Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, June 24, 2013

Watuhumiwa wa kurusha bomu waachiwa


 WATU watatu waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za urushaji bomu katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa CHADEMA, Juni 15 eneo la Soweto wameachiwa. Akizungumza na Tanzania Daima jana, kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi juu ya suala hilo ukiwa bado unaendelea. Alipotakiwa kuwataja watuhumiwa hao, Kamanda Sabas hakuwa tayari kwa kusema ni mapema mno kutaja majina ya watuhumiwa hao kwa sababu uchunguzi wa suala hilo unaendelea.

     Alifafanua kuwa watuhumiwa walihojiwa na askari wa upelelezi kuangalia uhusiano wao na mlipuko wa bomu katika viwanja vya Soweto na baada ya kukamilika mahojiano hayo wameachiwa kwa dhamana. Alisema kuwa jeshi hilo halihusiki na mpango wa kutaka kutorosha majeruhi walioko hospitali walioeleza tukio hilo na kudai ni taarifa za mitaani . “Kuhusu propoganda zilizoenea jijini Arusha kuwa vyombo vya dola vina mpango wa kutorosha wagonjwa wanaosema ukweli hospitalini na kuwapeleka kusikojulikana si za kweli na ni upotoshaji,” alisema.

       Alisema polisi au watu wa usalama wana wajibu wa kuhoji mtu yeyote pale tukio linapotokea ili kubaini ukweli wa jambo, hivyo wagonjwa hao hawana haja ya kuogopa na wasitishwe na maneno ya uongo ya mitani. Sabas alisema hivi sasa wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Freeman Mbowe, pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, wabunge wanne wengine na wafuasi wao 70.

Source: Siwayombe R. (June 2013).Watuhumiwa wa kurusha bomu waachiwa. Retrieved from Tanzania Daima

No comments: