Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA kimezidi kuonyesha umwamba wake kwa chama cha Mapinduzi baada ya
kukibwaga vibaya kwenye uchaguzi wa kijiji Kondoa Kusini.
Uchaguzi huo ulifanyika jana katika
kijiji cha Mlongia Kata ya Jangalo.Katika matokeo yaliyotangazwa muda mfupi
uliopita mgombea wa Chadema ameibuka mshindi kwa kupata kura 184 dhidi ya 96 za
CCM.Mgombea wa CUF ameambulia kura 9.Huu ni ushindi wa asilimia 64% kwa
Chadema.
Mbunge wa Jimbo hilo ni Juma Nkamia
wa CCM ambaye mara kadhaa amekuwa akiibeza na kuishambulia Chadema awapo
bungeni.
Huu ni ushindi mkubwa kwa wanamageuzi
kwani kijiji cha Mlongia ni kati ya vijiji vilivyoko ndani kabisa mkoani
Dodoma.
Molemo/JF
No comments:
Post a Comment