![]() |
| Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini (Tamwa), Valerie Msoka. |
Semakafu alisema katiba iweke na chombo maalum cha kusimamia haki za watoto na wanawake kwa kuwa rasimu haijaonyesha, hivyo kwa kuzingatia suala hilo utaratibu utawekwa wa kuunda tume itakayosimamia na kuhakikisha viongozi na wananchi katika ngazi zote wanaitekeleza ibara hiyo. Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini (Tamwa), Valerie Msoka alisema Katiba itaje umri kamili wa mtoto na muda rasmi wa kuruhusiwa kuoa au kuolewa. Pia alitaka itaje kiwango cha haki ya elimu kuwa mpaka kidato cha nne pamoja na kutoa mazingira rafiki ya kumwezesha watoto wa kike kupata elimu kwa usalama zaidi. Kwa upande wake, mjumbe kutoka Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika, Matrina Kabisana alisema rasimu haijatoa haki ya kuishi kwa asilimia 100, kwani bado haijaweka kipengele cha kukataza adhabu ya kunyongwa mpaka kufa (kifo).
Source: Ippmedia (August 2013).Wanawake wataka Katiba iainishe usawa. Retrieved from Ippmedia/ Nipashe
Source: Ippmedia (August 2013).Wanawake wataka Katiba iainishe usawa. Retrieved from Ippmedia/ Nipashe

No comments:
Post a Comment