Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Saturday, May 18, 2013

Live updates: Mkutano wa Dr Slaa uwanja wa Kwaraa Babati



Mtakumbuka kuwa leo Dr Slaa anafanya mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kwaraa Babati mjini.

Uwanja wa Kwaraa, Babati Mjini ndipo mahali ambapo Dkt. Slaa alimnyamazisha kbs aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Makamba wakath wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010, pale alipomwambia kuwa endapo ataendelea tu kusema uongo wake, angefumua siri zake kwa nini alifukuzwa kazi ya ualimu mkuu kule Kigoma. Kuanzia hapo, Makamba hakuzungumza tena kabisa lolote kuhusu Dkt. Slaa na CHADEMA hadi kampeni zilipomalizika.

YANAYOJIRI

• Lawrence Tara, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi (kabla ya kuhamia CHADEMA mwaka huu), amemshangaa James Mbatia kubweteka na ubunge wa mezani, wakati ameshindwa kupigania ubunge halali ambao ulichakachuliwa na CCM hao hao mwaka 2010 Jimbo la Babati Vijijini (mgombea akiwa Tara). Amesema ameamua kuhamia kwa watu walio serious na mapambano ya kupigania haki na matumaini ya Watanzania. 

• Pauline Gekul: nitaendelea kuwapigania wananchi na Watanzania wenzangu wa Babati Mjini katika nafasi yangu ya Viti Maalum, sasa tunawaonesha kuwa kuchakachua ubunge wetu mwaka 2010 hakukuwasaidia.

• Kazi ya mbunge ni kuisimamia na kuiagiza serikali. Kazi hiyo naifanya nanyi mnatambua jinsi ninavyowakaba koo kwenye ardhi yetu. Nawaomba Watanzania tuache mapenzi ya mshumaa kwa CCM, kuendelea kutumika kuimulikia huku sie tukiungua na kumalizika!

• Dkt. Slaa 'watu wa Babati mimi niliwaambia hapa kuwa Chambiri alifukuzwa kwao, akaja kugombea huku. Ninyi hamkuelewa. Simseng'enyi ni vibaya kumsema mtu kwa ubaya, lakini mbunge wenu namfahamu nimekaa naye bungeni. Wakati ule alikuwa anatokea Kenya kuja bungeni badala ya kutokea kwa wananchi wake Tarime. Si ajabu tena hata hapa haonekani.

• Dkt. 'Tanzania sasa ndiyo ina bunge, anamnukuu aliyekuwa Spika wa Bunge la Kenya Francis Ole Kapalo, ambaye alikuja wkt fulani Tz kuwafanyia wabunge semina na kusema Tz hakuna bunge, kuna mkusanyiko wa mashehe na wachungaji, hadi siku ngumi zitakapowaka bungeni kwa maslahi ya wtz ndiyo atajua kuna bunge'. 

• Dkt. Slaa anasema wabunge wake kamwe hawatakaa kimya bungeni wkt twiga wanakunjwa wazima na kupandishwa ndege, tembo wanauwawa, maisha yanazidi kuwa magumu, ufisadi unaongezeka. Anasema ni unafiki kutetea amani, kuliko kuangalia rasilimali za Watanzia zikiibiwa mchana kweupe'. 

• Anasema wawatukane na kuwabeza bungeni lakini mbele ya wananchi na Mungu wametimiza wajibu na wataendelea kutimiza wajibu huo bila kurudi nyuma.

• Anasema 'CCM waendelee kuchukua na kutumia sera zetu zile zile walizobeza mwaka 2010, sisi hatuna hiyana kwa sbb tunafurahi hatimaye ni Wtz wetu wananufaika. CCM watekeleze sera zetu, wasifikiri kuwa watatufilisi, mwaka 2015 tutakuja na akili mpya kabisa na tutawashangaza!

Updates by: Mohamedi Mtoi

No comments: