Mikael P. Aweda |
Ninazo taarifa kwamba Lameck Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu
katibu mkuu wa CCM ameshiriki kutengeneza kesi feki dhidi ya makada wa CHADEMA watajwa hapo juu, kutokana na
ushahidi unaozidi kuanikwa hadharani mtaani siku hadi siku. Nitalelezea matukio
4 ikiwepo sakata Lenyewe.
1) Mwigulu Vs kesi feki ya Dr Kitila na Mwita Mwikwabe Waitara
inayoendelea singida.
Leo nimepata taarifa muhimu ya ushiriki wa Mwigulu Nchemba
katika kesi inayomkabili Dr Kitila Mkumbo na Mwita Mwikabwe Waitara. Najua
wengi mnakumbuka kuwa Dr Kitila Mkumbo na Mwita M. Waitara walifanya mkutano wa
hadhara ktk Jimbo la Mwigulu mwaka jana. Baadaye CCM na serikali wakafungua
kesi dhidi ya makada hao wawili wa CHADEMA, wakituhumiwa kumkashifu Mwigulu mwigulu Nchemba. Kesi
inaendelea hadi sasa mahakamani, ingawa Mwigulu hajakamatwa wala hajaitwa
mahakamani.
Nimepata ushahidi gani leo??
Baada ya mimi na wenzangu kwenye Chama kufuatilia kwa niia zetu
tumegundua kwamba kesi zote mbili zilizofunguliwa (Lugha ya matusi dhidi ya
Kitila na waitara) na kesi ya mauaji dhidi ya wanachama wengine Singida,
zilitengenezwa na Mwigulu Nchemba na zilifunguliwa na Jamhuri kwa maelekezo
yake kama ushahidi unavyoonesha hapa chini.
Mosi, vijana waliotumika baadhi yao walitoka Dar es salaam na
walikodiwa na Mwigulu Nchemba kwa ahadi ya kupewa PIKI PIKI akiwepo Flavian
Njama ambaye ni katibu wa ccm wa kata ya Tandika hapa hapa Dar es salaam na
ambaye naye ni mmoja wa washtakiwa Singida. Mpaka sasa Mwigulu Nchemba hajawapa
piki piki na ndo maana siri zimeanza kuvuja. Shame on him.
Kijana Samaria rafiki yake Mwigulu Nchemba ambaye ni
katibu wa kata wa CCM jimboni kwa Mwigulu, pamoja na jina lake kutajwa mara
nyingi mahakamani lakini bado hajaitwa mahakamani sawa sawa na Mwigulu Nchemba
mwenyewe, ambaye naye alipaswa awe ameshatinga mahakamani kwa kuwa yeye ndo
mkashifiwa.
Tatu, nina ushahidi wa kutosha kwamba Mwigulu Nchemba ndo anayegharimia
kesi hizi kibinafsi na kutokana na kulemewa na gharama sasa anatamani
kesi hii iishe haraka.
Nne, kuna ushahidi ambao uko public tayari kwamba Polisi
wenyewe akiwepo ocs tayari wameshatoa ushahidi mahakamani kwamba vijana
waliohusika ni wanaCCM na kijana aliyeuawa ni mwanaccm, taarifa ambazo ni
kinyume na maelezo ya CCM na Mwigulu Nchemba nje na ndani ya Bunge.
NB; kuna tetesi ambazo ninaendelea kuzifuatilia ambazo zinadai
kwamba Mwigulu Nchemba anashawishi baadhi ya Viongozi muhimu serikalini ili ama
Dr Kitila Mkumbo atimuliwa Chuo kikuu cha Dsm, au aondolewe kwenye ukuu wa
idara alionao pale UDSM. Lengo lake anadai ni kuiokoa CCM Iramba 2015, wakati
ukweli ni kwamba, yeye anaona kibarua chake kitaoteshwa magugu na Dr Kitila 2015.
Je, atafanikiwa?
2) Mwigulu Nchemba Vs John Mnyika. Mwigulu Nchemba alidai kutumiwa meseji ya kutishwa maisha kwa
njia ya simu na John Mnyika. Baadaye Mwanausalama wa CHADEMA, Mabere Marando akamwuumbua kwa
kunasa taarifa za uwepo mashine (mitambo) za kutengeneza meseji feki
iliyonunuliwa kwa mabilioni fedha za walipa kodi wa nchi hii kutoka nje. Kama
siyo kunaswa kwa taarifa hiyo ina maana Mnyika angelala Lupango kama Lwakatare
kwa kuwa mchakato wa kufungua kesi ulishaanza serikalini
3) Mwigulu Vs Lwakatare. Nimeandika na watu wengi
wameandika uhusiano kati ya Mwigulu Nchemba Lodovick Joseph aliyekamatwa pamoja
na Lwakatare ikiwepo kumtumia Ths 50,000/=, pamoja na mawasiliano ya mara kwa
mara kati ya Ludovick na Mwigulu. Ikumbukwe kwamba, Mwigulu tayari ameshakiri
kwamba yeye ndo aliyepeleka CD polisi akidai kupewa na mwanaCHADEMA. Mpaka leo hajasema kada yupi wa
CHADEMA alimpa Mwigulu CD ya Lwakatare, Kwa nini huyo kada wa CHADEMA ampelekee Mwigulu CD badala ya
kuipeleka polisi, kwanini CD aliyoitangaza tangu dec 2012 iibuliwe march 2013,
siku mbili baada ya Kibanda kutekwa. Maswali ni mengi na hayajibiki, na ndo
maana kesi imeshafutwa.
4) Mwigulu Vs tuhuma za Kumkimbia Dr Slaa
Kuna watu walimwona Mwigulu Nchemba akiongea na Nyakarungu (kada
wa CHADEMA?). Walichozungumza ni siri
yao. Wakiwa ktk kuzungumza kwao wakamwona Dr Slaa anapita jirani, wakamkimbia.
Aliyewaona akaweka thread JF kuhusu sakata hilo. Mwigulu mwenyewe akaja
kukanusha thread hiyo hapa JF, na haya ndiyo maelezo yake yanayonitatiza sana
kuhusu uwezowake wa kufikiri.
Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya
kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati
nzuri hata Dr. Slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa
njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.
A) Mwigulu hakumwona Dr Slaa na hakumkimbia NA hana sababu ya
kumkimbia Vs B) kulikuwa na watu wengi tu na Dr Slaa alipita bila attention ya
watu.
Linganisha A na B ujue uwezo wa Naibu katibu mkuu wa CCM, yaani
hakumwona Dr Slaa na wakati huo huo Dr Slaa alipita bila attention ya watu
wengi kwenye tukio hilo hilo moja.
My take;A) Natambua kwamba huu
mradi wa CD ya Lwakatare, Kesi ya Mkumbo kitila/Mwita Waitara, Sakata la Mnyika
na Ununuzi wa viongozi wa CHADEMA haukuwa mradi wake kibinafsi -- ni mradi wa chama ni mradi wa
Nape, Wasira Jack Zoka nk, lakini kwa nini atumike yeye tu kama siyo wanamwona
ni mtu rahisi wa kumtumika kwa miradi ya kuokoa chama chao? Mimi ningekuwa
Mwigulu ningeshtuka, ningekataa, siwezi kutumika tu.
B) Kwa kuwa steven Wasira alipata kura nyingi kwa ahadi ya
kuisambaratisha CHADEMA, na kwa kuwa mtego wake umeshashindwa, namshauri akawaombe radhi
wanaCCM waliompa kura. Au ana Plan B ya kuisambaratisha CHADEMA?
C) Hivi hii habari ya Mwigulu Nchemba kufanya kila atakacho na
hakamatwi itakuwa hivi mpaka lini? Kuanzia tuhuma feki dhidi ya Mnyika, CD ya
Lwakatare na Kununua watu toka Dar es Saam kwenda kufanya mauaji Singida ktk
mikutano ya CHADEMA pamoja na ushahidi wa wazi wa Polisi Mwigulu hajaguswa. Je hali
hii mpaka lini?
Source: Aweda M. (May 2013). Siri za Mwigulu Nchemba kutengeneza kesi feki dhidi ya Dr Kitila Mkumbo na Mwita M. waitara zavuja. Retrieved from Jamii forums
No comments:
Post a Comment