Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, July 29, 2013

Amani: Vyombo vya dola tatizo


       Tanzania ipo katika kipindi hatarishi, inayotishia uvunjifu wa amani iliyodumu kwa zaidi ya miaka ya 50 iliyopita, huku mikakati makini ya kudhibiti hali hiyo ikikosekana. Kauli hiyo ilitolewa na Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Bernadetha Killian (UDSM), wakati akiwasilisha mada katika kongamano la kujadili ‘Mustakabali wa Amani na Usalama wa Taifa letu kwa miaka 50 ijayo’, lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana. Kongamano hilo liliandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa UDSM (Udasa) kwa kushirikiana na Televisheni ya ITV na Radio One Stereo.

    Alisema kinachofanyika hivi sasa ni kudhibiti vihatarishi vya amani, badala ya kutatua. “Ni kama kumpa mgonjwa Panadol kutuliza ugonjwa badala ya kutibu,” alisema Profesa Killian. Alivitaja baadhi ya viatarishi vya uvunjifu wa amani kuwa ni kuwapo demokrasia nusu, ukosefu wa ajira kwa vijana, mfumo kutoa fursa ya kuzuka vurugu za kidini na kuongezeka kiwango cha umaskini. Vingine ni matamshi ya uchochezi yanayotolewa na viongozi wa dini na siasa, uhusiano mbaya kati ya serikali na waumini wa dini na migogoro miongoni mwa waumini wa dini moja na nyingine.  Alisema inasikitisha kuona viongozi wa kisiasa wakishughulika na uchaguzi badala ya migogoro. Profesa Killian alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepoteza kuwa mfano wa kuigwa katika hilo, huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitumia muda wake kujihami na vyombo

Source: Said M. (July 2013). Amani: Vyombo vya dola tatizo. Ippmedia/ Nipashe

No comments: