Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Friday, July 26, 2013

CWT:Matokeao ya darasa la saba, kidato cha nne kuwa mabaya zaidi



 
     Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Tanga kimeitahadharisha serikali isipochukua hatua kuboresha huduma kwa shule za msingi na sekondari matokeo ya kidato cha nne na darasa la saba kwa mwaka huu yatakuwa mabaya kuliko ya kidato cha nne mwaka jana. Tahadhari hiyo inafuatia baadhi ya shule za Halmashauri ya Jiji la  Tanga kukosa fedha za kuchapishia mitihani na kuwaalzimu walimu kuandika maswali ubaoni hali inayopunguza kiwango cha upimaji wa uelewa wa wanafunzi kutokana mitihani iliyopaswa kuchapishwa kuwa na  maswali 50 kupungua hadi 25 kutokana na kuandikwa ubaoni. Akizungumza  NIPASHE Katibu wa CWT wa mkoa huo, Ndelamio Mangesho aliitaka serikali kurekebiesha kasoro hizo haraka ili kunusuru kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao.

       Alisema uandishi wa mitihani ubaoni unapunguza kiwango cha upimaji kwa wanafunzi  kwani karatasi zilizochapishwa zinachangia kumsaidia  kujifunza wakati wa kufanya masahihisho. Mwalimu Mangesho, alisema Wizara ya Elimu na Mafunzi ya Ufundi haina bajeti ya kutosha ya kuendesha shule pamoja Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutoa michanganuo ya michango isiyotakiwa shuleni. Alisema ni sahihi kwa serikali kupinga michango ya madawati na masomo ya ziada shuleni lakini michango ya ulinzi, maji, umeme na fedha za kuchapishia mitihani vinatakiwa kuangaliwa kwa kina kabla ya kuzuia wazazi kuchangia.  Kwa upande wa baadhi ya walimu wa shule za msingi na Sekondari za Wilaya ya Tanga, walisema  shule nyingi hazina miradi ya kuwaingizia kipato hivyo walimu wakuu wanalazimika kuzilipia kutoka kwenye mishahara yao.

      Walisema hali hiyo imesababisha wanafunzi kushindwa kufanya mitihani na mazoezi ya kujipima kutokana na shule kushindwa kuchapisha.  Mwishoni mwa mwaka jana, Mkuu wa Wilaya ya Tanga,  Halima Dendego alipiga marufuku wazazi kutoa michango kwa ajili ya ulinzi, maji, umeme na fedha za kuchapisha mitihani shuleni na kusabbaisha  wanafunzi kushindwa kufanya mitihani ya muhula wa kwanza juni mwaka huu.


Source: George L. ( July 2013).CWT:Matokeao ya darasa la saba, kidato cha nne kuwa mabaya zaidi. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: