Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, July 28, 2013

Mbowe: CCM inaogopa serikali tatu




    MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinapinga mfumo wa serikali tatu usiingizwe katika Katiba mpya  kwa vile kinajua kwamba huo ndio utakuwa mwisho wa utawala wake. Mbowe alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Chipukizi mjini Tabora na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi. Alisema kuwa CCM inakwepa kuzungumzia suala la serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuhofia kwamba vyama pinzani vitatwaa ushindi katika ujaguzi mkuu ujao.

     “CCM inaogopa serikali tatu kwa sababu inajua Zanzibar ni mali ya Chama cha Wananchi (CUF) na Tanganyika itakuwa ya CHADEMA; yenyewe itakuwa wapi?” alihoji. Mbowe alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili umekuwa manufaa kwa Wazanzibar kwani Watanganyika wengi wakienda kwao hawana uhuru wa kumiliki mali tofauti na ilivyo wao wakija bara wanamiliki kila kitu sawa na Watanzania wengine. “Tanganyika tupewe uhuru wetu kama Wazanzibari, wana bendera yao, wimbo wa taifa, rais wao na Bunge lao,” alisema. Mbowe pia aliwatahadharisha wananchi juu ya hujuma wanazofanyiwa na serikali iliyo madarakani ikiwemo kulipia kodi ya umiliki wa laini ya simu za mikononi.

     Alisema kuwa serikali ya CCM ilifuta kodi mbalimbali kwa ajili ya kumhadaa mwananchi ili aweze kuipigia kura lakini hivi sasa zimerejeshwa kwa mlango wa nyuma ikiwemo hiyo ya simu na ile inayowataka wananchi kununua visimbuzi ndipo waweze kupata mawasiliano ya runinga zao. Mbowe ambaye yuko kwenye ziara ya kawaida kwa ajili ya kuimarisha chama, alisema kuwa kuanzia Agosti 4 chama hicho kitafanya ziara ya kutembelea mikoa yote nchini na kukutana na wananchi ili kuzungumza na kujadili nao wanataka Katiba iwe na muundo gani. Katiika hatua nyingine wananchi wamelaani vikali kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kwamba wanaotaka serikali tatu ni wazee ambao wanagojea kifo.

Source: Murugwa T. ( July 2013).  Mbowe: CCM inaogopa serikali tatu. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: