Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, July 25, 2013

‘Sugu’azidi kumkalia kooni Pinda

     Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, (Sugu) (Chadema) ameendelea kumkalia kooni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusiana na kauli aliyoitoa bungeni ya kuruhusu polisi kuwapiga raia ambapo alidai kwamba hakupima kauli na wadhifa wake wakati akitoa kauli hiyo. Sugu alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika Mji Mdogo wa Mbalizi nje kidogo na Jiji la Mbeya wakati akiwahutubia wakazi na wafuasi wa chama hicho. Alisema kamwe hawezi kufuta kauli na maneno yake aliyoyatoa kwenye mtandao wa kijamii akimtuhumu Pinda kwa kauli yake na haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa kama huyo.
    “Kauli aliyoitoa Pinda bungeni kamwe haikubaliki na mwananchi yoyote na ndiyo maana hata mimi nilisema na nitaendelea kumsema Pinda kwa kauli zake hadi pale atakapowaomba radhi Watanzania,” alisema Sugu na kuongeza: Alisema ili kujisafisha kuhusiana na kauli yake yenye lengo la kuwanyanyasa Watanzania ni lazima awaombe radhi na kama hatafanya hivyo basi ajiuzulu wadhifa wake. Alisisitiza kwamba kamwe hatasita kusema jambo kwa masilahi ya wanaMbeya na Watanzania kwa jumla,kwa kuogopa vitisho vya vyombo vya dola kama walivyotaka kumchukulia hatua baada ya kumsema Pinda kupitia mitandao ya kijamii.
Source: Kahango G. (July 2013).‘Sugu’azidi kumkalia kooni Pinda. Mbeya. Retrieved from Mwananchi

No comments: