Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Monday, June 17, 2013

Mimi Mwanakijiji: Tulaani unyama huu wa Arusha


Mtazamo wangu     

KILICHOTOKEA mkoani Arusha juzi ni kitu cha kulaaniwa kwa kauli yote kali. CHADEMA inahitaji ioneshe kuwa 'sasa imetosha'. Inawezekana vipi ndani ya miaka takriban mitatu tu vitendo vya kinyama vimekuwa vikifanyika dhidi ya wana-CHADEMA mara kwa mara wanapojaribu kufanya mikutano ya amani?

Ni nani amesahau yaliyotokea Januari 5 huko huko Arusha na matukio mengine yaliyofuatia kuanzia Mwanza, Iringa, Morogoro, Songea, Tukuyu, Mbeya, Igunga na sehemu nyingine? Hivi ni kweli nchi yetu ina vyombo vya usalama? Ni kitu gani kwa kweli wameweza kukilinda kikawa salama? Matukio haya yote yangelazimisha kufukuzwa kwa watendaji wakuu wa vyombo vya usalama (polisi, Idara ya usalama wa taifa). Nilishawahi kuuliza huko nyuma katika mojawapo ya makala zangu – Hadi nani auawe ndio tutajua kuwa tuna tatizo?

     Tukio la Arusha ni ishara tu ya kile ambacho kiko vibaya - ubovu wa mfumo wetu wa intelijensia na usalama. Kama tunavyojua tukio hili limekuja miezi michache tu baada ya tukio kama hilo huko huko Arusha katika Ibada ya Wakfu ya Kanisa Katoliki. Nani atasahau mazingira yale ni kama yamejirudia tena? Na safari hii sijui watamkamata kijana gani, maana hawa vijana wenye ujuzi na uthubutu wa hivi ni lazima wawe makini kweli! Yule mwingine bado yuko ndani halafu kuna mwingine au wengine?

    CHADEMA waoneshe msimamo, vinginevyo - na nilishawahi kuwaambia ndugu zangu hawa - wataendelea kuzika na kubeba majeneza ya wanachama wao na mashabiki wao. Msimamo wao uwe wazi kabisa kuwa sasa imetosha. Baadhi ya mambo ambayo naamini yanatakiwa yawepo kwenye msimamo huo: 

(a) Kutaka Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Operesheni pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), kujiuzulu au kufukuzwa kazi.
Matukio kama haya yanahitaji watu kuwajibishwa siyo kupandishwa vyeo kama ilivyotokea kwa Kamuhanda!

(b) Kutaka Mkuu wa Usalama wa Taifa awajibishwe. Taasisi hii imekuwa dhaifu kuliko wakati wowote wa historia yetu. Udhaifu wake unatokana kwa kiasi kikubwa na kuwa ‘compromised’.
Inapofikia mtumishi wa idara anakufa kwenye kisima cha maji Makao Makuu ya Idara pamoja na mauaji na vifo vya baadhi ya maofisa wa TISS ndani ya miaka miwili tu, inatosha kuhoji weledi, uwezo, na utendaji wa Mkurugenzi wa Idara hiyo.

(c) Kutaka Waziri wa Mambo ya Ndani awajibike au awajibishwe. Ameshindwa kuonesha uongozi na maono ya kulibadilisha Jeshi la Polisi kulifanya liwe la kisasa na siyo la kisiasa kama lilivyo sasa.

(d) Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa awajibike yeye mwenyewe kwa kuvumilia kauli za viongozi wa CCM ambao kwa kauli zao wao wenyewe wamejithibitisha kuwa wako katika mipango ya kuidhulumu CHADEMA.

      Msajili anaposhindwa kukemea na kuwawajibisha watendaji hawa, anaonekana kukibeba na tusije kushangaa na yeye akimaliza zamu yake atapozwa na ka-jiubalozi fulani 'somewhere'. Sasa yasiwe matakwa ya juu juu tu, ujio wa Rais Barack Obama ni nafasi nzuri ya kusukumikiza ajenda ya haki za kiraia na binadamu nchini na mbele ya jamii ya kimataifa. Njia mojawapo ni kutumia nafasi ya ujio huu ni kuitisha maandamano makubwa zaidi nchini yawe ya active (ya watu kuandamana) au 'passive' ya kusimamisha shughuli zote nchini dhidi ya Jeshi la Polisi na serikali endapo watajwa hapo juu hawatakuwa wameondolewa.

      Ni kwa hili tu nitaendelea kuwaunga mkono CHADEMA badala ya kusubiri kauli za kisiasa na kunyemeleana. Wanachama na Mashabiki wenu wanataka kuona mnaongoza siyo mnavaa magwanda, lakini hamuoneshi uthubutu wa kusimamia mnachoamini. Magwanda na kauli kali wakati wa mazishi mengine hazitoshi tena. Ni wakati wa vitendo.

No comments: