Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, July 26, 2013

Maelezo kesi ya Dk. Ulimboka kutolewa Agosti 6



   MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imesema taarifa zaidi kuhusu kesi ya kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, itatolewa Agosti 6 mwaka huu. Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema, wakati kesi hiyo ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa. 
“Taarifa zaidi za shauri lako zitatolewa Agosti 6 mwaka huu na mshitakiwa utaendelea kubaki rumande,”alisema Hakimu Lema. Mara ya mwisho, kesi hiyo ilipotajwa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu iliiahirisha kwa mara ya mwisho kutokana na upande wa mashtaka kueleza kwamba bado unaendelea na upelelezi wa shauri hilo.

     Hakimu Lema aliutaka upande huo kukamilisha upelelezi wake ifikapo jana kesi hiyo ilipotajwa tena mahakamani hapo. Katika kesi hiyo, mtuhumiwa Joshua Mulundi, ambaye ni raia wa Kenya, anatuhumiwa kuhusika na tukio la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka. Wakati huo huo, leo mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu dhidi ya Wachungaji waliokuwa wakiendesha biashara ya Upatu bila kibali.

Source: Kulwa M. (July 2013). Maelezo kesi ya Dk. Ulimboka kutolewa Agosti 6. Retrieved from Mtanzania

No comments: