MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika, (Chadema) ameitaka jamii kupaza sauti juu ya mwenendo wa mchakato wa Katiba Mpya ili kuepusha mianya inayoelekea kuvuruga mchakato huo. Mnyika alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa vijana waliochujwa katika Mabaraza ya Katiba ya Kata Wilaya ya Ilala. Alisema kuna kila dalili zinazoashiria mchakato huo kuvurugwa na mkono wa serikali iliyopo madarakani kwa sababu ya kuwapo kwa shinikizo la kupitisha sheria ambazo zinampa mamlaka zaidi Rais kuingiza mkono wake katika mchakato unaoendelea sasa. “Jamii inabidi ipaze sauti kwa hili kwani ni dhahiri kwamba mchakato huu unaelekea kuvurugwa, kwa mfano kuna miswada miwili inayopelekwa katika bunge hili linaloendelea, ambayo ina msukumo ya kupitishwa haraka ili iwe sheria kamili ambazo rais ataitumia kuingiza nguvu yake ndani ya mchakato huu,”alisema Mnyika.
Source: Magege E. (August 2013). Mnyika ahofia
Katiba mpya kuvurugwa. Retrieved from Mtanzania

No comments:
Post a Comment