifa la Tanzania na bara la Afrika.
Gavana
wa Jimbo la Indiana katika Kipindi chake cha Radio Jijini Indianapolis ,
amesema kwamba ili Afrika iondokane na maradhi, ujinga, na umasikini, viongozi
kama Dr. Slaa ndio dawa. “ I was amazed and humbled to meet such a visionary
man. My huts off to him. He is a brilliant and a visionary fellow whose time
has come. He is a hero of our time. I can’t imagine how difficult it must have
been for him to campaign under police horrific bombings” alisema governor
Pence.
Dr.
Slaa ameonyesha kiu ya maendeleo, na sisi kama taifa inayoipa elimu kipaumbele,
ni lazima tuwe tayari kumpa huyu kiongozi wa kipeke mkono ili atayarishe nguvu
kazi ya kesho. Ni aibu kiongozi kama huyu mzalendo kubughudhiwa na vyombo vya
dola kwa sababu tu ni mpinzani wa chama iliyopo madarakani.
Viongozi
wengi barani Afrika wamesahau kwamba elimu ndiyo ukombozi wao. Dr. Slaa
ameonyesha njia ya kulikomboa nchi yake aliongeza gavana Pence. Kadhalika
wachangiaji mbali mbali walioshiriki katika kipindi hicho, walionekana
kumkubali Dr. Slaa mpaka kumfananisha na Nelson Mandela pamoja na Kwame Nkurumah
Katika
kipindi kifupi akizunguka katika majimbo tofauti nchini marekani, Dr. Slaa
ameonyesha uchungu na nchi yake. Kadhalika ameonyesha umahiri mkubwa kusimama
na kupigania haki, licha ya kufanya hivyo katika mazingira magumu na kandamizi.
Ameweka wazi msimamo wake, kwamba kamwe Afrika lazima ijiondoe
katika biashara kandamizi na pia kuweka wazi msimamo wake wa kutokukukubali
misaada ya kigeni isipokuwa biashara itakayo wanaufaisha wananchi wake na sawa
na mwekezake. Siyo biashara inayoegemea upande mmoja.
2 comments:
Nabii hatambuliki kwao.....
Dr. Slaa kama tusipo ku support tayari Mungu amekukubali na endeleza kupigania haki za taifa, Tanzania ni Nchi kama zingine na mabadiliko haya epukiki
Post a Comment