Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, July 22, 2013

Mwigulu Nchemba aumbuka katika jaribio la kuhonga madiwani wa CHADEMA,taarifa zanaswa mapema


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimenasa mpango mchafu wa naibu katibu mkuu wa CCM Mwigulu Nchemba wa kuwahonga madiwani wa CHADEMA jimbo la Igunga ili wajiunge na CCM

Madiwani hao 3 akiwemo diwani mmoja wa kata na wawili wa viti maalumu walimkatalia kata kata .

Diwani wa kata ni yule ambaye baba yake alifanyiwa hujuma ya kugombea akiwa CCM na kisha mtoto wake akagombea kupitia CHADEMA na wananchi wakampitisha kwa kishindo

Kwa taarifa za awali ni kwamba CHADEMA baada ya kujulishwa mipango hii kiliwapongeza madiwani wake kwa kuheshimu dhamana waliyopewa na wananchi na kuheshimu misingi ya demokrasia.

Aliwaahidi fedha na pia kumuhakikishia diwani huyo wa kata kuwa endapo angegombea kupitia CCM basi chama chake kingempitisha kwa gharama yoyote hivyo asiwe na shaka

Ni jambo la ajabu kuwa Mwigulu anafanya siasa chafu za kurubuni madiwani wahamie chama chake bila kujali maadili ya kisiasa na misingi mipana ya kidemokrasia huku mamilioni ya kodi za watanzania maskini zikiteketezwa katika chaguzi pasipo sababu
  
Taarifa zaidi kuhusu hili zitatolewa pamoja na majina ya madiwani hao kupitia mamlaka husika kichama.

Kamanda Ben Saanane

No comments: