Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, July 28, 2013

Kyela waitungia wimbo CHADEMA


         KUNDI la Sanaa la Kyela Various Artist limeingia studio kuandaa kibao cha kukipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kazi kubwa inachofanya katika kupigania masilahi ya wananchi. Akizungumza mjini hapa jana, kiongozi wa kundi hilo la wasanii sita, Chriss Sikwese, alisema kilichowagusa hadi kukipongeza chama hicho ni sera yake ya kuhimiza amani, upendo, maendeleo na vita yake dhidi ya ufisadi. Alisema kutokana na kukithiri vitendo vya kifisadi kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana, wanaungana na chama hicho kukemea vitendo hivyo kupitia sanaa ya muziki.

      Sikwese alisema wanaamini kwa njia ya sanaa, ujumbe utafika kirahisi kwa jamii ili wawe makini katika chaguzi mbalimbali kwa kuchagua watu ambao watapigania masilahi ya wanyonge. “Tumeshindwa kupanda majukwaani kupinga vitendo hivyo kwa vile sisi si wanasiasa, lakini tumeamua kufikisha ujumbe wetu kwa jamii kwa njia ya sanaa ya muziki,” alisema Sikwese, maarufu kama Jerry B. Alisema hivi karibuni watarekodi albamu ya video iliyobeba jina la ‘CHADEMA ndio chama’ ambayo itasambazwa nchi nzima.

     Mbali ya Jerry B, vichwa vingine vinavyounda kundi hilo ni Hassan Nyoni ‘Chance J’, Ramadhani Popos ‘Ramso’, Denis Kibodia (D Nice, Benson Nsemwa (Ben Flavour na Julius Mwaipopo ‘J people.’ Alisema kibao cha ‘CHADEMA ndiyo Chama’ kimekamilika na kimepokewa vizuri na wakazi wa Kyela na vitongoji vyake. Alisema hivi karibuni wataanza kukisambazwa katika mikoa mbalimbali kwani lengo ni kufika Tanzania nzima kutokana na ujumbe kumgusa kila Mtanzania.

Source: Yassin I. ( July 2013). Kyela waitungia wimbo CHADEMA. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: