Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema kwa sasa haina fedha za kutekeleza agizo la Kamati ya Hesaba za Serikali (PAC) la kurudia upya zoezi la utoaji wa hati za ardhi, pamoja na kuziweka katika mfumo wa kielektroniki badala ya mfumo wa karatasi (analojia). Hayo yalisemwa na Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Anna Tibaijuka, wakati akizungumza na NIPASHE muda mfupi baada ya kufungua kongamano la kimataifa la haki ardhi kwa amani endelevu, jijini Dar es Salaam jana. Aidha Tibaijuka aliwaomba wajumbe wa PAC waipiganie Wizara ya Ardhi iongezewe fedha katika bajeti ijayo ili iweze kutekeleza agizo hilo kwa haraka zaidi.
Agosti 21, mwaka huu PAC kupitia mwenyekiti wake Zitto Kabwe, iliiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kurudia upya zoezi la utoaji wa hati za ardhi zote, pamoja na kuziweka katika mfumo wa kielektroniki badala ya mfumo wa karatasi. Hatua hiyo ilifikiwa baada ya kamati hiyo kugundua kuwa zaidi ya viwanja 7,000 nchini vipo katika rekodi lakini havionyeshi vinamilikiwa na nani. Zitto alisema zaidi ya viwanja 160 vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 500 vilivyopo jijini Dar es Salaam havina rekodi huku vikionyesha vimenunuliwa. Alisema kwa mwaka wa fedha uliopita, Wizara hiyo ilipangiwa kukusanya Sh.bilioni 96 lakini ilikusanya bilioni 20 sawa na asilimia 21 kitendo kilichosababisha kuongeza kodi ya ardhi ili wafikie kiwango walichopangiwa.

Source: Ippmedia (Sept. 2013). Wizara ya Prof. Tibaijuka yashindwa kutekeleza agizo la wabunge. Retrieved from Ippmedia/Nipashe
No comments:
Post a Comment