Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, September 11, 2013

Profesa atahadharisha mchakato Katiba mpya


       
Mhadhiri wa Chuo Kikukuu cha
Dar es Salaam,  Profesa Chris Maina
Mhadhiri wa Chuo Kikukuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Maina, amesema kuna hofu ya kuwa na Katiba yenye mtazamo wa chama kimoja cha siasa kutokana na utaratibu uliowekwa wa wajumbe wanaotakiwa kushiriki kwenye Bunge la
Maalumu la Katiba.  “Kuna hatari ya kupatikana kwa katiba ya chama kimoja cha siasa mfano kulinangana na idadi ya wajumbe wa Bunge la Katiba asilimia 72 watakuwa wabunge kutoka chama tawala,”alisema Maina. Alitoa angalizo hilo wakati wa mkutano wa wataalam wa masuala ya Katiba wakiwamo maprofesa ambao ni magwiji wa Katiba kutoka Tanzania na nchi jirani unaofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefadhiliwa na mashirika ya Konrad Adenaure Stiftung na Friendrich Abert Stiftung.

      Profesa Maina alisema katika Bunge hilo, wabunge wote 357 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambao idadi yao ni 81 watakuwa wajumbe wa bunge hilo huku wananchi wa kawaida wakiwa ni 166 tu. Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, amewataka wabunge na wawakilishi wanaotaka kuingia katika Bunge Maalumu la Katiba, wajiuzulu kwanza ubunge. Kibamba alisema  kimsingi wananchi wengi hawataki kuona mbunge yeyote aliyopo Dodoma au Baraza la Wawakilishi anakwenda kushiriki kwenye mkutano wa Bunge la Katiba kwa sababu siyo kazi yake ambayo alitumwa na wapiga kura wake. Kwa upande wake, Kamishina wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, alisema Tume haitahusika katika suala la Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu kazi yake itakuwa imekoma.

Source: Mwanakatwe T. ( Sept. 2013). Profesa atahadharisha mchakato Katiba mpya. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: