"Whats
going on in Tanzania? Jana usiku nilikoswakoswa kutekwa na ccm, nikajiokoa na
nikawakamtisha polisi watekaji kwa msaada wa ocd wa monduli afande Okinda na
ocs wa makuyuni. Watekaji wakashikwa wakiwa wameniblock usiku wakakutwa na
madawa ya kulevya mirungi kwenye gari dogo aina ya mark II. Maelezo yapo polisi
makuyuni lakini watekaji waliachiliwa huru pamoja na kukutwa na madawa na
kukutwa wameniblock." Mh. Nassar
"Leo ndo
inekuwa mbaya zaidi, gari langu aina ya L/C GX ikiwa imebeba mawakala
kuwapeleka kulala kusikojulikana lakini nje ya makuyuni limezuiliwa na ·agari
matatu likiwemo lile la jana barabarani katikati ya pori kabla ya kufika mto wa
mbu, dereva akafanikiwa kugeuzia porini na kutoroka wakarudi makuyuni, na mimi
nikiendesha mwenyewe ford ranger ya chama kama kuelekea tarangire
junction/babati wakanifuata lakini wakashindwa kuifukuza gari yangu nikawaacha,
niliendesha kasi ya km 180 ambayo sijawahi before. Nimeingia kwenye lodge moja
hifadhini tarangire ikawa pona yangu kwa usiku wa leo. Ni siku ya pili watawala
wanataka kuniteka, wanausalama wanajua lakini bado hawajachukua hatua."
Mh. Nasssar
"Kwenye
picha, kushoto ni mdogo wake na aliyekuwa diwani wa makuyuni msomali, katikati
ni dereva wangu, kulia ni mkuu wa kituo cha makuyuni monduli OCS na ameshika
madawa (mirungi) iliyokutwa kwenye gari yenye wasomali watatu waliotaka
kuniteka kwa maelekezo ya Lowassa". Mh. Nassar
"Ccm
hoy makuyuni. Lowasa kabeba watu toka mto wa mbu, lokisale, monduli juu chini
na kati, duka bovu, babati, longido etc. Tutarusha picha. Wameleta watu mpaka
kwa semi-trela kama zile zinazobeba ng'ombe toka usukumani. Hakika na
tumewabana. Wafanyakazi kadhaa wa halmashauri ya monduli ambaye pia nasimamia
uchaguzi wameniambia hawajawahi kuona hii monduli kwa miaka yote waliyosimamia
chaguzi ndogo na kuu." Mh. Nassar
Walikuwemo wanaume watatu wenye asili ya kisomali. Leo tena mawakala wetu wamekoswakoswa kutekwa between makuyuni na mto wa mbu.mimi nimewatoroka watekaji wengine eneo la mswakini karibu na minjingu, nikaingia kwenye hoteli ya kitalii hifadhini tarangire. Hii ni saa chache baada ya bomu la Soweto Arusha" Mbunge Joshua Nassar
No comments:
Post a Comment