Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, September 20, 2013

MAANDAMANO YAKO PALE PALE KESHO SEPTEMBER 21, 2013


Pamoja na Kamanda Kova kuongea jambo ambalo halieleweki la kuzuia Maandamano ya Kesho tarehe 21September 2013. Viongozi wa Vyama vya Upinzani wamesisitiza Maandamano yako palepale na hakuna wa kuyazuia wala sababu ya kuyazuia haipo.

Kama ujio wa Obama wa siku moja tu ulifunga barabara kwa siku tatu sembuse Katiba yetu sisi Watanzania!!? Je Oboma ni bora zaidi kuliko Katiba yetu??

Kova na wenzako mkumbuke popote mlipojaribu kuingilia mambo ya kisiasa nchini mliua au mliwaacha watu vilema au yote mawili kwa pamoja. Tumieni busara ila uminyaji huu wa demokrasia hauwezi kukubalika hata kidogo wala damu ya Watanzania haiwezi kuchezewa kwa ulevi tu wa madaraka na ukosefu wa busara na hekima wa viongozi wa Jeshi la Polisi.

Maandamano yataanzia kwenye vituo viwili ambavyo ni Tazara na Ubungo kuelekea Jangwani yakiongozwa na viongozi wakuu wa vyama vyote vya Upinzani ambapo kutakuwa na Mkutano Mkubwa ambao haujawahi kufanyika katika historia ya siasa za nchi hii.

Taasis mbalimbali hapa nchini zitashiriki katika Mkutano huo ambazo ni pamoja na Jukwaa la Katiba, Shura ya Maimau, CCT,TEC, SHIVYAWATA, TGNP, Vyama vyote vya Upinzani vyenye usajili hapa nchini n.k

Maandamano yataanza saa tatu kamili asubuhi

NGUVU YA MAJESHI HAIJAWAHI KUSHINDA NGUVU YA UMMA

No comments: