Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Tuesday, July 16, 2013

Nape akwepa kuzungumzia matokeo udiwani Arusha


   Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema wanaopaswa kuulizwa jambo lolote linalohusu uchaguzi wa udiwani wa kata nne uliofanyika Jumapili wiki iliyopita, jijini Arusha, ni viongozi wa chama wa mkoa huo. Alisema hayo alipozungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, baada ya kutakiwa kutoa maoni yake kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuibuka mshindi katika kata zote nne. “Waulize wenyewe. Siwezi kuzungumzia issue (suala) ndogo. Unajua chama chetu kimegawa majukumu. Kule kuna mwenyekiti wa mkoa, katibu pamoja na wengineo,” alisema Nape.

    Alipoulizwa sababu  za kutoa maoni katika chaguzi nyingine mara tu matokeo yanapotangazwa, kama vile Jimbo la Igunga, Nape alisema uchaguzi huo unahusu ubunge  tofauti na udiwani.Alisema hata katika uchaguzi wa kata nyingine 22, alizungumza kwa kuwa ulikuwa umehusisha kata mbalimbali nchini na siyo mkoa mmoja.

Source: Ippmedia (July 2013).Nape akwepa kuzungumzia matokeo udiwani Arusha. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: