Ninaunga mkono maazimio ya
kamati kuu ya CHADEMA ya kuanzisha mafunzo ya ukakamavu kwa vijana kwa ajili ya
kujilinda,kulinda viongozi na mali za chama chao.Binafsi nimefurahia sana jinsi
mwitikio ulivyokua mkubwa,vijana wamehamasika,ari yao ipo juu.Tusonge mbele
tena tufanye haraka
Ni jambo la ajabu kuwa
tunae Rais asiyejua kuelekeza hasira na kauli zake sehemu sahihi.Rais Kikwete
alinukuliwa na shirika la utangazaji la BBC akilaani hatua hii ya CHADEMA
alipokua katika zoezi la kufunga kongamano la amani lililoitishwa na TCD.
Kongamano la amani bila amani halina mantiki,ni kongamano nje ya
mantiki.Unapokua na kongamano la Amani ambalo linashindwa kukemea kauli za
kichochezi zilizotolewa na Waziri mkuu, basi moja kwa moja dhana nzima
inabadilika na sasa linakua ‘kongamano la unafiki’
Naomba nikope busara za
Rais kupitia kauli yake maarufu ‘Akili za kuambiwa,changanya na zako”
kwa kumkumbusha Rais kikwete yafuatayo
Mosi, Katiba ya CHADEMA
ambayo ilipelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa ipo wazi kuhusu suala la kuwa
na kikundi cha ulinzi kulingana na ibara hii,naomba kuinukuu‘
‘’7:7:5 Kutakua na
mfumo wa ulinzi na usalama wa mali,viongozi na maslahi ya chama utakaotambulika
kama brigedia nyekundu(Red Brigade)’’
Hii ni katiba ya CHADEMA
ambayo haijawahi kupigiwa kelele na haijavunja sheria wala katiba ya nchi maana
kama ingekiuka sheria basi ofisi ya msajili wa vyama vya siasa pamoja na
wanasheria wakuu walitakiwa wakamatwe mara moja na hata Rais atakua ameshiriki
kuvunja katiba mana siku zote ilikuwepo.Kinachofanyika sasa hivi ni kuwa Red
Brigade inaimarishwa zaidi na vijana kupata mafunzo ya ukakamavu zaidi.Rais
alitakiwa kutafakari na pengine kuomba ushauri kabla hajaibuka na kauli hii
inayoweza kumvunjia heshima na kutufanya sisi vijana tuwe wepesi wa kuhoji
weledi wake nap engine katika hatua mbaya zaidi kuishia kudharaulika
Pili,Rais Kikwete alitakiwa
amlaani waziri mkuu wake aliyemteua.Kauli ya Pinda ya kutaka jeshi la polisi
kupiga Raia ni kauli ya ovyo kutolewa na kiongozi mwenye busara na Rais
alitakiwa amfukuze kazi mara moja badala ya kuwalaani Raia wanaojilinda.Hapa
ndipo nilipoona konagamano lile ni mkusanyiko wa wanafiki na wasaliti wakubwa
wa Taifa hili.Nami natumia fursa hii sasa kuwalaani.
Pinda alivunja Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoapa kuilinda na kuitetea.
Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Ibara ya 13(2) inasema: “Ni marufuku kwa sheria yoyote
iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka
sharti lolote ambalo ni la kibaguzi ama wa dhahiri au taathira yake.”
Kifungu cha nne cha ibara
hiyo hiyo kinasema:
“Ni marufuku kwa mtu
yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya
sheria yoyote au katika utekelezaji wa shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.”
Pinda alitoa kauli hiyo akiwa anatekeleza kazi yake kama Kiongozi wa Serikali
Bungeni.
Katiba Ibara ya 13 (6) (e)
inaonya kuwa: “Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu
zinazomtweza au kumdhalilisha, pia Ibara ya 16 ya Katiba inasema: “Kila mtu
anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi ya nafsi yake, maisha yake binafsi na
familia yake na pia heshima na hifadhi ya maskani na mawasiliano yake binafsi.”
Waziri mkuu amevunja
katiba na Rais kwa kulinyamazia hilo, ameshiriki kuvunja katiba ya nchi.
Tatu,Sotetunatambua kuwa
Katiba yaJamuhuri ya muungano ya Tanzania inakataza mtu, chama au taasisi
yoyote kuunda jeshi au chombo chenye muelekeo wa kijeshi “Para-millitary
groups” ispokuwa serikali yenyewe. Kwa mfano; Katika sura ya tisa ya Katiba;
Ibara ya 147 (1) inaeleza :
“Ni marufuku kwa mtu
yeyote au shirika
lolote au kikundi chochote
cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la
aina yoyote”. Sasa pamoja na kifungu hiki cha katiba; CCM(Green Guard),
CUF(Blue Guard) na sasa CHADEMA(Brigedia nyekundu kwa ajili ya kujilinda) wana
vikosi vya ulinzi ndani ya chama. Je ina maana ni ukiukaji wa katiba?
Nne,Mwenyekiti hiuyu wa CCM
Ndugu Jakaya Kikwete alitakiwa atangaze maslahi katika laana zake alizotoa
maana inajulikana kwamba Chama chake kinachomiliki vikundi vya green Guard
wakati huo huo wakisaidiwa na polisi kama alivyokiri kwenye mkutano wa NEC
mwaka jana ndicho kinachohatarisha amani
Pia nimeona maelezo ya
naibu katibu mkuu wake Mwigulu Nchemba yaliyojaa upotoshaji na au pengine ni
mgumu kuelewa na pengine lugha ya kiingereza inamtatiza hasa pale alipotumia
maneno ya kiingereza yasiondana na dhana maarufu ya misamiati husika.Kikosi cha
Green Guard hapa chini hakifanyi mazoezi ya kawaida maana wanafanya hadi
mazoezi ya silaha na pia wameanza kufanya mazoezi hayo kwa kutumia vijana wadogo
wenye umri chini ya miaka 18 na kuwalea kwa viapo.Maelezo ya mwigulu ni ya
uongo na upotoshaji
RED BRIGADE ya Italy ilikua Political Group ambayo ilikua na itikadi kinzani dhidi ya umoja wa kujihami wan chi za Magharibi NATO.Ilitambulika kama Brigate Rosse yaani BR.Ilikua na mrengo wa kiitikadi unaoendana na Leninism au Marxism ukiongozwa na Mario Morreti.Hapo ni lazima tuweke historia sawa
Mathalani CCM wanaogopa kivuli chao kwa maovu wanayotekeleza kupitia Green Guard ambayo ina muundo kama wa The green Armies ya Russia ya chama cha Kisoshalisti cha mapinduzi na walikua wakifanya kazi ya kuteka na kushambulia wafuasi wa vyama vingine.Red guard ambayo baadae ilikuaja kugeuka kuwa red army ilipambana na wafuasi hao .CHADEMA hakipambani,kinachukua hatua ya kujilinda maana wafuasi na viongozi wetu wanashambuliwa huku polisi wakiwa kimya
Nampa Mwenyekiti wa CCM
ndugu Jakaya kikwete na Mwigulu Nchemba changamoto.Wasome Ripoti ya Amnesty
International ya Mwaka 2001 juu ya kikundi cha kihuni cha Ghaddafi kilivyokua
kikiwafanyia wananchi wa Libya.Kikundi hicho kilikua kikifanya hayohayo Mwigulu
Nchemba aliyosema
Ripoti ina kichwa cha
habari
‘Libya: Existence of the
Green Revolutionary Guard; origin, composition and activities; whether this
organisation is involved in kidnappings and torture; possible threats against
returned asylum seekers by the Revolutionary Guard or other groups ‘ Pia
muundo wa Green Guard hauna tofauti na muundo wa Red Guard ya China ambayo
ilikua ikitesa,kuteka na kushambulia Raia miaka ya 1960.Ilikua Political
movement group ya vijana iliyoratibiwa na baadhi ya makada waliokua wakimuunga
mkono Chairman Mao
RED NA GREEN ni Rangi
tu ila dhamira na vitendo vinatofautiana. Picha hizo hapo juu zinatoa taswira
halisi na watanzania sasa waamue
Katika Picha: Kushoto ni Mbunge wa Ilemela (CHADEMA) Highnes Kiwia aliyeshambuliwa na wafuasi wa CCM tarehe 31 Machi,2012 baada ya kufunga kampeni ya uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Kirumba-Mwanza.Polisi hadi leo wapo kimya,kongamano la Amani lipo kimya na msemaji wa Jeshi la polisi hana majibu
Pichani Kulia:Mzee Nyaulingo Lunyiliko ambaye ni mwenyekiti wa wazee wa wilaya ya kilolo akivuja damu baada ya kushambuliwa na Green Guard wakati wa kampeni za ichaguzi mdogo uliofanyika Juni16,2013
Maiti ya kada na
Mwenyekiti wa CHADEMA USA RIVER aliyeuawa kinyama.Miongoni mwa watuhumiwa ni
viongozi wa Kitongoji cha Mgadini wa CCM Davis Mkumba na Mathias
Nathan ambao walitoroka Oktoba 4,2012 wakiwa chini ya ulinzi wa polisi
walipokua wakipelekwa mahakamini.Marehemu aliacha mjane na watoto wadogo
Hapa Chini ni kada wa CCM
aliyekua akipewa mafunzo tofauti na uongo alioueleza Mwigulu Nchemba,sasa Laana
za Mwenyekiti wa CCM Ndugu Jakaya Kikwete azielekeze huku.Jeshi la polisi
lilikua wapi.Sikiliza hiii na baada ya hapo Rais achague moja Green Guard
ifutwe ama TUIMARISHE RED BRIGADE. Hakuna compronise!!
Source: Saanane B. (July 2013).Tumpuuze Mwigulu Nchemba na Mwenyekiti Wake(Picha), Tuimarishe haraka Red Brigade. Retrieved from Jamii Forums
No comments:
Post a Comment