TAYARI upande wa utetezi, ukiongozwa na Wakili Msomi Peter
Kibatala umewasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, maombi ya marejeo chini ya
hati ya haraka sana, akiiomba kuitisha mafaili mawili ya kesi ya awali Igunga
ambako watuhumiwa wanne walifunguliwa mashtaka ya kushambulia na kudhuru mwili
(kabla ya kuachiwa na kuunganishwa kwenye kesi ya ugaidi na Henry Kilewo) na
faili la kesi ya ugaidi iliyofunguliwa Tabora, akiiomba mahakama hiyo ifanye
marejeo juu ya;
1. Suala la individual calendar, kama lilivyojitokeza leo
mahakamani
2. Kitendo cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora kujivua mamlaka
3. Kama uamuzi wa kufuta kesi ile ya Igunga kutoka jinai ya kushambulia na kudhuru mwili na kuwa jinai ya ugaidi, ulikuwa sahihi.
4. Kwa nini the same incident, ilifunguliwa kesi ya kosa jingine
washtakiwa wakiwa wanne ghafla limebadilishwa na kuwa kosa jingine, ambapo DPP aliondoa shtaka wakati washtakiwa wote wanne tayari dhamana yao iko wazi.
5. Mamlaka ya DPP yanatumika vibaya kwa nia mbaya ya
kuwafungulia watu kesi kwa lengo ambalo si la kutenda haki.
6. Mahakama ikishindwa kuondoa mashtaka ya ugaidi, basi iamuru
kila mshtakiwa arudishwe na kushtakiwa mahali alikokamatwa.
Katika maombi hayo, upande wa utetezi pia umeiomba Mahakama Kuu
ifanye marejeo ya hoja za awali ambazo Mahakama ya Hakimu Mkazi imejivua
mamlaka ya kuzitolea maamuzi.
KILICHOTOKEA leo Tabora
Mahakama ya Hakimu Mkazi, kesi ya madai
ya ugaidi inayomkabili Kamanda Henry Kilewo na wenzake wanne, Henry Kilewo,
Evodius Justinian wa Buboka, Oscar Kaijage wa Shinyanga, Seif Magesa Kabuta wa
Mwanza, Rajab Daniel Kihawa wa Dodoma.
Washtakiwa waliingia chumba cha mahakama saa 5.00 asubuhi,
Hakimu Mkuu Mkazi, Issa Magori, ameingia saa 5.07. Korti ikaanza kwa mawakili
wa pande zote mbili kujitambulisha, ambapo upande wa mashtaka ulioongozwa na
Wakili Juma Masanja, upande wa utetezi ulikuwa na Wakili Msomi Peter Kibatala
na Wakili Emmanuel Musiani.
Hakimu Mkuu Mkazi, Issa Magori akaanza kwa kusema kuwa yale
yalikuwa ni maelekezo ya mahakama (si maamuzi?) kwamba ni bahati mbaya kuwa
Juni 24, 2013 shauri hilo (namba PI 75 ya mwaka 2013) lilipokelewa mahakamani
hapo (Mahakama ya Hakimu Mkazi, Tabora) na mawakili wa pande zote mbili
wakafanya mawasilisho yao mahakamani...ni bahati mbaya kwamba mawasilisho hayo
yaliandikiwa maelezo hapa kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi leo.
Akatoa maelekezo/uamuzi;
Kuhusu shtaka la kwanza, mahakama haina mamlaka ya kusikiliza
shauri hilo, yote yaliyofanyika hayakupaswa kufanyika. Hivyo utetezi wowote
uliopo unapaswa kuwasilishwa Mahakama Kuu, si katika mahakama ya hakimu mkazi
kwani haipaswi kuufanyia maamuzi. Mahakama hiyo haina uwezo wa kuskiliza kesi
hiyo.
"Mahakama imeahirishwa hadi baadae...upande wa mashtaka
uandae taratibu zingine kwa ajili ya Mahakama Kuu, si hapa," amesema
Hakimu Magori, kisha akainuka huku akiacha watu wamepigwa na butwaa, bila kujua
hasa kinaendelea.
Kilikuwa ni kitendo cha dakika 7
Hakimu alionekana kuwa na haraka sana, kiasi kwamba alionekana
kusahau masuala kadhaa;
1. Kumuuliza mwendesha mashtaka kama ana lolote la kusema,
mathalani kujua kama upelelezi wa kesi umekamilika
2. Kutoa uamuzi wowote juu ya shtaka la pili kwenye kesi hiyo,
ambalo linahusu kushambulia na kudhuru mwili.
Kwa kweli aliwaacha watu wengi wakiwa puzzled wakiwa hawajui
kitu gani cha kufanya, ikiwemo waendesha mashtaka...kwani alifanya kitu
kisichokuwa cha kawaida.
Kuhusu marejeo aliyowasilisha Wakili Kibatala
1. Suala la individual calendar; itakumbukwa kuwa kwenye kesi ya
Lwakatare, baada ya maamuzi ya Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi ya ugaidi,
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilishindwa kutoa dhamana (iliyokuwa wazi) kwa
Lwakatare hadi Hakimu mwenye kesi arudi kutoka likizo. Lakini leo, suala la
namna hiyo hiyo limetokea, ambapo 'maelekezo' ya leo yametolewa na hakimu
mwingine badala ya hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi, Jocktan Rushwela.
Haijulikani hadi sasa faili hilo lilihamaje kutoka kwa hakimu wa awali hadi
hakimu mwingine.
2. Kujivua madaraka kwa mahakama kwa kushindwa kutoa uamuzi hata
kwa mambo yaliyoko 'usoni mwake'
Hoja za awali za upande wa utetezi zilizotolewa Juni 24, wakati
kesi iliposikilizwa kwa mara ya kwanza, ambazo ilidhaniwa leo zingetolewa
maamuzi ilikuwa ni pamoja na;
1. Mashtaka hayo ya tuhuma za ugaidi, hazina concent ya DPP kwa
kadri ya hitaji la sheria katika tuhuma za ugaidi. Katika suala hilo, sheria
inasema 'shall'.
2. Charge sheet ya shtaka hilo la ugaidi, haina maelezo yoyote
ya kuonesha kuwa kulikuwa na ugaidi au ni tukio la ugaidi (kama ilivyokuwa
kwenye kesi ya Lwakatare, mtakumbuka alivyosema Wakili msomi Tundu Lissu wakati
ule), kiasi kwamba kwa nini wasishtakiwe kwa kosa jingine la jinai ambalo
wanaweza kupata dhamana.
3. Kila mshtakiwa arudishwe na kushtakiwa mahali
alikotoka/ alikokamatwa kama ambavyo sheria inaelekeza.
No comments:
Post a Comment