Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Thursday, May 30, 2013

Upelelezi kesi ya Lema wakamilika

      Upelelezi wa kesi ya kuchochea kutenda kosa na kusababisha uvunjifu wa amani katika Chuo cha Uhasibu Njiro  inayomkabili Mbunge  wa Arusha Mjini Godbless Lema umekamilika. Wakili wa Serikali, Eliainenyi Njiro, alieleza hayo jana wakati akiomba tarehe nyingine ya kusikilizwa shauri hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Devotha Msofe.

      Aliomba kesi hiyo itajwe tena mahakamani hapo Julai 2 kwa ajili ya kumsomea Lema maelezo ya awali. Njiro alieleza kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika. Kwa upande wake, Hakimu, Msofe alikubaliana na upande wa Jamhuri pamoja na Wakili wa Lema ambaye ni  Humphrey Mtui kuwa kesi hiyo ipelekwe tena mahakamani hapo Julai 2 mwaka huu, kwa ajili ya mshtakiwa Lema kusomewa maelezo yake ya awali yanayomkabili katika kesi hiyo.


Source: Mwilolezi C. (May 2013). Upelelezi kesi ya Lema wakamilika. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments: