Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, September 10, 2013

Mbunge Lema akemea dini kupokea fedha chafu


  Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amewataka waumini wa dini kujifunza wajibu wao wa kutoa sadaka nzuri na kuacha kupokea fedha chafu. 
Alisema hayo mwishoni mwa wiki akiwa mgeni rasmi wakati wa harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Parokia ya Mtakatifu Francis Xaver, iliyopo Olosipa eneo la Sakina kwa Iddi.  Katika harambee hiyo, jumla ya Sh. 43,034,900 zilipatikana ikiwa ni ahadi na fedha taslim. Lema alisema Tanzania ina wafanyabiashara wengi wenye uwezo mkubwa, lakini wengi wao biashara zao haziendi katika mazingira ya Mungu.

       “Wapo wanasiasa ambao hawana sifa mbele ya jamii...kutoa kwa Mungu siyo hasara bali ni baraka kubwa. Kuna wakati mambo ya msingi hayafanyiki siyo kwa sababu hakuna fedha ila ni kukosa vipaumbele,” alisema.  Naye Makamu wa Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Padre Simon Tenges, alisema Mfuko wa Maendeleo wa Parokia hiyo, unatarajia kujenga nyumba ya mapadre, shule, zahanati na chuo cha ualimu. Alisema ujenzi wa nyumba ya mapadre ambao kwa sasa wanaishi kwenye nyumba za kupanga, utagharimu Sh. milioni 120. Alisema tayari wamechimba kisima kwa gharama ya Sh. milioni 30 ambacho kinahudumia kaya zipatazo 500.

Source: Ngunge J. (Sept. 2013). Mbunge Lema akemea dini kupokea fedha chafu. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: