Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, July 23, 2013

Wanasheria wamuunga mkono Mbowe




  MVUTANO kati ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, na Jeshi la Polisi nchini umechukua sura mpya baada ya wanasheria kadhaa mashuhuri nchini kukosoa hatua ya jeshi hilo kutumia mamlaka yake kumlazimisha mwanasiasa huyo kuwasilisha ushahidi anaodaiwa kuwa nao. Mmoja wa wanasheria wakongwe hapa nchini na ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alisema kuwa polisi wangekuwa na haki ya kutumia kifungu cha sheria kinachomlazimisha mtu kuwasilisha ushahidi polisi, katika mazingira mengine. Mwanasheria huyo alisema katika tukio ambalo polisi wenyewe ni watuhumiwa, hawawezi tena kutumia sheria hiyo kumlazimisha mtu anayewalalamikia kuwakabidhi ushahidi uwe ni wa nyaraka au kitu kingine chochote.


       “Ni kweli sheria waliyoinukuu polisi (kifungu na 10 (2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura ya 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002) inawapa uwezo polisi kumwamuru mtu kuwasilisha ushahidi kwao. “Lakini lazima pia tujue kuwa hii ni kwa yale mazingira ambayo mtu mwenyewe hana tofauti au kusigana na jeshi hilo. Lakini, hawawezi kutumia tena sheria hii kwa sababu wao nao ni watuhumiwa,” alisema. Badala yake, alilishauri jeshi hilo kuacha kutumia mabavu kumshinikiza Mbowe na liachie mamlaka za juu kuunda tume ambayo itaweka mambo yote hadharani. “Katika hali ya sasa ya mvutano, ni bora kwa jeshi letu kukubali changamoto kama hizi na wala halitaonekana kuwa linahusika, bali litaonyesha ishara ya ukomavu zaidi katika utendaji na pia kutoa fursa kwa vyombo vingine kuchukua nafasi yake,” alisema.

        Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wake wa Makosa ya Jinai Julai 17, mwaka huu, lilimwandikia Mbowe barua yenye kumbukumbu namba AR/IR/6223/2013 ikimtaka kupeleka ushahidi wake leo kabla ya saa nane mchana, kiongozi huyo amewataka polisi kumpeleka mahakamani kwani hatawapa ushahidi huo. Mbowe hata hivyo, alisema kamwe hawezi kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake kilichoamua kutoukabidhi ushahidi huo polisi hata kama watawapa vitisho kama walivyozoea.
Alisema CHADEMA ilimwandikia Rais Jakaya Kikwete barua ikimwomba kuunda tume huru ya majaji kwa ajili ya tukio hilo.

Source: Tanzania Daima ( July 2013).Wanasheria wamuunga mkono Mbowe. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: