Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Wednesday, July 10, 2013

Wilfred Lwakatare alazwa Muhimbili,Aomba Watanzania Wamuombee

Lwakatare akiwa hospitalini leo

Tangu Jana Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Kamanda Alfred Lwakatare amelazwa hospitali ya Muhimbili(Pichani).Nanukuu maelezo yake hapa

‘’Mkirejea tatizo la kiafya nililolipata nikiwa Central Police baada ya kukamatwa; la kuumwa sana na mgongo/mkono na baadaye nikiwa gerezani Segerea nilipelekwa Muhimbili Moi na baada ya vipimo (M.R.I) wakabaini kuna ulazima wa kufanyiwa upasuaji. Tatizo hili limeendelea na hata baada ya kutoka Segerea na nimekuwa nikiwaona madaktari kwa ukaribu. Jana mchana,imelazimu kulazwa hospitali ya Muhimbili ward ya Sewahaji NO.18,chumba No.024 kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Kama ilivyo kawaida yetu; Tunaanza na Mungu,Tunaendelea na Mungu na kumaliza na Mungu.

Tuzidi kuombeana na yote tumkabidhi Mungu.
Nawapenda sana!’’

Ofisi ya Katibu Mkuu imetuma timu kutoka makao makuu muda mfupi uliopita wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Mzee Victor Kimesera ambayo ilienda kumjulia hali.Taarifa Rasmi itatolewa na msemaji wa chama

Kipindi chote alichoshikiliwa kwa makosa ya kubambikiza kimechochea tatizo kubwa alilokua nalo kiafya.

Tunaomba tuungane tena katika hili kama tulivyoungana katika kipindi chote cha kesi

No comments: