KUHUSU MAPITIO YA
UTEKELEZAJI WA BAJETI YA 2012/2013 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA
YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/14
I. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, hakuna ubishi
kwamba ardhi ndio msingi mkuu wa uchumu wa taifa lolote, na kwa maana hiyo
ardhi ni msingi maisha ya mwanadamu. Ardhi ni miongoni mwa vitu vikuu
vine vinavyohitajika ili taifa liendelee. Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere aliwashi kusema “Ili taifa liendelee linahitaji watu, ardhi, siasa
safi na uongozi bora”
Mheshimiwa Spika, nimekuwa
nikijiuliza kuhusu chimbuko la umasikini uliokithiri Tanzania kwa kuzingatia
vigezo vya maendeleo alivyotoa Hayati Mwalimu Nyerere. Baada ya kufanya
marejeo ya machapisho mbalimbali lakini pia baada yakupata uzoefu wa uongozi
kama Mbunge wa Wananchi na hasa kama Waziri Kivuli kwa Arhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, na kwa kuzingatia mwenendo halisi wa watawala hapa Tanzania
nimegundua kuwa kiwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu sio watu (watu wapo
wengi sana takribani milioni 45), tatizo sio ardhi (hiyo ipo ya kutosha na
ziada takribani hekta milioni 94.3[1]).
Mheshimiwa Spika, tatizo ni “siasa
safi na uongozi bora”. Tofauti na Kauli Mbiu mkakati za kisiasa
enzi za Mwalimu, kwamba Sisa ni kilimo, Uhuru na Kazi, Kilimo cha Kufa na
Kupona, sasa hivi tunashuhudia siasa za watawala za kuongeza umasikini wan chi
hii “kwa ari na kasi zaidi, tunashuhudia watawala wakijigamba
kwamba “wamethubutu na wameweza” kuwa mafisadi wa rasilimali za
nchi hii.
Mheshimiwa Spika, maneno
niliyoyatumia hivi punde hayanifurahishi hata kidogo, lakini nimelazimika
kuyasema kwa kuwa sioni watawala wa nchi hii wakifikiri namna ya kumkomboa
mtanzania kutoka kwenye wimbi la umasikini, bali kila mmoja anajitahidi
kujilimbikizia mali hasa kwa hofu ya kuondolewa madarakani (akakosa namna ya
kuishi) kutokana na kuenea kwa kasi na kuungwa mkono kwa wingi na wananchi kwa
chama kikuu cha upinzani nchini cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mheshimiwa Spika, nasikitika
sana kwamba badala ya Serikali ya CCM kutumia muda na rasilimali ilizo nazo
kutatua matatizo sugu ya kiuchumi ya taifa hili (hususan uporaji wa ardhi ya
wananchi), inatumia fedha nyingi za umma kupambana na CHADEMA ambayo inatetea
maslahi ya wananchi.
Mheshimiwa Spika, Nchii hii
ina rasilimali nyingi sana ikiwemo ardhi ambazo zingeweza kuifanya
Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za ulimwengu wa pili kiuchumi, lakini
tuna tatizo la uhaba wa viongozi wenye “ufahamu, maadili
na busara” ya kutumia rasilimali hizi kwa maslahi ya taifa.
Mheshimiwa Spika,
kutokana na
ombwe la uongozi katika taifa hili, na kutokana na “ubinafsi, ulafi na
ufisadi” wa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi
yetu, leo taifa hili ni masikini, miaka hamsini na mbili baada ya uhuru.
Mhshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani inayoongozwa na CHADEMA imekuwa ikibainisha mapungufu na kasoro nyingi
katika masuala ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi tangu mwaka 2011 hadi
leo, lakini Serikali hii ya CCM imeendelea kuwa na shingo ngumu kuyafanyia kazi
mapendekezo ya Kambi ya Upinzani jambo ambalo linaendelea kusababisha migogoro
mingi na ufisadi katika umiliki na matumizi ya ardhi hapa nchini
Mheshimiwa Spika, katika hotuba
ya msemaji mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika bajeti ya wizara hii kwa
mwaka wa fedha 2011/2012, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilianisha matatizo
makubwa ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi na kuitaka Serikali
kutafuta ufumbuzi kwa kuchukua hatua za haraka. Matatizo hayo yalikuwa kama
ifuatavyo:-
1. Uporaji wa ardhi ya Tanzania
unaofanywa chini ya usimamizi wa Serikali kwa mbinu au hila ya uwekezaji,
2. Ufisadi wa ardhi unaofanywa na
viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi kwa kuuziana ardhi kwa bei ya
kutupwa,
3. Ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya
Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na Sheria namba 5 ya ardhi ya vijiji ambapo
viongozi wa Serikali walikuwa wakigawa ardhiki holela bila kuzingatia matakwa
ya sheria hizo,
4. Migogoro mikubwa ya ardhi baina
ya wakulima na wafugaji ambayo kwa nyakati tofauti imepelekea umwagaji wa damu
miongoni mwa wananchi,
5. Matatizo makubwa katika
tathmini ya malipo ya fidia kwa wananchi wanaotakiwa kuondoka katika maeneo yao
kupisha matumizi mapya ya ardhi,
6. Kuendelea kupanda kwa bei ya
vifaa vya ujenzi jambo ambalo limesababisha wananchi kuendelea kuishi katika
makazi duni na hivyo kuhatarisha usalama wao na kutweza utu wao,
7. Serikali na taasisi zake
kutolipa kodi za pango kwa wakati kwa Shrika la Nyumba la Taifa na hivyo
kulirudhisha nyuma kimaendeleo, na
8. Wakala wa Taifa wa Utafiti wa
Nyumba bora na Vifaa vya Ujenzi kushindwa kuleta mabadiliko kutokana na
kuongezeka kwa nyumba zisizo bora ( kama vile nyumba za tembe, tope na nyasi)
na kuongezeka kwa bei ya vifaa vya ujenzi
Mheshimiwa Spika, Aidha, katika
bajeti ya wizara hii kwa mwaka 2012/2013, Kambi Rasmi ya Upinzani iliendelea
kuipigania ardhi ya watanzania inayoporwa kwa kuitaka Serikali kufanya
yafuatayo:-
1. Kuyarejesha kwa wananchi,
mashamba yote yaliyobinafsishwa ambayo wawekezaji wameshindwa kuyaendeleza,
2. Kutatua mgogoro wa ardhi kati
ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na vijiji vya Gijedabung, Ayamango[2]
na Gedamar[3]
katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara ambapo mamlaka ya hifadhi ilitoa amri
kwa wananchi wa vijiji hivyo kuondoka kwa kuwa walikuwa wako ndani ya hifadhi,
3. Kutatua migogoro ya ardhi kati
ya wafugaji na wakulima hasa katika Wilaya ya Karagwa na Biharamulo
Mkoani Kagera ambapo wananchi walifukuzwa kwenye maeneo yao ya kilimo na maeneo
hayo kugawiwa kwa wafugaji matajiri bila wananchi kuhusishwa,
4. Kulipa fidia stahiki kwa
wananchi wanaotakiwa kuondoka katika maeneo yao kupisha matumizi mapya ya ardhi
hasa katika maeneo ya Kibamba –Luguruni, Kwembe Kati na Kigamboni Mkoa wa Dar
es Salaam,
5. Kuandaa mpango mkakati na
endelevu wa kukomesha uvamizi wa ardhi (hasa katika Manispaa ya Kinondoni )
unaofanywa na magenge ya watu wenye silaha wanaovamia maeneo ya watu,
kuharibu mali na kuyakalia maeneo hayo kwa nguvu jambo linalosababisha uvunjifu
wa amani na hatimaye vifo,
6. Kubatilisha mkataba wa kifisadi
kati Kampuni ya Uwindaji ya Game Frontiers of Tanzania Limited na Kampuni mbili
za nje za uchimbaji madini za Uranium Resourses PLC na Western Metals, kufanya
utafiti wa uchimbaji wa madini ya Uranium kwenye kitalu cha uwindaji katika
kijiji cha Mbarang’andu kinyume cha sheria.
7. Kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti
wa Kodi za Nyumba (Real Estate Regulatory Authority) ili kuratibu, kuweka
viwango na miongozo ya kodi za nyumba ili kuwaondolea wananchi wapangaji wa
nyumba adha kubwa ya gharama kubwa za pango zisizo na viwango.
Mheshimiwa Spika, baada ya
Serikali hii ya CCM kuoneka kutojali maslahi ya wananchi katika kumiliki na
kutumia ardhi yao, na baada ya kuongezeka kwa kasi ya kugawa ardhi kwa wageni
kwa hila ya uwekezaji, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA
iliendelea kupambana kuitetea ardhi ya Tanzania ili wananchi wawe wanufaika wa
kwanza wa rasilimali ardhi.
Mheshimiwa Spika, Safari hii,
Kambi Rasmi ya Upinzani ilileta hoja binafsi bungeni tarehe 8 Novemba, 2012 kwa
ajili ya hatua za kibunge baada ya Serikali kuoneka kutojali uporaji wa ardhi
ya wananchi unaofanywa kwa kisingizio cha uwekezaji.
Mheshimiwa Spika, katika hoja
hiyo, Bunge liliazimia kwamba :
1.Zoezi la ugawaji ardhi kwa wawekezaji wa nje na ndani lisitishwe
hadi hapo tathmini ya kina itakapofanyika kubaini ni kiasi gani cha ardhi kipo
mikononi mwa wawekezaji na wasio wawekezaji.
2.Tathmini ya kina ifanyike kuweza kubaini raia wa kigeni na wa
ndani waliojipatia ardhi kinyemela kupitia serikali za vijiji kinyume na
matakwa ya sheria ya ardhi Na. 5 ya mwaka 1999.
Mheshimiwa Spika, baada ya
mvutano mkali kati ya wabunge wa CCM wakiisaidia Serikali yao dhidi ya Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, hatimaye Serikali ilikubali kwa shingo upande
kufanya tathimini ya ardhi iliyoko mikononi mwa wageni lakini ilikataa
kusitisha uwagaji wa ardhi kwa wageni. Hata hivyo, Serikali ilitakiwa kuleta
ripoti ya tathmini hiyo bungeni mwezi Aprili, 2013, lakini mpaka sasa
Serikali haijafanya hivyo.
Mheshimiwa Spika, kabla
sijajielekeza katika mambo mahsusi yanayohusu wiza hii kwa mwaka wa fedha
2013/2014 napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni kuitaka Serikali ilieleze Bunge hili na wananchi wote, kwamba imetatua
kwa kiasi gani matatizo yaliyoainishwa hapo juu na imetekeleza kwa kiasi gani
mapendekezo ya Kambi Rasmi ya Upinzani yaliyoorodheshwa hapo juu (moja baada ya
jingine) ya tangu mwaka 2011 hadi leo?. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,
inayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikali kulieleza Bunge hili imetekeleza vipi
maazimio ya bunge ya tarehe 8 Novemba, 2012 yaliyoitaka Serikali kufanya
tathmini ya ardhi iliyopo chini ya umiliki wa wageni (wawekezaji) na kuleta
taarifa ya tathmini hiyo bungeni mwezi Aprili, 2013?
Mheshimiwa Spika, ni masikitiko
yangu kwamba mpaka nawasilisha bajeti hii, licha ya kupeleka taarifa ya
maandishi kwenye ofisi yako nikikutaka uielekeze serikali kuwasilisha ripoti
husika mbele ya Bunge hili tukufu ,ili kuliwezesha Bunge kufanya maamuzi ya
msingi/muhimu katika sekta ya ardhi sioni jitihada zozote za kuleta ripoti hiyo
katika mkutano huu wa bunge.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo,
Taarifa ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imezipata, ambazo
tunaamini ndicho chanzo cha serikali kushindwa kuleta ripoti kwa wakati ni
kushindwa kwa timu iliyopewa jukumu la kuzunguka nchi nzima kufanya tathmini
kushindwa kumaliza kazi ndani ya muda iliyopewa, sambamba na kukumbana na
upinzani mkubwa wa kupata taarifa kutoka kwenye mashamba ambayo yanamilikiwa na
viongozi na vigogo wakubwa serikalini!
II. UWEKEZAJI KATIKA ARDHI YA TANZANIA
Mheshimiwa Spika, Tanzania
ina ukubwa wa Zaidi ya Km2 940,000. Kwa mujibu wa sheria za ardhi
na 4 na 5 za 1999 ardhi ya Tanzania imegawanyika katika makundi 3
ambayo ni ardhi ya Jumla, ardhi ya kijiji na ardhi ya hifadhi. Hadi sasa ardhi
ya hifadhi inaelezewa kufikia zaidi ya 30% ya ardhi yote. Ardhi yenye
rutuba na inayofaa kwa kilimo cha aina mbali mbali
inakadiriwa kufikia hekta milioni 80, eneo linalotumika kwa sasa
linakadiriwa kufika 10% tu.
Mheshimiwa Spika, shughuli za
uwekezaji huongozwa na sheria ya uwekezaji ya mwaka namba 26 ya
1997. Hata hivyo sheria ya ardhi inatamka wazi kuwa wasio
raia wa Tanzania hawaruhusiwi kumiliki ardhi isipokuwa kwa matumizi ya
uwekezaji ambapo hupewa hati hafifu kupitia kituo cha uwekezaji (TIC)
Mheshimiwa Spika, pamoja na
katazo hili la kisheria, tumeshuhudia mara nyingi wawekezaj
wasio watanzania wakimiliki ardhi,wakiwaondoa wamiliki wa asili katika
maeneo yao na kuharibu kabisa mifumo yao ya maisha.Hii mara nyingi imetokea kwa
sababu ya kukiuka kwa makusudi sheria na taratibu zilizopo , udhaifu wa mifumo
ya utekelezaji wa sheria na dharau kwa vyombo vya ngazi za chini za
utawala na wananchi wao kwa kuwa maamuzi hufanywa na ngazi za juu.
Mheshimiwa Spika, ingawa karibu
kila eneo limevutia wawekezaji wa aina fulani katika ardhi, lakini maeneo ya
uchimbaji madini, shughuli za wanyhama pori (kama vile uwindaji, mahoteli, na
utalii) pamoja na kilimo yameonekana kuwavutia zaidi wawekezaji.
Mheshimiwa Spika, katika Kilimo,
ambako kuna wazalishaji wadogo, shabaha ya hivi karibuni imekuwa ni kuwekeza
kwenye kilimo cha “nishati uoto” kwa ajili ya mafuta ya magari na
mitambo. Jambo la kutilia shaka ni kwamba; wawekezaji wengi sasa wanaenda
vijijini kutafuta ardhi wenyewe badala ya kupewa na kituo cha uwekezaji kama
sheria inavyotaka. Kutokana na wanavijiji kutokuwa na uwezo wa kimaarifa
na ujuzi wa kujadiliana na wawekezaji kwa mizania sawa, wamekuwa wakitoa ardhi
kiholela bila kufuata taratibu za kisheria .Pale ambapo
wanavijiji wamethubutu kuhoji, sheria imetafsiriwa vibaya kuwapora
ardhi na haki yao. Kwa mfano; sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 inaeleza
kwamba: ardhi ya kijiji isiyotumika, wala kukaliwa, ni ardhi
ya jumla na hivyo inaweza kuchukuliwa na serikali kuu wakati wowote
ingawa ukweli unabaki pale pale kuwa ni ardhi ya kijiji.
III. UKADIRIFU NA TATHMINI YA
WAMILIKI WA MASHAMBA TANZANIA BARA 2013
Mheshimiwa Spika, kikosi kazi
kilichopewa kazi na Wizara ya Ardhi , kilipewa jukumu la kufanya tahmini nchi
nzima ya watu wanaomiliki mashamba makubwa .Mashamba yaliyofanyiwa tathmini ni
yale tu yenye ukubwa zaidi ya ekari 50 (Hekta 20).
Malengo ya Tathmini:
i) Kufanya uchunguzi wa mashamba ya wawekezaji wa ndani na wa nje
yaliyopatikana kwa njia halali na ambazo sio halali,
ii) Utaratibu uliotumiwa na wawekezaji kupata mashamba
iii)Kuangalia uhalali wa umiliki (kwa wenye hatimiliki)au ukodishaji wa
mashamba,
iv) Kutambua tozo mbali mbali (land rent,fees,levies) za ardhi au malipo
mengine yeyote yananayotakiwa kulipwa kutoka katika mashamba husika,
v) Kutambua matumizi ya ardhi, kama yanaendana na matakwa ya Mkataba,
vi)Kutambua maendelezo yaliyofanywa katika mashamba husika, kama yapo!
vii)
Kutambua migogoro ya ardhi (kama ipo) kati ya wamiliki wa mashamba na
wanavijiji na hatua ambazo zimeshachukuliwa/zinazochukuliwa kutatua migogoro
husika
viii)
Kutambua faida iliyotokana na uwekezaji na kwa namna vijiji vinavyowazunguka
wawekezaji vimenufaika kutokana na uwekezaji huo!
Mheshimiwa Spika, tathmini hii
ilikuwa muhimu kutokana na ukweli kwamba ongezeko la mahitaji ya
chakula duniani, nishati mbadala, mali ghafi, mbao na uhifadhi wa misitu
imesababisha ongezeko kubwa la uhitaji wa ardhi duniani . Uhitaji huu ndio unazisukuma kwa kasi kubwa nchi zilizoendelea kuja Afrika kutafuta
ardhi.
Mheshimiwa Spika, watafiti
hawakutembelea nchi nzima, walitembelea wilaya 79 tu! na kukagua
mashamba 763 tu (sampling). Licha uchache wa maeneo yaliyotembelewa
ripoti hii sio ya kupuuzwa kwa kuwa inatoa sura ambayo,yawezekana ikawa ndio
hali halisi ya maeneo mengine ya nchi.
Utafiti umegundua yafuatayo:
1) Umiliki.
Imegundulika kwamba katika mashamba makubwa 763
yaliyotembelewa, mashamba 455 sawa na 65.8% yalikuwa yanamilikiwa na
watanzania wenyewe (individual ownership), ikilinganishwa na 14 (2%)
yaliyokuwa chini ya umiliki wa raia wa kigeni . Mashamba yaliyokuwa
yanamilikiwa kwa ubia kati ya watanzania na wageni yalikuwa 31
(4.4%).
Hata hivyo, licha ya raia wa kigeni kuwa na mashamba machache
kiidadi walikuwa wanamiliki maeneo makubwa ya ardhi
ukilinganisha na watanzania. Timu ya uchunguzi imebainisha kwamba hali hii
inatakiwa iangaliwe kwa jicho pana!
Kielelezo Na. 1
|
Aina ya umiliki
|
Wastan wa ukubwa wa shamba
|
Idadi ya Mashamba
|
Jumla (Ekari)
|
% ya eneo lote
|
|
|
|
|
Kampuni zinazomilikiwa na watanzania
|
2,972.03
|
72
|
213,986.38
|
23.71
|
|
|
|
|
Kampuni zinazomilikiwa kwa ubia kati ya watanzania na wageni
|
3,091.66
|
31
|
95,841.37
|
10.62
|
|
|
|
|
Kampuni za Kigeni
|
6,301.55
|
31
|
195,348.04
|
21.65
|
|
|
|
|
Mashamba yanayomilikiwa na watanzania (individuals)
|
280.59
|
455
|
127,669.61
|
14.15
|
|
|
|
|
Mashamba yanayomilikiwa na wageni (individual)
|
2,547.18
|
14
|
35,660.50
|
3.95
|
|
|
|
|
Mashamba yanayomilikiwa na Taasisi
|
2,049
|
63
|
129,108.09
|
14.31
|
|
|
|
|
Mashamba ambayo hayajulikani ya nani
|
4,191.58
|
25
|
104,789.39
|
11.61
|
|
|
|
|
Jumla
|
1,305
|
691
|
902,403.38
|
100
|
|
|
|
Mheshimiwa Spika, utafiti
umeonyesha kwamba kuna tofauti kubwa sana ya umiliki wa mashamba makubwa kati
ya raia wa kigeni na watanzania. Wakati watanzania (mmoja mmoja) wanaonekana kumiliki
60% ya ‘mashamba’ yote yaliyotembelewa, mgao wao katika jumla kuu ni ekari 127,670
ambayo ni sawa na 14% ya eneo lililofanyiwa utafiti. Wakati huo huo,
makampuni yanayomilikiwa na wageni, ambayo wana miliki asilimia 4% tu
ya idadi ya mashamba yaliyotembelewa, lakini wanahodhi/miliki eneo lenye
ukubwa wa Zaidi ya 21% (ekari 195,348 ) ya ardhi yote
iliyofanyiwa utafiti. Mashamba yanayomilikiwa na makampuni ya
kitanzania ni ekari 213, 986 tu.
Mheshimiwa Spika, kwa wastani
makampuni ya kigeni wana maeneo makubwa ya mashamba , yakifuatiwa na
makampuni yanayomilikiwa kwa ubia baina ya watanzania na raia wa kigeni. Ni
muhimu hapa ikaeleweka kwamba, katika makampuni ambayo watanzania inasemekana
wana ubia, hisa zao ni finyu sana kati ya (1%-10%)..ya hisa zote.
Mheshimiwa Spika, utafiti
umeonyesha pia kwamba; wakati raia wa kigeni kwa wastani
wanamiliki shamba lenye ukubwa wa ekari 6,302, raia wa kitanzania
kwa wastani wanamiliki shamba lenye ukubwa wa ekari 280 tu!
Aidha, mashamba mengi ya raia wa kigeni yalikuwa na ukubwa
unaokaribia ekari 1,526, ambao ni mara 18
zaidi ya mashamba yanayomilikiwa na watanzania. Wataalam hao wanazidi
kusisitiza kwamba: ni ukweli usiofichika kwamba:
umiliki wa mashamba makubwa umetawaliwa na raia wa kigeni.
Mheshimiwa Spika, ni muhimu wabunge
na wananchi wakaelewa kwamba; kinachozungumziwa hapa ni
mashamba ambayo tayari yana hati miliki (miaka 33, 66 au 99) na
sio ardhi za vijiji ambazo ( kisheria ziko chini ya vijiji)lakini
zinaweza kubadilishwa wakati wowote na kupangiwa matumizi mengine pasipo kijiji
kuwa na mamlaka ya kuzuia. Hii inashabihiana kabisa na utafiti
uliofanywa na Oxfarm uliobainisha kwamba katika nchi zinazoendelea kuna
zaidi ya ekari 203 milioni ambazo ziko chini /zimechukuliwa
na raia/wawekezaji wa kigeni.
Mheshimiwa Spika, baadhi ya
mashamba yaligundulika kwamba yanamilikiwa na maafisa
waandamizi wa serikali, ambao taarifa za mashamba yao zilishindwa
kupatikana katika utafiti huu wa serikali, chini ya usimamizi wa wizara
ya ardhi kwa sababu wamiliki husika hawakuwepo kwenye
mashamba yao na walinzi wao hawakuwa tayari kutoa taarifa za mashamba
husika zaidi ya kutaja majina ya wamiliki wa mashamba!hii ilitokea
Dakawa, na ilihusisha mashamba 28! Ni azma ya Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni kuwataja wamiliki wa mashamba hayo, kama serikali itagoma kufanya
hivyo!
Mheshimiwa Spika, katika kile
ambacho hakikutarajiwa uchunguzi umebaini kwamba kuna makampuni ya kigeni na
raia wa kigeni wanaomiliki ardhi kimila (customary land right)
ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi, ni maalum/ mahsusi kwa raia wa
Tanzania pekee mpaka pale ambapo ardhi husika itahuilishwa (transferred from
one category to another). Huu ni uvunjwaji mkubwa sana wa sheria ya
umiliki ardhi kimila… Aidha, utafiti umegundua pia kwamba; wageni
wanamiliki ardhi ambayo haijulikani iko kwenye kundi gani (‘the unspecified
category’) la ardhi ambayo ina ukubwa wa ekari 94,360 (10%ya ardhi iliyofanyiwa
utafiti).
Mheshimiwa Spika, ni jambo la
kusikitisha na kushtua sana kama ardhi yenye ukubwa kiasi hicho iko mikononi
mwa wawekeaji wa kigeni. Aidha, ni jambo la kushangaza sana kama Wizara
haifahamu kiasi kikubwa hivyo cha ardhi kiko katika himaya ya nani? Kama wizara
au mamlaka zilizo chini yake hazijui jambo hili , ni nani atakaye jua?
IV. MUDA WA UMILIKI WA MASHAMBA
Mheshimiwa Spika, utafiti
umeonyesha sehemu kubwa ya makampuni ya kigeni au raia wa kigeni wanaomiliki
ardhi ndio wanaoongoza kwa kuwa na mikataba ya muda mrefu ya umiliki
wa ardhi, yaani miaka 99! (ekari 500,135 kati ya 902,403
zilizofanyiwa utafiti). Halika dhalika utafiti umegundua pia kuna
wawekezaji ambao wana umiliki wa ardhi wa kimila (Customary Right of
Occupancy). Kitu aambacho ni kinyume kabisa na sheria za nchi , ambazo
zinampa fursa Mtanzania tu kuwa na umiliki wa aina hiyo!
V. UPORAJI WA ARDHI
Mheshimiwa Spika, imebainika
pia kwamba watu wenye fedha na watu wenye ushawishi wa kisiasa wamekuwa
wakitumia nguvu zao kushawishi na kupoka ardhi za vijiji , katika
mazingira ambayo hakuna ushirikishwaji wa wanakijiji (55.11% ya maeneo
yaliyotembelewa, wanakijiji waliohojiwa walikiri hakukuwa na
ushirikishwaji wakati ardhi yao inapochukuliwa). Ushawishi husika ni
pamoja na kutoa ahadi za uongo na hongo kwa viongozi wa serikali za vijiji kama
ilivyotokea kwa makampuni ya Bioshape (Wilaya ya Kilwa na Sun
Biofuels- Wilaya ya Kisarawe).
Mheshimiwa Spika, utafiti pia
iligundua kwamba fidia kwa wananchi wanaoondolewa kwenye maeneo yao ili kupisha
uwekezaji kama ilivyoelekezwa na kifungu 34(3)b cha
sheria ya ardhi, namba 4 ya 1999 hailipwi.
VI. TOZO ZA
ARDHI ( LAND RENT , FEES,LEVIES AND OTHER PAYMENTS)
Mheshimiwa Spika, kifungu cha
33 cha Sheria ya Ardhi (Sheria na 4,ya mwaka 1999) kinatamka kwamba ,
mwenye hati miliki anatakiwa, pamoja na masharti ya vifungu vingine vya
sharia, kulipa kodi ya mwaka kama ilivyoelekezwa na Sheria ya
Fedha za Umma (Public Finance Act). Utafiti umegundua kwamba kati ya mashamba
763 yaliyotembelewa, ni mashamba 278 (36.4%) tu ndio yaliyolipa kodi ya ardhi
(2012) kama sheria inavyotaka. Wamiliki wa mashamba 432 (56.6%) waliohojiwa
walikiri kwamba hawajalipa kodi husika. Halikadhalika utafiti umegundua
kwamba 43.47% ya wenye mashamba waliohojiwa walikiri kwamba hawajawahi
kulipa kodi ya ardhi toka walipomilikishwa mashamba hayo!. Hii inaonyesha
kwamba , hata wale watu ambao wanamiliki ardhi kihalali, uhalali wa
umiliki wao una mashaka kutokana na kutokidhi takwa muhimu la kumiliki
ardhi husika ambalo ni ulipaji wa kodi ya ardhi. Zaidi ya hayo, utafiti
umeonyesha pia kwamba; mashamba 643 kati ya 763
yaliyotembelewa yalishindwa kutoa ushahidi (risiti) kuonyesha kama ni kweli
walikuwa wanalipa kodi za ardhi kama matakwa ya kisheria yanavyoelekeza.
VII. UWEKEZAJI KATIKA NISHATI UOTO (BIOFUELS) NA MUSTAKABALI WA
ARDHI YA WATANZANIA
Mheshimiwa Spika, kupanda kwa bei
ya mafuta katika soko la dunia na mabadiliko hasi ya hali ya hewa
duniani vimechangia kwa kiasi kikubwa wimbi la utafutaji nishati
mbadala ili kukabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa na pia kuleta
uhuru katika matumizi ya nishati. Kuanzia miaka ya 2000, matumizi ya
nishati yalianza kushika kasi sana katika maeneo mbali mbali duniani. Kwa
Tanzania, tangu nishati hiyo ianze kuchukua mkondo wake
ikiwahusisha wawekezaji wakubwa na wadogo , ujio wake umeshuhudia kiasi
kikubwa cha ardhi kikichukuliwa kwa ajili ya mashamba ya kuzalisha
nishati hiyo.
Mheshimiwa Spika, watetezi wa Nishati
Uoto, wamekuwa wakiipigia chapuo aina hiyo ya nishati kwa kutaja faida zake
ambazo ni pamoja na kuzalisha na kukuza ajira kwa wananchi waishio maeneo
yalipo mashamba au viwanda vinavyozalisha aina mbalimbali za nishati hiyo,
kuongeza mapato kwa wakulima wadogo na kupambana na gesi zijulikanazo
kama Green house gases (GHG). (Wizara ya Nishati na Madini, 2006)
Mheshimiwa Spika, maeneo kadhaa
nchini yamekuwa katika utekelezaji wa miradi ya mashamba ya kuzalisha Nishati
Uoto kama vile Kilwa, Kisarawe, Bagamoyo, Arusha, Manyara, Shinyanga, Singida
na Mwanza. Tokea makampuni haya ya kigeni,yalipokabidhiwa ardhi ya watanzania
kama njugu, na katika mazingira mengine chini ya ukuwadi wa Kituo cha uwekezaji
nchini hakuna faida “endelevu” iliyopatikana zaidi ya kuongezeka kwa migogoro
ya ardhi kati ya wawekezaji na wanavijiji na kutamalaki kwa rushwa,
udanganyifu, hadaa na mizengwe miongoni mwa watendaji wa vyombo
vinavyosimamia masuala ya ardhi, wananchi na wawekezaji.
Mheshimiwa Spika, taratibu nyingi
za ugawaji na uhawilishaji wa ardhi zilikiukwa makusudi kwa lengo la
kuwapendelea wawekezaji hasa wa kigeni. Katika maeneo ya uwekezaji, mifumo ya
maisha ya wananchi imehatarishwa kwa kunyang’anywa ardhi walizokuwa wakitumia
kwa shughuli za kilimo, malisho na shughuli nyinginezo za uzalishaji na za
kijamii. Wale waliobahatika kupata ajira katika kampuni za wawekezaji nao
wameachwa njiani hawajui kesho yao baada ya wawekezaji kuwaachisha kazi na
wengine kususa miradi yao, kuwatelekeza wafanyakazi na kutokomea
kusikojulikana.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa
taratibu za kisera na kisheria nchini ni dhaifu katika usimamizi wa Nishati
Uoto, uanzishwaji wa miradi ya nishati hii nchini kwa kiwango fulani
umesababisha kuwapo kwa unyonyaji wa rasilimali muhimu za taifa ambazo ni
ardhi, maji,misitu na nguvu kazi ya watanzania.
VIII. HALI YA MASHAMBA WALIYOPORWA WANANCHI NA KUKABIDHIWA
WAWEKEZAJI KWA KILIMO CHA MAZAO YA NISHATI UOTO (BIOFUEL)
Mheshimiwa Spika, uchunguzi
umebaini kuwa katika wilaya ya Kilwa,mwekezaji alikuwa kampuni iitwayo Bioshape
kutoka nchini Uholanzi. Kampuni hii ilipewa ardhi yenye ukubwa wa
hekta 80,000 kwalengo la kulima zao la mbono kaburi.Ardhi hiyo
ilihusisha vijiji vine ambavyo ni Mavuji, Migelegele,Liwiti na
Inokwe. Mwekezaji hakuwahi kulima eneo lote bali alilima hekta 800 ambazo
ni shamba la mfano lililopo katika kijiji cha Mavuji.
Mheshimiwa Spika, dhana ya
uwekezaji ni jitihada za kugeuza mali asili za nchi
kuwa katika rasilimali kwa kutumia nyenzo kama mtaji , teknolojia
na nguvu kazi. Ziada inayotokana na uzalishaji hurejeshwa katika
kuimarisha miundombinu , mitaji, teknolojia na rasilimali watu ( watu,
fedha, malighafi ) ili faida iweze kupatikana na pale inapopatikana
faida ndipo matunda ya maendeleo huonekana!
Mheshimiwa Spika, kama ambavyo
tulifanya makosa ya kutokulinda maslahi ya watanzania katika uvunaji wa madini
mbali mbali yanayopatikana nchini, na kama ambavyo tunaelekea kufanya makosa
katika uvunaji na nishati muhimu ya gesi , ama kutokana kuwa na viongozi wasio
na upeo/wabinafsi/wanaoendekeza njaa/waliokosa uzalendo kutokana na nchi yetu
kutokuwa na intelijensia ya kiuchumi, nchi yetu imejikuta
ikikaribisha wawekezaji wa hovyo,wasio na mitaji, teknolojia wala nguvu kazi!
Mheshimiwa Spika, serikali
ilikaribisha makampuni ya kigeni pasipo hata kuandaa sera kwa ajili ya
nishati uoto. Sote tunafahamu fika kwamba sera ndio dira, na
mwongozo utakaoelekeza nini kifanyike,kwa namna gani na malengo yapi.
Uzembe huu umelisababishia Taifa na vijiji vilivyoporwa mashamba yao hasara
kubwa. Ikumbukwe kwamba katika maeneo mengi kama sio yote wananchi walipoteza
ardhi yao pasipo kulipwa fidia,waliolipwa fidia walilipwa kidogo sana,ajira
zilizopatikana katika mashamba hazikuwa endelevu. Maeneo yaliyokuwa mapori huku
yakiwanufaisha wananchi kwa kufanya shughuli za kijamii kama
kupata miti ya dawa ,kuchota maji,kukata kuni na shughuli nyingine za kijamii
na kiuchumi, hivi sasa yamegeuka kuwa majangwa ). Na katika mazingira
mengine vijiji vilikumbwa na njaa kwa sababu ardhi waliyokuwa wakiitumia
kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo, walipewa wawekezaji ambao walijikita
katika uzalishaji wa mibono!
Mheshimiwa Spika, kutokana na
uzembe wa serikali, wawekezaji waliokuja kwa ahadi kemkem waliiishia kutelekeza
mashamba.
Mheshimiwa Spika, kwa ufupi naomba Bunge lako tukufu lipate
taarifa juu ya hali ya maelfu ya hekta ya ardhi zilizoporwa kwa wanakijiji, kwa
mabavu kulikoenda sambamba na kuvunjwa kwa sheria kwa makusudi : Naamini
taarifa hii itapelekea Bunge lako tukufu, kutoa au kufanya maamuzi yenye busara
kwa manufaa ya taifa na wananchi wake:
1. Sun Biofuel (Mwekezaji toka
Uingereza) alipewa eneo la – Kisarawe ardhi ya vijiji 11
( hekta 8200-9000) kwa miaka 99, akiahidi kutengeneza ajira 5000.
Walianza kusafisa eneo kwa ajili ya kupanda mazao mwezi Juini, 2009,na
kufanikiwa kupanda hekta 600 ilipofika Novemba, 2009. Waliahidi kusaidia
wakulima wadogo wadogo wa pembezoni, ahadi ambayo haikutimia mpaka
walipositisha shughuli za uwekezaji (HAKIARDHI). Mwaka 2011 eneo husika
liliuzwa kwa mwekezaji mpya 30 Degree ( ubia kati ya Raia wa Mauritania
90% na Mtanzania 10%. Mwaka 2012 kampuni ilifilisika .Imeachisha kazi ghafla
wafanyakazi 750..ahadi zake zote za kiuchumi na kijamii zilizoahidiwa zikaishia
hapo…
2. Africa Biofuel & Emmission Reduction Co. (Tanzania Ltd).Ardhi
waliyopewa hekta 60,000 , wilaya ya Biharamulo (Biofuel) Taarifa za serikali zinaonyesha ,kampuni ilisimamishwa na ofisi ya makamu
wa Rais kutokama na masuala yanayohusiana na masuala ya ardhi (
locher 2010)/wako kwenye hatua za mwisho za kumilikiswa eneo na
walitaraji ingia mkataba 2010.
3. Agrisol energy Tanzania ( ubia kati ya Serengeti
Adivisors ltd na Agrisol Energy LLC / group (IOWA based ) . Mshirika: Pharos Global Agricultures Fund, chini ya usimamizi
wa Pharos Financial Group (Dubai), wilaya ya Mpanda –Rukwa na Kigoma
(Oakland Institute) Mchakato wa kupata eneo la Rukwa bado unaendelea (
325117 ha). Eneo ambalo limeshakabidhiwa kwa mwekezaji hekta10,000(
Lugufu) na 3250 (Basansa)- kigoma .Agrisol Energy Tz inamiliki 25% ya
hisa za kampuni. Kampuni hii imeungana na Kampuni ya Kitanzania the Serengeti
Advisors (Inayoundwa na vigogo/viongozi wastaafu wa serikali wenye ushawishi
mkubwa sana kwenye serikali ya CCM) ili kuhakikisha kampuni inapata
ardhi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mpanda ( Baha 2011).
4. Agro Forest Plantation ( Misri), Rufiji ,(kilimo cha sukari kwa soko la Misri na la
ndani) ardhi waliyoomba ni hekta 10,000 iliyopo ni hekta
8,000 (RUBADA) , Ilikuwa ardhi ya Kijiji (Mojoro,Chumbi A,B,C na
Ruma Villages ,imeasjiliwa na TIC Desemba, 2011, na
inatarajiwa kuanza kazi Desemba 2014
5. Arkadia Ltd (Italia),
imesajiliwa Brela Septembe 2007 , Wilaya ya Mkinga( jatropha ), Wilaya
iliidhinisha hekta 500, wizara ya adhi imesajili/register hekta
25,000 ( Project bado ina utata ,maofisa wa wilaya hawaelewi ni
vigezo gani na kwa utaratibu upi kampuni iliweza kupewa na wizara ya
ardhi hekta 25,000 (Sulle 2012)
6.Bagamoyo Eco Energy Ltd. (Eco Energy Tanzania Ltd). Kampuni hii ina mchanganyiko wa wamiliki toka mwaka 2009. Eco
Energy Bagamoyo[12]
inamilikiwa kwa 100% na Agro EcoEnergy Tanzania (ambayo nayo inamilikiwa
93.5% na EcoEnergy Africa AB, na 5% Tanzania Petroleum
Development Co Ltd.(TPDC ) na 1.5% Community Finance Corporation
Ltd(CFC).
EcoEnergy Africa nayo inamilikiwa na Eco Development
Europe AB , mwanahisa mdogo wa SEKAB (SEKAB ndiye alikuwa mmiliki wa awali
,kabla ya kushindwa kuendelea na uwekezaji kisha kuikabidhi ardhi kwa kampuni
nyingine ya Sweden EcoEnergy October 2009 , mwaka 2010 Eco
Energy inaunda Kampuni nnyingine, Bagamoyo EcoEnergy Ltd-Kampuni tajwa hapo
juu!).
TPDC inamilikiwa kwa 100% na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na CFC ina milikiwa na watanzania watatu. Kampuni
inamiliki hekta 8000. Kwa makubaliano ya sasa Eco Energy watapata
mkataba wa miaka 99 na fursa ya kutumia ardhi kwa uhuru kwa kuipatia serikali
25% ya hisa za Kampuni na ujumbe wa Bodi.
7. Bio shape Tanzania ltd (Dutch)- Kilwa-Lindi
(Jatropha), hekta 81, 000. Kampuni
imefilisika mwishoni mwa mwaka 2009, imefanikiwa kusafisha eneo lenye
ukubwa wa hekta 70 (Simeye 2011). Kampuni ilianza kufanya biashara ya Magogo
badala ya kulima. Baada ya shughuli zenye utata na hatimaye kufilisika kwa
kampuni hii, inasemekana kuwa wawekezaji wapya toka Netherlands,
Uingereza, Marekani na Italia wanataka kuuziwa eneo husika na BIOSHAPE
(Valentino 2011).
8.Bio Energy Tanzania ( Mtanzania na Mcanada), amepewa hekta 4500.
Kilimo cha Jatropha , ardhi ya vijiji (Vigwaza na Kidogozero). Bado
haijaanza uzalishaji kicha ya kukabidhiwa ardhi,pia kuna mgogoro mkubwa wa
ardhi baada kijiji cha awali kugawanywa mara mbili ,kijiji kipya hakikuhali
eneo lake kuchukuliwa na mwekezaji (Sulle 2012)
9. CAMS Agrienergy Tanzania Ltd. Inamiliki
hekta 45000 .Katika maeneo ya Handeni na Bagamoyo . Mpango ukia ni
kuzalisha lita 250 milioni za Ethanol na umeme wa 120MW (Oakland
Institute 2011a) .Kutokana na mgogoro wa fedha mpango
ulipunguzwa kukiwa na malengo ya kuzalisha lita milioni 20 kwenye hekta
18,000. Kampuni iko kwenye mipango wa kuanza uzalishaji. Kwa sasa nguvu
wamezielekeza miradi yao huko Uganda na Kenya!
10. Eco Carbon (French) - Zamani
ikiitwa (Diligent Tanzania Ltd)- Bagamoyo kilimo cha Jatropha
.Waliomba hekta 75000, bado hawajakabidhiwa ardhi.
11.Euro Tech ( ya Korea). Ina mpango
ya kulima hekta 100,000 za Jatropha na Castor Oil for
biodiesel , wanaanza na hekta 10,000 na wana mpango wa kuwekeza dola za
kimarekani milioni 20
12. Eurovista Trading Co. Ltd ( ya India), Kampuni hii imepewa
hekta 6,000 za ardhi ya Kijiji, kwa ajili ya
kilimo cha mahindi. (Inasemekana kwamba alikuwa kwa madhumuni ya kulima
pamba, lakini amekuwa akilima mahindi toka 2006).
13. FELISA (Farming for energy for better Livelihoods in
Southern Africa) Kampuni hii ni ubia kati ya
Tanzania na Ubeligiji. Hawa walipewa hekta 4,258 huko Kigoma kwa ajili ya
kilimo cha nishati joto kwa soko la ndani. Wananchi
hawakushirikishwa ipasavyo katika suala hili na matokeo yake ni kwamba vyanzo
vya maji vimezuiwa na mwkezaji (LEAT 2011).
14. FJS African Starch Development Ltd. ( ya
Kimarekani), Hawa waliomba hekta 5,000 za
ardhi ya vijiji vya Nyambili na Nyambunda huko Rufiji kwa ajili ya Kilimo
cha Mihongo. (Rubada 2012).
15.Green Resourses Ltd ( Subsidiary of Green
Resources SA (ya Norway), mwekezaji huyu anamiliki hekta 20,434 zikiwa ni ardhi ya
kijiji huko Mufindi, kwa ajili ya upandaji wa misitu, uzalishaji wa
nishati , na uuzaji wa mbao.
16. Green Resources Ltd. (ya Norway), hawa wanamiliki shamba kubwa la Kilombero Forest
Plantation, lenye ukubwa wa hekta 12,121. Wamepeleka maombi ya
ziada hekta 10,000, na maombi hayo yamepata Baraka za Halmashauri ya Wilaya,
ila kibali cha Kamishna wa ardhi kinasubiriwa (Sulle 2012)
17.Kagera Sugar Plantation (Mhindi na Mtanzania), hawa wamepewa hekta 7,000 huko Misenyi kwa ajili ya
kuzalisha sukari, hata hivyo kiasi cha ardhi kinachotumika ni hekta 300
tu
18. KYC Mpanga Co. Ltd (Kilimo cha Yesu) ya Switzerland, Kampuni hii ilipewa hekta 3,000 za ardhi ya
kijiji huko Kilombero kwa ajili ya Kilimo cha Mpunga. Baada ya kupata hasara
mwaka 2004, kampuni hii ilianza kukodisha mashamba kwa wakulima wadogowadogo
kwa shilingi 170,000/= kwa heka moja.
19. Kilimanjaro Aloe Vera Plantation Ltd (Mwingereza), huyu alipewa hekta 400 kwa ajili ya kulima jatropha lakini
baadaye alibadili mpango na kuanza kulima Aloe Vera. (Mwamila et al. and
Bengesi et.al 2009)
20.Kilombero Plantations Ltd (KPL), subsidiary fo AGRICA Ltd. Kampuni hizi zilipewa hekta 8,000 katika bonde la Mto Rufiji kwa
ajili ya kilimo cha Mpunga (Chachage 2010). Mwaka 2010, AGRICA
ilipewa tuzo ya Mwekezaji wa Kimkakati wa Kitaifa na Serikali. Ni kampuni
inaoongoza Afrika Mashariki kwa uzalishaji wa mchele.
21.Kilombero Sugar Company Ltd. (Afrika Kusini hisa 55% - Ilovo Sugar Plantation , mwingereza
hisa 20% ED &F Man, na Serkali ya Jamhuri ya Muungazo –Tanzania, hisa 25%).
Hawa wana hekta 8,000 za ardhi ya vijiji vya Msolwa Station, Hifadhi ya Selous,
Gombala na Nyange.
22. Kilomero Valley Teak Co. (Finland), hekta 4,748 - Kilombero –Ulanga [17].
23. Korean Rural Community Cooperation (KRC) ( Korea Kusini na
RUBADA). Hawa wana hekta 15, 000 za ardhi
kwa ajili ya kilimo cha Mpunga huko Rufiji (Oakland Institute
2011a;Daily News & RUBADA 2012). Mwaka 2010, kampuni hii ilipanga
kuwekeza Dola za Kimarekani 50 milioni.
24. Lindi Forests LTD (Subsidiary of Green Resources
SA(Norwegian). Kampuni hii inamiliki hekta 13,000
za ardhi huko Lindi. Kiasi cha hekta 600 tu zilikwa zimelimwa na kupandwa mazai
mpaka 2009.
25. Lukulilo Farm Holdings (ya Uingereza) ina jumla ya hekta 5,000 za ardhi ya vijiji vya Ndundunyikanza,
Nyaminywili na Kipo – Rufiji. Kampuni imesajiliwa na TIC, 10/11/2011 na
Itaanza kazi Novemba 2014.
26.Mufindi Paper Mills (Mhindi), huya amepewa kibali cha kumiliki hekta 10,000 na
Halmashauri ya Wilaya kwa ajili ya Kilimo cha Mbao laini huko Kilombero,
27.Nava Bharat Africa Resources PVT Ltd. (NBAR) (Mhindi), huya ameomba hekta 10,000 za ardhi ya kijiji huko kwa
ajili ya kilimo cha Michikichi ili kuzalisha mafuta ya Mawese,( RUBADA 2012-
Sulle).
28. Pharos Financial Group ( Kampuni binafsi UAE)-Pharos Miro Agriculture Fund – hawa wamepewa hekta 50,000
kwa ajili ya kilimo cha Mpunga ila Kampuni hii haijasajiliwa Brela (Bakr 2010-
Reuters article )
29.Rufiji Sugar Plant (mwekezaji wa nje, asili yake haifahamiki, (RUBADA 2012), hawa wana hekta 12,132 ikiwa ni ardhi ya
vijiji vya Tawi, Nyamwange na Utunge – Rufiji. Wanatumia ardhi hii kwa kilimo
cha sukari, Kampuni imesajiliwa na TIC 9/5/2012. Itaanza ifikapo shughuli zake
Mei, 2015 (DAO 2012- Sulle2012)
30.SAP Agriculture Ltd.(Uturuki), Kampuni hii ina hekta 5,000 za ardhi ya kijiji (Nyamwange na
Ikwiriri) – Rufiji. Wananchi wamelalamikia sana utarajibu wa utwaaji wa ardhi
husika uliotawaliwa na ubabe na vurugu( Sulle 2009 field visit: Kweka
2012). Mpaka mwaka 2006, kampuni ilifanikiwa kuendeleza hekta
500-600 tu. Kwa mujibu wa Uongozi wa Halmashauri ya kijiji, ardhi husika
amepewa mwekezaji mwingine anayetambulika kwa jina la Majani ya
Chai (Mwami & Kamata 2011), Kampuni haijasajiliwa Brela.
31. Shanta Estate Ltd. (Mkenya na Mhindi) Hawa wa jumla ya hekta
14,500 huko Bagamoyo kwa ajili ya Kilimo cha Jatropha
Eneo hili limetolewa kwa makubaliano baina ya mwekezaji na
wanavijiji wa Kibindu,Mkange na Miyono, (Mwamila et.al). TIC haina
taarifa kususiana na huyu mwekezaji (Locher 2010). Sehemu ya eneo ambalo
mwekezaji huyu analimiliki hekta 2000 , mwekezaji mwingine Eco
Energy naye anadai analimiliki kutokana na makubaliano waliyoingia na
wizara ya Ardhi (Sulle 2012).
32.Sun BioFuels ( huyu alibadilisha jina na sasa
inaitwa 30 Degree East). Shamba lipo Kisarawe
kwa kilimo cha Jatropha.
33.SyEnergy – hekta 30,000 za
ardhi ya kijiji kwa ajili ya kilimo cha mpunga – Kilombero (sulle 2012 interview
with District land Officer).
34. The New Forest company (NFC)(Uingereza na Afrika ya Kusini).
Hawa wana hekta 6,000 za ardhi huko Kilolo -
Iringa kwa ajili ya upandaji miti kwa ajili ya mbao kupunguza
hewa ukaa (Chachage & Baha 2010) . Mchakato huu ulivihusisha vjiji 11, hata
hivyo mchakato wa kuhamisha ardhi kwa mwekezaji ulifanikiwa katika vijiji sita
( hekta 4800, mchakato ulifanyika 2009 ukihusisha vijiji vya Isele,
Ukwega,Ipalamwa na Magome na hekta 1,175 ukihusisha vijiji
vya Kisang’a na Iselemwaka mwaka 2010 (Locher 2011). Mwekezaji anaendelea
kupora ardhi ya wananchi, hali iliyopelekea kuibuka kwa mgogoro mkubwa
katika kijiji cha Kidabaga na Kilawamo ambacho kinapinga
ardhi yao kuchukuliwa kimabavu pasipo wananchi kushirikishwa wala kutoa
ruksa!. Wananchi wamelazimishwa kutia sahihi nyaraka za fidia kuonyesha kwamba
wamehalalisha uporaji huo! Mwekezaji huyu anaendelea kuhodhi ardhi kwa kununua
rdhi kutoka kwa mwananchi mmoja mmoja katika vijiji husika(Locher 2010/2011).
35. TPC Ltd (CUEL Agro – Industry, Mauritius & Group
Quartier –France), - Kampuni hii inahodhi hekta
15,000 za ardhi ya vijiji huko Moshi vijijini kwa ajili ya kilimo cha miwa
(uzalishaji wa sukari).Hata hivyo ni hekta 7,700 tu zilizolimwa.
36.Vita Grain Ltd/GK Farm Ltd (RUBADA
2012- Sulle 2012 ) Kampuni hizi zina hati ya Makubaliano (Memorandum Of
Understanding) na RUBADA na mchakato ulikuwa katika hatua za
mwisho, mwaka 2012 (RUBADA 2012).
IX. MASHAMBA AMBAYO TAARIFA ZA WAWEKEZAJI HAZIKO
WAZI/HAZIELEWEKI
1.CHAWAGWA – hekta 200 za ardhi ya
Kijiji[18],
lipo Kisarawe. Lilikuwa ni kwa ajili ya kilimo cha Jatropha lakini
halijaendelezwa
2 . Euro Mine Export Ltd – Kampuni hii ina shamba Mikese- Morogoro kwa ajili ya kilimo cha
Jatropha. Hali ya sasa ya kampuni haijulikani (Sulle 2012)
3. Oxman Tanzania Ltd – Shamba lipo
Rufiji, ni kwa ajili ya Kilimo cha Mpunga. Halijaendelezwa[19]
4. RUBANA - Shamba lipo
Mwanza, ni kwa ajili ya kilimco cha Jatropha, ila halijulikani kwa
maafisa kilimo wa ardhi wa Wilaya[20]
5.SYNERGY Tanzania Ltd - Kampuni hii
ina shamba la hekta 20,000 huko Rufiji kwa ajili ya kilimo cha Mpunga [21]
6. Tanzania Biodiesel Plant – hekta 16,000 za
shamb, lipo Bagamoyo, ( Halmashauri ya wilaya
iliidhinisha mwaka 2008[22]
Mpaka Novemba 2012 Rais bado alikuwa hajaibadilisha toka ardhi ya kijiji
(village lands) kwenda general lands[23].
X. BAADHI YA MAKAMPUNI AMBAYO YAMETELEKEZA MASHAMBA/YAMEACHA
KUFANYA KAZI
1. African Green Oils Ltd Kampuni
hii imetelekeza
hekta 5,000ha huko Rufiji. Kwa sasa kampuni haifanyi kazi
2.Bio diesel East Africa Ltd - Bahi, hekta 10000ha zimetelekezwa.
3. Bio Massive – hekta 7500 zimetelekezwa
huko Lindi Vijijini. Kampuni ilisitisha shughuli zake kutokana na
mtikisiko wa kiuchumi na mgomo wa wanakijiji kutoa ardhi yao kwa
mwekezaji.
4.Boleyn International (T) Ltd. Ilisajiliwa na Brela 2012 ila haifanyi kazi kwa sasa.
5.CAMS AGRI-Energy Tanzania - Rufiji
6. Clean Power Tanzania - Bagamoyo
7.Donester - Bagamoyo
8.J &J group - Tabora
Kaliua
9.JCJ Co. Ltd- Mwanza,
Mara, Shinyanga ,Tabora
10.Kitomondo Ltd - Bagamoyo
(Shamba la Makurange)
11.Safe Production Ltd - Rufiji.
12.Savannah Biofuels Ltd - Handeni
13.Savannah Biofuels Ltd. - Kongwa
14.Sekab Bioenergy Tanzania - Rufiji
15.Tanga Forest(s) - Handeni
16. Tanga Forest(s) - Mkinga
17.Tanga Forest(s) - Pangani
XI. NTELIGENSIA MBOVU YA KIUCHUMI
Mheshimiwa Spika, kama
ilivyojidhihirisha hapo juu wanaojiita au kutambulishwa kama wawekezaji,
ambao wametawaliwa la lugha tamu ,zilizojaa hadaa na matumaini makubwa, wengi
wao hawana mitaji au wamefilisika huko waliko toka,wakitarajia
kutumia mtaji wa ardhi ya Tanzania kwenda kutafuta/kukopa fedha nje. Na mbaya
Zaidi , baadhi yao badala ya kutumia mikopo kwa manufaa ya kuendeleza kilimo,
wamekuwa na mtindo wa kuzihamishia fedha kwenye miradi yao mingine. Hali
iliyopelekea miradi mingi kushindwa kuanza wakati tayari miliki ya ardhi
imeshapokwa toka kwa wanakijiji.
Mheshimiwa Spika,
Kambi ya upinzani inaitaka serikali, kurejesha mashamba yote
ambayo hayajaendelezwa/yametelekezwa chini ya miliki ya vijiji vilivyoathirika
.
Mheshimiwa Spika, wakati taarifa
za kiuchunguzi naonyesha kwamba hakuna uwiano wa miliki za mashamba
makubwa kati ya wawekezaji wa nje na raia ya watanzania, ripoti ya hivi
karibuni ya Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC)
Raymond Mbilinyi wakati akitoa taarifa ya uwekezaji nchini, alisema kuwa
Tanzania ina hazina kubwa ya ardhi kwa shughuli za uwekezaji kwa
kuwa mpaka sasa ni wawekezaji 52 pekee ndio waliopewa hati ya kumiliki ardhi
nchini, akiwataka watanzania kuondokana na dhana kwamba ardhi yao
inaporwa! Alibainisha hayo alipozungumza katika kikao
cha kikundi kazi kilichojadili umuhimu wa kuwa na Bank ya ardhi nchini.
Alisisitiza kuwa kampuni za uwekezaji zinazokuja kuwekeza nchini
zinahitaji ardhi hivyo ni lazima Tanzania kuweka mazingira kulingana na
hali ilivyo na kwenda na wakati[28].
Mheshimiwa Spika, hawa ndio
watendaji wa serikali ambao kutokana na kuzoea kufanyia kazi makaratasi hawana
uelewa wa kile kinachoendelea DUNIANI! Ni rai ya Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni kwa TIC kabla haijaendelea na utaratibu wake wa kupiga mnada ardhi ya
Tanzania, wafanye tathmini ya uendelezaji wa ardhi ambayo mpaka sasa
wamewapa wawekezaji. Inakadiriwa kwamba zaidi ya hekta 640,000 zilitolewa
kwa kilimo cha mazao ya nishati pekee...ardhi ambayo ilipatikana kwa
kuhawilisha ardhi ya vijiji . Mengi ya mashmba hayo yameendelezwa kidogo
au hayajaendelezwa kabisa!
XII. SHERIA NO. 5 NA MUSTAKABALI WA TAIFA
Mheshimiwa Spika, katika hotuba yetu
ya Bajeti ya mwaka mwaka 2011/12, pamoja na mambo mengine tuliieleza Serikali
juu ya haja ya kuifanyia marekebisho sheria ya Sheria ya Ardhi ya Kijiji ambayo
inatoa mamlaka kwa Halmashauri ya kijiji kusimamia ardhi yote ya
kijiji, na imepewa mamlaka ya kugawa ardhi isiyozidi heka 50 baada ya
kuruhusiwa na Mkutano Mkuu wa Kijiji. Kambi ya upinzani ilitoa mapendekezo hayo
kutokana na uchunguzi wa kitaalam iliyoufanya na kugundua kwamba kutokana na
kutokuwa na ufahamu mpana wa sheria, watu wenye fedha wamekuwa wakitumia
fursa hii ya kisheria vibaya kwa kuwarubuni viongozi wa vijiji, na
hatimaye kugawa maeneo ya kijiji kwa watu wachache wenye fedha /ushawishi wa kisiasa,
huku ikiwaacha wanakijiji bila ardhi kinyume na matakwa ya kisheria.
Mheshimiwa Spika,hali inakuwa
mbaya zaidi pale ambapo watu ambao sio watanzania wanatumia upenyo huu wa
kisheria ,na kumilikishwa maeneo makubwa ya kijiji kinyemela! Hakuna
ubishi kwamba kuna wageni wengi waliopata maeneo ya vijiji kinyemela kwa
kutumia upenyo huo ,wakati sheria ya Ardhi No.4 , kifungu na 20 kinakataza
wageni kumiliki ardhi nchini isipokuwa kwa malengo ya uwekezaji tu, na ambao
umiliki wake lazima upitie Kituo cha uwekezaji Tanzania na si vinginevyo.
Mhesimiwa Spika,kama ilivyo
kawaida,maoni ya Kambi ya Upinzani yalipuuzwa...miaka mitatu baadae utafiti wa
chombo kilichopewa kazi na serikali kufanya tathmini ya ardhi nchini, pamoja na
watafiti wengine wamethibitisha kile ambacho Kambi ya Upinzani ilikisema, kwa
vielelezo zaidi ya miaka mitatu iliyopita!
Kambi Rasmi Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA
inaitaka serikali ilieleze Bunge hili tukufu...ni lini sheria hii
itafanyiwa mabadiliko? Aidha, ni lini serikali itawanyang’anya ardhi watu wote
(watanzania na wageni) ambao wamemilikishwa ardhi za vijiji kinyume na sheria
ya ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999?.
XIII. UKOMO WA ARDHI KWA WAWEKEZAJI WA KILIMO- MKANGANYIKO NA
KAULI ZA SERIKALI .
Mheshimiwa Spika, tarehe
28/11/2012 (Kufuatia hoja binafsi ya Ardhi Bungeni tarehe 8/11/2012)
Serikali ilitangaza ukomo wa ardhi kwa wawekezaji kwenye sekta ya kilimo
nchini, ambao utakuwa kati ya hekta 5,000 hadi 10,000 ili kutoa nafasi kwa
wawekezaji wengi na kuongeza ushindani katika sekta hiyo.
Serikali pia imeweka masharti kwa kila mwekezaji anayekuja
nchini, kulazimika kumsaidia mkulima mdogo katika uwekezaji, ili kumwinua
kiuchumi na kumfanya awe sehemu ya uwekezaji huo.
Mheshimiwa Spika, kauli hiyo ilitolewa
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kufungua mkutano maalumu wa wadau wenye ari ya kuwekeza katika sekta
ya kilimo kupitia Mpango wa Ukuzaji wa Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
Waziri Mkuu alisisitiza kwamba si busara kwa Serikali
kutoa eneo kubwa la zaidi ya hekta 60,000 au 100,000 kwa mwekezaji na badala
yake, uwepo ukomo wa ardhi.
“Moja ya mambo ambayo ni ya msingi ni hili la kupunguza ukubwa
wa eneo kwa mwekezaji, kwa mfano kama mwekezaji wa mpunga, tumeona hekta 5,000
ni nyingi kuzimaliza mapema, zinamtosha hivyo tunaanza na kiasi hicho,”
Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu
alisema uchunguzi wa Serikali umebaini kuwa wawekezaji wenye maeneo
makubwa hawajayafanyia kazi na hivyo kuwanyima nafasi wengine na kuongeza kuwa
kwa upande wa mashamba ya sukari, hekta 10,000 zinatosha kuanzia.
Mheshimiwa Spika, wakati Waziri
Mkuu akitoa taarifa juu ya ukomo wa ardhi kwa wawekezaji, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais , Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Stephen Wassira (Mb)
akiwasilisha katika Kamati ya Bunge Mapendekezo ya mpango wa
maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2013/14 (Ofisi ya rais Tume ya Mipango,
Machi 2013[29] alisema katika kuendeleza kilimo cha ‘miwa’
kwa mwaka 2012/13 , mashamba kwa ajili ya uwekezaji katika
mabonde ya Wami, Ruvu,Kagera,kilombero na Malagarasi kiasi cha Hekta
277,000 yametambuliwa na uhakiki wake unaendelea kwa ajili ya
kuwezesha uwekezaji . Wawekezaji walioonesha nia ni:- Kampuni ya Ecoenergy[30]
(Bonde la Ruvu- hekta 20,000); Agroforestry (Muhoro Rufiji-
hekta 20,000). Wawekezaji hawa wanatarajia kushirikiana na ‘wakulima
wadogo’ (rejea taarifa ya tathmini ya ardhi juu ya nafasi ya wazawa katika
kuhodhi ardhi). Aidha shamba la ukubwa wa hekta 50,000 katika eneo la
Mkulazi (Morogoro) limepatikana na utafiti wa maji unaendelea!
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni inaitaka serikali kupitia waziri wa ardhi
,ilieleze Bunge lako tukufu, utekelezaji wa kauli ya Waziri Mkuu juu ya ukomo
wa ukomo wa ardhi ya kilimo kwa wawekezaji unaanza lini? Mipango na kauli za
waziri Mkuu zina uhusiano na Mpango wa Taifa wa Taifa wa miaka mitano
kama ulivyowasilishwa na Mhe. Wassira au kila mtu ana jipangia mipango yake kwa
kadiri atakavyoona inafaa? Kauli ipi hasa ni msimamo wa serikali: Kauli ya
Waziri Mkuu au kauli ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu?
XIV. UPANGAJI WA MATUMIZI YA ARDHI
Mheshimiwa Spika, katika miaka ya
hivi karibuni tumeshuhudia migogoro ya ardhi isiyokwisha. Migogoro ikiwahusisha
wakulima na wafugani, vijiji na vijiji , wawekezaji na wananchi wenyeji n.k . Migogoro
hii mara nyingi inachangiwa na serikali ya CCM kutokuwa na mipango thabiti ya
matumizi bora ya ardhi.
Mheshimiwa Spika, miaka
52 baada ya uhuru, Wizara imeandaa mipango ya matumizi
ya ardhi ya vijiji takriban 1,300 tu (sawa na asilimia 11 ya vijiji vyote
nchini) kati ya vijiji 12,000. Hadi mwaka 2011 kwa upande wa mijini,
miji mikuu ya mkoa , yenye mipango ya uendelezaji (master plans) iliyo hai
ilikuwa 10 tu kati ya miji 25. Miji mikuu ya wilaya yenye mipango
ya matumizi ya ardhi ni 20 kati ya miji zaidi ya 110, na miji midogo
yenye mipango ni 25 tui kati ya miji 95 !Mwisho lakini nsio kwa
umuhimu....miaka 52 baada ya uhuru viwanja vilivyopimwa ni laki
tisa na tisini na tano elfu tu ( 995,000).
Mheshimiwa Spika, kwa kasi hii ,
hatutaweza kumaliza squatters, hatutaweza kumaliza migogoro
ya ardhi ambayo imekuwa donda ndugu katika Taifa hili...donda ambalo halina
dalili yoyote ya kupata tiba !!! Kwa kuonyesha ni kwa kiwango gani serikali
haina mpango kabisa wa kuhakikisha vijiji vinakuwa na mipango bora ya matumizi
ya ardhi ,sambamba na kuhakikisha kwamba kasi ya upimaji wa ardhi inaongezeka,
serikali imekuwa na mkono wa birika katika kutenga fedha mahsusi kwa
ajili ya upimaji wa viwanja hususan kuwezesha ujenzi wa kituo cha satelite
ambacho kingekuwa mhimili wa kupima viwanja haraka na kwa njia ya kisasa!
Mheshimiwa Spika, kwa miaka
miwili mfululizo (mwaka 2010/11 (bilioni 3), 2011/12 (bilioni 4)) Bunge lako
tukufu limekuwa likitenga fedha imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya
ujenzi wa kituo husika, lakini ama kwa dharau ama kwa kutokuona umuhimu
wizara ya fedha (hazina) wamekuwa wagumu kutoa fedha....na kwa taarifa
iliyonayo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mwaka huu hakuna fedha
iliyotengwa kwa ajili ya kupima viwanja !
Mheshimiwa Spika,taarifa za
kitaalam zinaonyesha kwamba kama wizara wangepewa shilingi bilioni 12 tu,
wangeweza kupima viwanja visivyopungua milioni 5. Ni
rai yangu kwa wabunge, tunaokabiliwa na changamoto ya migogoro ya ardhi
inayotishia amani na ustawi wa nchi yetu,tuungane kwa pamoja kuhakikisha kwamba
kwa mwaka huu wa fedha zinapatikana fedha kwa ajili ya maandalizi ujenzi wa
kituo cha satelite, na fedha kwa ajili ya upimaji viwanja.
XV. VIONGOZI WA CCM NA UJAMBAZI WA ARDHI
Mheshimiwa Spika, dhuluma hii
inalihusisha shamba namba 24 Lorkisalie ( OLDUPAI SEED CO. LTD) ,lililopo
Wilayani Simanjiro, Jimbo la Simanjiro , Kitongoji cha Lemooti, Kijiji
cha Loiborsoit A. Kwa mujibu wa barua ya ofisi ya Msajili wa
Hati Kanda ya Kaskazini- Moshi ya tarehe 1/3/2010 yenye
kumbukumbu namba LR/MS/T/1127 4/15 inaonyesha kwamba shamba husika
lilisajiliwa tarehe 28/11/1994 na kupewa hati namba 11274.
Mheshimiwa Spika, mhusika mkuu
katika mgogoro huu ni bwana Brown Mathew Oleseya, Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Simanjiro, ambaye amejimilikisha kiujanja-ujanja hekta za
kijiji 3,425 ambazo ni sawa na ekari 8,562.5. Licha ya kujipatia eneo
husika kimizengwe, Mheshimiwa huyu wa Chama Tawala amefungia
wananchi njia zote za chemchem za maji na malisho ya mifugo.
Mheshimiwa Spika, barua yake ya
maombi ya shamba ya tarehe 14/4/1978 , yenye kumb Na:PF/MI/40
inaonyesha kwamba aliomba eneo tofauti na analolitumia
kwa sasa. Barua inaonyesha aliomba eneo la LESHUTA, ambayo ipo katika kijiji
cha Engonongoi Kata ya Terat na Shamba ’analolimiliki’ kwa
sasa lipo eneo la LEMOOTI kijiji cha Loiborsait A.
Mheshimiwa Spika, muhtasari wa
kikao cha kamati ya maendeleo ya Kata kilichoketi tarehe 26/4/1978.
kilichohudhuriwa na wajumbe 19 kinachosemekana kilimpatia Mwenyekiti huyu wa
CCM Ardhi (ekari 5000, ekari 2000 za kulima na 3000 kwa ajili ya mifugo ),
haujaidhinishwa na mamlaka yoyote na hakuna muhuri wala
sahihi ya Mwenyekiti , Katibu wala wajumbe. Barua pekee yenye
sahihi, bila muhuri wowote ni ya Katibu Kata ya tarehe 26/4/1978 ikimtaarifu
kwamba amepewa shamba husika.
Mheshimiwa Spika, Kamati ya
Ushauri wa ardhi ya Wilaya ya Kiteto Ilioketi tarehe 16 Januari
1979 iliyohudhuriwa pia na na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya kipindi hicho , Ndugu
Ole Kone na katibu wa CCM (W) ,ndugu P.Bura , pamoja na mambo mengine
walijadili maombi ya mashamba , yaliyopitishwa na ngazi ya Kata pamoja na
shamba la Bwana Brown Mathew Ole Suya. Kikao husika kiliamua
kwamba katika ekari 5000 zilizoombwa , eka 2000 za kilimo atazitumia kwa
miaka 5 kisha zirejeshwe kijijini, na ekari 3,000 apewe lease ya miaka 33.
Lakini asiingilie Hifadhi , sehemu ya jeshi na wilaya ya Monduli. Kama
ilivyo nyaraka zilizotangulia Muhtasari wa kikao husika,hakikuwa na sahihi ya
Mwenyekiti wala Katibu!
Mheshimiwa Spika, licha ya
kwamba nyaraka husika (anazozitumia kiongozi huyu kama ushahidi wa kupewa
shamba) hazina uhalali wowote kisheria , kwa mujibu wa makabidhiano ya ardhi
husika,kama ilivyoamauliwa na kamati ya ardhi ya Wilaya, Bwana Brown
alitakiwa arejeshe ardhi ya kijiji( ekari 2000 za kilimo) mwaka 1985, na
ardhi ya mifugo (ekari 3000 kwa ajili ya malisho ) mwaka 2011! Mwaka
1985, shamba la kijiji halikurudishwa (ekari 2000), mwaka 1991 kada huyu
aliendelea kupora ardhi ya kijiji kwa kuongeza ukubwa wa eneo lake
kutoka! Hekta 2000 za awali mpaka hekta 3,425 (Ekari 8,000)!, ambayo ni hekta
1425 zaidi ya kiasi ’alichopewa’. Eneo hilo jipya liliingia kwenye kijiji
cha Lolksale wilaya ya Monduli !
Mheshimiwa Spika, kada huyu wa CCM, licha ya kutokuwa mmiliki
halali wa eneo husika ,tarehe 31/8/ 2009 kwa
kushirikiana na watumishi wa serikali wasio waaminifu walibadilisha
matumizi ya shamba kutoka kilimo na ufugaji na kuwa Hifadhi
ya kitalii.
Uhalali wa Kubadilisha Matumizi ya Ardhi na Mwenye Mamlaka ya
Kubadilisha Matumizi
Mheshimiwa Spika, Kanuni na
na taratibu za kubadilisha matumizi hazikufuatwa:
i) Bango kwa lengo la kukusanya
maoni ya wananchi majirani kuhusu nia ya mmiliki kutaka kuongeza
matumizi kama inavyotakiwa kwenye waraka wa kitaalam Na.1 wa
mwaka 2006
ii) Kibali cha Mkurugenzi wa mipango Miji na
vijiji kama inavyotakiwa kwenye Sheria ya Mipango miji
Na.8 ya mwaka 2007 kifungu 32(1) na 6(3)
iii) Kibali cha nyongeza ya matumizi katika Miliki (
Land Form na. 28) kimetolewa na kusainiwa Paulo E .Kibona ambaye
hana mamlaka kisheria kusaini Fomu hiyo. Fomu hiyo husainiwa na Kamishna
wa ardhi kwa mujibu wa sheria ya ardhi na.4 ,1999 kifungu 35(4)
Nyaraka ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani inazo zinaonyesha
kwamba Wizara ya Ardhi, kupitia kwa Kamishna Msaidizi Kanda ya Kaskazini
kwa barua yenye kumbukumbu Na. LD /NZ/6014/22/DW ya tarehe 22/09/2010
ilimtaka arejeshe hati iliyoofanyiwa mabadiliko ya matumizi....lakini alipuuza
amri ya mamlaka halali! Hali iliyoilazimu Kamishna msaidizi kuandaa
hati ya marekebisho ya mabadiliko ya matumizi (deed of rectification) na
kuiwasilisha kwa Msajili wa hati msaidizi kanda ya Moshi ili
afanye marekebisho kwenye daftari lake . Marekebisho yalifanyika
tarehe 26/01/2011 na kusajiliwa kwenye FD. No. 29828 ambapo
matumizi kwenye hati yalitakiwa yabaki yale ya awali (japokuwa hakuwa na
uhalali wowote wa umiliki)
Mheshimiwa Spika, licha ya kuwa
na uelewa wa mgogoro husika bado Kada huyu wa CCM aliuza eneo
husika (ardhi ya kijiji) kwa raia wa kigeni , mmiliki wa Kampuni
Maasai steppe Conservancy limited mnamo tarehe 14/12/2010.
Kwa mujibu wa Taarifa za BRELLA , kampuni ya Maasai Steppe
Conservancy limited ina jumla ya hisa 10,000, kama
ilivyoainishwa hapa chini:
i)
BCZV Holdings limited ni kampuni inayomilikiwa na Baastian
bruins 9Mdachi) na Jerome Bruins (Mdachi) wana hisa 9700
ii)
John warren (Mwingereza ) ana hisa 100
iii)
Brown Mathew Ole suya ( Mtanzania) ana hisa 200.
Kutokana na hisa nyingi ( 9800) za kampuni ya Maasai Steppe
Conservancy kumilikiwa na wageni ni dhahiri kwamba kampuni
hiyo ni ya kigeni.
Kwa mujibu wa sheria ya ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, fungu
la 20 : Kampuni /raia wa kigeni kabla ya kumiliki ardhi wanatakiwa
wapate kibali ( Cerificate of incentives) kutoka TIC. Utaratibu huu
haukufuatwa! Wakati nchi inakabiliwa na changamoto kubwa ya ardhi kumilikiwa na
wageni! Kada/kiongozi wa chama cha mapinduzi amegeuka kuwadi namba moja
wa kuuza nchi kwa wageni! Waziri wa ardhi ana taarifa zote kuhusiana na
uvunjwaji huu wa sharia kuanzia na uporaji wa wa eneo la kijiji, kubadilishwa
kwa matumizi ya ardhi pasipo kufuata sharia na taratibu na kuuza ardhi kwa raia
wa kigeni kinyume na sharia za nchi! Waziri aliahiidi kwenda
kulishughulikia toka mwaka 2011 mpaka sasa hajatia mguu.
Kambi ya upinzani inataka kupata majibu ya maswali yafuatayo:
I)
Wizara ya ardhi ilitumia vigezo gani kumpatia hati?
II)
Wizara ilitoaje uhalali wa kubadilisha matumizi ya ardhi
III)
Wizara imeafiki vipi wa umiliki wa ardhi kwa raia wa kigeni
(Mdachi)
IV)
Hatua gani zitachukuliwa kwa kada huyu wa CCM kwa kukiibia kijiji
na watanzania ardhi yao na kwa kuvunja sheria?
XVI. UVAMIZI WA MAENEO YA WAZI MKOA WA DAR ES SALAAM
Mheshimiwa Spika, Rais,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifanya
majumuisho ya ukaguzi wa hali ya maji katika mkoa wa Dar es salaam
tarehe 24 Mei, 2010 alitoa hoja ya kuvamiwa kwa maeneo mengi ya
wazi katika Mkoa wa Dar es salaam,ambapo alilalamikia baadhi ya Madiwani
kuhusika na uvamizi huo.
Halikadhalika aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.
William Lukuvi, alipotembelea Manispaa ya Kinondoni tarehe 15 Juni
2010 alibaini mapungufu husika hali iliyopelekea kuunda
kamati maalum ya kuchunguza maeneo yote ya wazi
yaliyovamiwa katika Mkoa wa Dar es salaam. Kamati ambayo iliundwa
tarehe 18 Juni, 2010 lengo la kazi likiwa ni kuchunguza
maeneo ya wazi yaliyomo katika Jiji la Dar es salaam, ambayo
yamevamiwa, kuendelezwa au kuuzwa kinyume na taratibu za mipango
miji. Kamati ambayo ilikamilisha kazi yake tarehe 13/7/2010 (taarifa ya
Kamati husika,pamoja na mapendekezo tunayo).
Mheshimiwa Spika,Kambi ya
upinzani inaitaka serikali itueleze, baada ya miaka 4 kupita tokea Kamati
husika imalize kazi yake;
1) Ni hatua gani
zimeshachukuliwa ili kuyarudisha maeneo husika?
2) Ni maeneo mangapi kati ya
yaliyobainishwa yamesharudishwa?
3) Ni Hatua gani
zimechukuliwa dhidi ya maafisa waliohusika na ubadhirifu huu na kwa kiwango
gani?
4) Ni lini serikali
inatarajia kukamilisha utekelezaji wa mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati
husika?
5) Je serikali itakuwa tayari
kuvunja majumba makubwa makubwa ya watu wenye fedha waliouziwa maeneo ya wazi
kinyume na utaratibu na kupewa hati na maafisa wasio waaminifu ?
6) Serikali inatoa tamko
gani juu ya Kiwanja namba 856 Msasani beach, ambacho kwa
mujibu wa Ramani ya upimaji iliyosajiliwa namba 29331 ilikuwa
ni kwa matumzi ya wazi, lakini baadae kilimilikishwa kwa mtu binafsi.
Matokeo yake njia ya mkondo wa maji kuelekea baharini imezibwa,na mvua
ikinyesha maeneo ya kwa Warioba, mpaka njia panda ya kuelekea Clouds FM
yanajaa maji.
7) Mheshimiwa Spika, Kambi
Rasmi ya Upinzani inaitaka serikali itoe maelezo kuhusiana na
viwanja namba 9 & 10 Kitalu ’S’ Tabata Segerea. Mgogoro huu ni wa muda
mrefu sana, Waziri wa Ardhi anayo taarifa. Barua ya mwisho kwa waziri
iliandikwa tarehe 2/5/2013 ,ilikuwa na viambatanisho kumi. Viwanja husika
vilivyotengwa mahsusi kwa matumizi ya Umma (soko). Tume ya Ardhi iliyoundwa
tarehe 23/9/2008 kuchunguza mgogoro husika ilibaini kwamba viwanja husika
vilimilikishwa kimakosa kwa Walter Camilius na Rose Samwel
Binagi.
8) Kambi Rasmi ya Upinzani
bungeni, inataka Serikali itoe maelezo juu eneo la wazi la Kitalu D, Registered
Plan namba 8750, mtaa wa Mikumi na Makongoro,
Magomeni , lango la JIJI , ambalo licha wa maelekezo na kauli mbali mbali za
serikali,bado linaendelea kuendelezwa!
XVII. SHIRIKA
LA NYUMBA LA TAIFA
SERIKALI
NA TAASISI ZAKE KUTOLIPA KODI ZA PANGO KWA WAKATI
Mheshimiwa Spika, ’Katika kipindi
cha Julai 2011 shirika lilikusanya kodi za pango
pamoja na malimbikizo kiasi cha shilingi bilioni 31.Pamoja
na na jitihada za kukusanya kodi na malimbikizo na hasa yale
yanayodaiwa serikali na taasisi zake, malimbikizo bado ni makubwa . Hadi
machi 2011, Serikali na taasisi zake ilikuwa
ikidaiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.543, baada
ya kupunguza malimbikizo kwa kiasi cha shilingi milioni
115 ,sawa na asilimia 8 tu!’ hii ilikuwa hotuba yetu ya mwaka
2011...miaka mitatu baadae taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya wizara katika
mwaka 2012/13 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2013/14 kwa kamati
ya kudumu ya Bunge ardhi , maliasili na mazingira inaonyesha kwamba
madeni[32]
ya serikali na taasisi zake yaliongezeka kutoka shilingi bilioni 2.8
mwaka 2011/12 mpaka bilioni 3.4 mwezi Februari 2013!
Kambi ya upinzani inataka serikali ieleze ni kwa
nini imekuwa ni mdaiwa sugu , na kwa nini hailipi madeni ya shirika la
nyumba?
XVIII. MIKOPO YA UNUNUZI NA UJENZI WA NYUMBA
Mheshimiwa Spika,Pamoja na
kuwepo kwa sheria ya Mikopo ya nyumba (Mortgage Financing Act) ya
mwaka 2008 na sheria ya umiliki wa sehemu ya majengo ( Unit
Titles Act) ya mwaka 2008, masharti ya mikopo hii bado ni magumu.
Mfano, kwa sasa benki zanazotoa mikopo ya nyumba masharti
yake ni pamoja na muda wa marejesho ya kati ya miaka 6
mpaka 15 na riba kati ya asilimia 17 mpaka 22 kwa mwaka .
Mheshimiwa Spika, Iwapo
hali hii haitabadilika , itakuwa vigumu kwa wananchi , halikadhalika
shirika letu la nyumba kujenga nyumba za gharama nafuu
na kwa wananchi walio wengi kuweza kumudu mikopo ya ununuzi
wa nyumba.
XIX. SERIKALI KUVUNJA AHADI YA KUWAUZIA NYUMBA (KWA BEI NAFUU)
WAPANAGAJI WA SHIRIKA LA NYUMBA KINYEMELA.
Mheshimiwa Spika, Serikali, tangu
mwaka 1996, ilpitisha maamuzi ya kuliruhusu Shirika la Nyumba kuwauzia
wapangaji wake nyumba za gharama ndogo na gharama ya kati zilizojengwa na
Shrika lenyewe. Hata hivyo, nyumba zilizotaifishwa hazihusiki na uamuzi huu.
Mheshimiwa Spika, Mwaka 2008,
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Ziarani Manispaa ya Iringa kuzindua
majengo ya SNT/NHC (Agosti, 07 2008) alikazia uamuzi wa Serikali kwa
kusema ”Sheria ya Mikopo ya Nyumba inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni
Oktoba mwaka huu, ambapo ikipitishwa, itawezesha Watanzania wanaoishi kwenye
nyumba za Shirika la Taifa, kununua nyumba hizo” Rais aliongeza kuwa ”MTU
HAWEZI KUISHI NDANI YA NYUMBA ZA NHC KWA MIAKA 30 BILA KUFAIDIKA”.
Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko
makubwa, Sheria ilitungwa lakini Serikali imeamua kubadili mwelekeo kimyakimya.
Serikali imesema kwamba jukumu la msingi la Shirika la Nyumba litakuwa ni
kufanya bishara ya kujenga na kuuza nyumba badala ya jukumu la sasa la
kupangisha nyumba na kukusanya kodi kwa mwezi. Hata hivyo, bei ya nyumba
inazingatia bei ya soko la sasa hivi ambapo gharama ni kubwa sana na kihalisia
hakuna mtanzania masikini anayeweza kununua nyumba hizo.
Kwa mfano: UNUNUZI WA NYUMBA UBUNGO KN 242/1-242/12
BEI YA UNUNUZI BILA
VAT
TSHS 67,946,567.86
VAT
18%
TSHS 12, 230,382.21
BEI YA UNUNUZI PAMOJA NA VAT TSHS.
80,176,950.07
RIBA YA BENKI
18%
TSHS. 144,318,510.234
MUDA WA KULIPA NI MIAKA 15
TSHS 800,000 KWA MWEZI XMIAKA 15 = 144,000,0000
MAJI TAKA 3000X48 DEPARTMENT BLOC 1 =TSHS. 144,000
BLOCK 9X
144,000
BLOCK 9= MWEZI TSHS. 1,296,000
KWA MWAKA TSHS. 15,552,000
PARKING – HAKUNA
VIWANJA VYA MICHEZO – HAKUNA
Mheshimiwa Spika, kwa hali hiyo,
ni mtanzania gani ataweza kununua nyumba ya Shirika la Nyumba la Taifa? Hakika
huu ni ubaguzi mkubwa kwa kuwa sasa hivi wenye uwezo ambao wengi ni wageni
(wahindi, wachina na wazungu) ndio wameanza kujaa katika nyumba hizo. Haki ya
Mtanzania iko wapi?
Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya
Upinzani inaitaka Serikali kutoa kauli mbele ya bunge hili leo hii kama bado
ina mpango wa kuwauzia nyummba za bei nafuu wapangaji wa shirika la nyumba la
taifa. Aidha, Kambi ya upinzani , inaitaka Serikali itueleze ni
kwa namna gani imejipanga kuweza kutatua tatizo hili ! Lazima
Serikali iweke Mazingira ya kuziwezesha Benki kutoa mikopo
yenye masharti nafuu kwa wawekezaji na wanunuzi wa nyumba.!!!!
XX. KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT) NA ONGEZEKO LA
MTAJI (CAPITAL GAIN TAX) KWENYE MAUZO YA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA
SHIRIKA
Mheshimiwa Spika, Shirika la
Nyumba la Taifa, lilipoanzishwa mwaka 1962 , moja kati malengo yake
ilikuwa ni kujenga nyumba nafuu kwa ajili ya watanzania wafanyao
kazi mijini . Hata hivyo kwa kadiri siku zilivyosonga mbele,
Shirika hili liligeuka kutoka kuwahudumia masikini na watu wenye kipato cha
kati na badala yake kuwahudumia watu wa kipato cha juu.
Mheshimiwa Spika, kodi
ambazo Shirika hulipa pale linapouza nyumba: Uwepo wa kodi
hizi huzifanya nyumba zinazojengwa na shirika kuwa ghali na hivyo
zisiweze kushindana kwenye soko na kuwa mzigo mkubwa sana kwa wananchi
wanaotaka kununua nyumba . Mfano dhahiri, kwa mwaka wa fedha
2010/11 shirika lilitarajia kujenga nyumba 49 , zenye jumla
ya thamani ya shilingi bilioni 4.08. Kwa gharama
iliyotumika, wastani wa nyumba moja ililigharimu shirika shilingi milioni
83.4,
Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa
Taarifa ya utekelezaji wa Kazi za Shirika la Nyumba la Taifa kuanzia
Julai 2010 hadi Mei 2011 wanatarajia kupata shilingi bilioni
6.3 kutokana na mauzo ya nyumba hizo , yaani faida ya
shilingi bilioni 1.9 Kwa tafsiri nyingine nyumba moja
itauzwa na shirika la nyumba kwa shilingi milioni 129.2, wakati gharama
halisi za ujenzi ni shilingi milioni 83. Kwa kila nyumba
iliyounzwa shirika limepata faida ya shilingi milioni 46.
Mheshimiwa Spika, Kwa hali hii,
inawezekana kweli Shirika hili kujenga nyumba kwa ajili ya wananchi wa
kawaida ,kuweza kumudu? Kama kweli tatizo ni kodi la ongezeko la
thamani na kodi ya ongezeko la mtaji, serikali haioni kwamba ina
wajibu wa kuondoa hizi kero ili shirika lifanye kazi kwa maslahi ya wengi, na
sio kwa maslahi ya wachache?
XXI. KODI KWA VIFAA VYA UJENZI
Mheshiwa Spika,gharama
za vifaa vya ujenzi imekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wengi,
tumekuwa tukilizungumzia hili kwa kipindi kirefu sasa na serikali imekuwa
ikiahidi kulitafutia ufumbuzi ili kuwapungumzia raia wake mzigo katika
ujenzi wa nyumba..ili hatimaye makazi na nyumba za wananchi wetu
ziakisi maendeleo na mafanikio yanayotokea nchini na
kuondokana kabisa na nyumba za matope, fito na nyasi ifikapo 2020.
Mheshimiwa Spika ,Kambi ya
upinzani inaitaka serikali ilieleze Bunge lako tukufu ni lini kodi katika
vifaa vya ujenzi wa nyumba kama saruji, mabati, nondo nk. itaondolewa ili
kuweza kufanikisha dhamira hii?
XXII. KODI ZA PANGO
Mheshimiwa Spika, eneo lingine
ambalo ni kero ,ni kodi za nyumba. Kila mwenye nyumba katika nchi hii
amekuwa akijipangia kodi , kwa kadiri atakavyoona inafaa. Ni kwa bahati mbaya
sana wamiliki wa nyumba licha ya kupata mapato (ya kibiashara),hawalipi
kodi serikalini. Kambi ya upinzani imelizungumza hili kwa kipindi kirefu sana,
hivyo tunaitaka Serikali ianzishe Taasisi itakayosimamia na kudhibiti kodi za
pango la nyumba ambazo hivi sasa ni kubwa mno! zinatozwa kwa mwaka mzima,
hivyo kuwatesa wapangaji husan wa kipato cha chini.
XXIII. UENDELEZAJI MAJENGO MIJINI
Mheshimiwa spika, yamekuwepo
matukio ya kujirudia ya kuanguka kwa majengo ya maghorofa
yaliyokamilika na yanayoendelea kujengwa katika jiji la Dar es
salaam, na tukio la hivi karibuni jengo lililokuwa linaendelea
kujengwa katikati ya jiji la Dar es salaam, mtaa wa Indira
Ghandi,kiwanja namba 2032/73 na kupoteza maisha ya watanzania wasiopungua
36. Kambi ya upinzani inasikitishwa kwa tukio hilo ambalo lingeweza
kuzuilika iwapo mkandarasi angezikatia kanuni za usalama,
halikadhalika kama mamlaka zenye jukumu ya kusimamia sekta hii ya ujenzi
zingetekeleza wajibu wao ipasavyo!
Mheshimiwa Spika, kama ilivyo
kawaida yetu , pale ambapo panatokea tatizo watu wenye dhamana ya kutafuta
mbinu za kutatua matatizo wamekuwa ni mabingwa ya kujificha kwenye vivuli vyao!
Mheshimiwa spika, hakuna ubisihi
kwamba Waziri pekee aliyeonekana japo kuguswa kilichotokea na hata kutoa
maelekezo ya kiutendaji kwa mamlaka za chini kwa utekelezaji ni waziri wa
ArdhiM(japokuwa mpaka sasa kauli yake haijafanyiwa kazi) mawaziri wengine
walidiriki, kukana mbele ya Bunge lako tukufu ( akiwemo waziri wa Ujenzi,
Mhe.John Pombe Magufuli wakati akijibu hoja za wabunge ,wakati wa wa
mawasilisho ya Bajeti ya wizara ya Ujenzi na wengine walikuja kuchungulia
kwenye kamati ya ardhi na maliasili,walipopewa maelekezo ya nini wanatakiwa
walete kwenye kamati,waliingia mitini – Mhe Aggrey Mwanri, naibu waziri
TAMISEMI) huku kiti cha Spika kikiwalinda kwamba hawahusiki kwa
namna yoyote,na hoja zote za wabunge zikatupiwa kapuni!
Mheshimiwa Spika, ni muhimu Bunge
lako tukufu likaelewa kwamba kuna mamlaka zaidi ya moja katika suala zima la uendelezaji
wa majengo mjini. Ni muhimu mamlaka zote hizi zielewe wajibu wake,na ziwajibike
ipasavyo kwa mema na mabaya!Katika sakata hili,wizara zifuatazo haziwezi
kukwepa uwajibikaji:
1) Wizara ya Ardhi
2) Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
3) Wizara ya Ujenzi na
4) Wiza ya Kazi na Ajira
Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa
sheria ya mipango miji , No.8 ya mwaka 2007,Wizara ya ardhi , Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ina jukumu la kusimamia upangaji na uendelezaji
wa maeneo ya mjini(Kisera).
Mheshimiwa Spika, Mamlaka
zinazohusika na kutekeleza sheria ya Mipango Miji , namba 8 ya mwaka 2007
ni Halmashauri za Jiji, Miji na Wilaya pamoja na kampuni au taasisi
yeyote itakayopewa hadhi ya kuwa mpangaji . Sheria ya serikali za mitaa( Local
government Act number 3 of 1982)inazipa mamlaka halmashauri zote
nchini kuandaa mipango ya uendelezaji maeneo yaliyomo kwenye eneo
lililotangazwa kuwa la upangaji kisheria (kulingana na sheria ya mipango
miji namba 8 ya 2007).
Mheshimiwa spika, kimsingi usimamizi
wa uendelezaji wa majengo mijini uapaswa kusimamiwa chini ya wizara
ya Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI).Maeneo muhimu yanayosimamiwa
na Halmashauri ili kuhakikisha majengo yanayopjengwa yanakuwa katika ubora
stahiki ni pamoja na:
i)
kukagua ramani zinazowasilishwa kwao kutumia wataalam mbali mbali,
ii)
kutoa vibali kwa waombaji ambao ramani zao zimebuniwa na kampuni
zilizosajiliwa ,
iii)
kufanya ukaguzi wa majengo kwa kutumia timu ya wakaguzi wa majengo
ili kubaini kama majengo yanayojengwa kwa kufuata sheria,
iv)
Kukagua na kujiridhisha kama wajenzi wanaojenga ndani ya
Halmashauri wamesajiliwa na Bodi husika !
Mheshimiwa Spika, Wizara ya
Ujenzi inawajibIka kwa kupitia vyombo mbali mbali ambavyo viko chini yake,
ambavyo kisheria vinawajibuka katikasuala zima la usimamizi wa majengo: Bodi ya
wabunifu wa majengo na wakadiriaji Majenzi ni mamlaka iliyoanzishwa
na sheria Na. 16/1997 ( the Architects and Quality Surveyors
(Registration) Act { Cap. 269 R.E 2002) na mwaka 2010. Fungu la 4
la sheria hii linaweka majukumu kuwa ni pamoja na :
i)
Kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wabunifu majengo na
wakadiriaji majenzi , pamoja na kampuni zinazofanya kazi ya utaalam ushauri
katika kusimamia miradi ya ujenzi
ii)
Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa
madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikisha kama kazi ya ujenzi inayofanyika
inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na Bodi na anazingatia taratibu, kanuni na
sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini
iii)
Kuhakikisha kuwa maeneo yote ambako ujenzi unafanyika kumewekwa mabango yenye
kuonyesha jina na anwani ya mradi,jina la mmiliki ,wataalam wahsauri
kwa maana wabunifu majengo ,wakadiriaji majenzi ,wahandisi pamoja na
mkandarasi endapo atakuwa hakufanya hayo atachukuliwa hatu za kisheria
Mheshimiwa Spika,Chombo kingine
ambacho kiko chini ya wizara ya ujenzi ni Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).
Bodi hii ilianzishwa chini ya Fungu la 4 la sheria Na .15 ya mwaka
1997 (The Engineers registration Act [Cap . 63 R.E 2002]. Sheria
hii imeainisha wajibu na majukumu ya Bodi mbali mbali kama
ifuatavyo:
i)
Kufuatilia na kusimamia shughuli za utendaji kazi wa wahandisi ikiwa ni pamoja
na kampuni zinazofanya kazi ya utaalam ushauri wa usimamizi wa miradi ya
majenzi mijini,
ii)
Kuingia na Kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini
kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikisha kama kazi ya ujenzi inafanyika
/inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu,
kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi nchini,
iii)
Kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo ujenzi unafanyika kumewekwa mabango
yenye kuonyesha jina na anwani ya mradi ,jina la mmiliki ,wataalam
washauri kwa maana wabunifu majengo , wakadiriaji majenzi
,wahandisi pamoja na mkandarasi endapo atakuwa hajafanya
hivyo,atachukuliwa hatua za kisheria.
Mheshimiwa Spika, Chombo kingine ni bodi ya wakandarasi
(CRB) ,imeanzishwa na sheria Na. 17/ 1997 (The Contractors Registration
Act [ Cap. 234 R.E 2002.Fungu la 4 la sheria hii imekipa chombo hichi
majukumu yafuatayo:
i)
Kusimamia shughuli za utendaji kazi wa wakandarasi katika kujenga majengo
imara yenye kufuata viwango kwa mujibu wa michoro ya majengo hayo
ii)
Kuingia na kukagua shughuli zote za ujenzi unaofanyika hapa nchini kwa
madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikisha kama kazi ya ujenzi
inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anaingatia
taratibu ,kanuni na sheria zote zinazosimamia ujenzi mijini,
Wizara ya Kazi na ajira , inabeba dhamana kwa kupitia
chombo chake cha wakala wa afya na usalama kazini (OCCUPATIONAL,SAFETY
AND HEALTH AGENCY –OSHA). Chombo hiki kinasimamia usalama mahali pa kazi ,pia
kinashiriki kusimamia miradi ya ujenzi mijini. Mamlaka hii hutoa kibali na
kusajili mradi kama ambavyo mamlaka nyingine zinafanya kwa kutoa sticker.
Mheshimiwa Spika, Wizara zote
hizi zinawajibika kwa namna moja au nyingine kwa maisha ya watanzania 36
yaliyoteketea kutokana tu na uzembe! Ni TAMISEMI kupitia Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala iliyohusika moja kwa moja na kubadilisha kibali cha
awali cha ghorofa tisa ( 10 storeys) ilichokitoa 4/12/2007 na kutoa kibali kingine cha kuongeza sakafu saba ,kufikia ghorofa
16!Kinyume na matakwa ya Mpango wa Uendelezaji upya wa eneo la Kati la jiji la
Dar es salaam wa mwaka 2000. Mpango ambapo unaainisha kuwa
ujenzi kwenye viwanja vilivyoko eneo hilo uwe wa uwiano wa
jengo 2.0, ujazo wa kiwanja wa asilimia 60 hadi 70 na sakafu
kati ya 7 na 10 . Na kama kuna nyongeza yotote inayotaka kufanyika,
lazima kibali kitolewa na Wizara yenye dhamana, suala ambalo halikufanyika.
Halikadhalika wizara ya ujenzi na wizara ya kazi na ajira kwa vyombo vilivyo
chini ya wizara husika, kama ilivyoainishwa hapo juu vyenye mamlaka ya
kisheria ya usimamizi kushindwa kufanya hivyo!
Mheshimiwa Spika, licha ya
uthubutu ulioonyeshwa na waziri wa ardhi , kulishughulikia suala hili, Shirika
la nyumba la Taifa haliwezi kukwepa wajibu kama mbia. Mbali na kwamba
Sera ya Ubia ya NHC na Mkataba wa Ubia baina ya pande mbili(NHC na
M/S LADHA CONSTRUCTION LTD),inabainisha kwamba NHC itatoa Kiwanja na mbia
atagharamia mradi husika kwa 100%. Na kwamba Mbia ana wajibu wa kuteua
wakandarasi na washauriwa ujenzi na kulipia gharama zao zote, Ni ukweli
usiopingika kwamba baad ya jengo kukamilika, NHC angekuwa na umiliki wa
50% ya Jengo lote. Jengo ambalo ( kama yalivyo majengo mengine ya NHC) ni kwa
ajili ya makazi au biashara!
Mheshimiwa Spika, kwa namna
yeyote ile , shirika la nyumba lilikuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba
linafuatilia kwa ukaribu(kama ambavyo taasisi nyingine za serikali zinazoingia
ubia na zinavyofanya) ili kuwa na uhakika na usalama wa majengo kwa watumiaji!
Shirika lina wajibu wa kufuatilia kila hatua ya ujenzi. Ni muhimu
ikaeleweka kwamba miradi ya ubia ni mhimili muhimu sana wa shirika,
ikumbukwe kuwa hadi Februari ,2013 miradi na majengo 11 ilikamilika
na miradi ya majengo 19 iliendelea na mradi wa jengo 1 ulianza! Hii ni miradi
inayogharimu si tu mabilioni ya shilingi ,bali yanahusisha maelfu ya watanzania
ambao wanatarajia kuishi au kufanya biashara katika nyumba husika!
XXIV. KIWANJA NAMBA 1662 INDIRA GHANDI /ASIA
Mheshimiwa Spika,kufuatia
kuporomoka kwa jengo kiwanja namba 2032/75 tarehe 29/ March 2013
ilibainika kwamba jengo lililoko mkabala na eneo hilo lenye kiwanja na
1662/75 chenye mita za mraba 150 nalo limejengwa kwa viwango
visivyokidhi kanuni za upangaji miji kama zilivyoainishwa kwenye
Mpango wa Uendelezaji Upya eneo la Kati la jiji la Dar es salaam !
( Rejea Mpango unasemaje katika maelezo ya kiwanja 2032/75).
Mheshimiwa Spika, TAMISEMI-
kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, iliendelea na mtindo ule ule wa
kukiuka sheria baada ya kupokea maombi ya kibali cha ujenzi wa michoro ya
ghorofa kumi na nne (15 Storeys yenye sakafu ya wazi (Terrace) tarehe 21
Mei ,2009 kwa ajili ya biashara na makazi yaliyosajiliwa kwa plan
na. ILA /213/2009, maombi ammbayo yalipishwa na kamati ya vibali vya
ujenzi iliyoketi tarehe 20/07/2009 na kuthibitishwa kwenye kikao
cha tarehe 24/08/2009. Na kupewa kibali Na.0398 cha tarehe 12/08/2009.[34]
Mheshimiwa Spika,licha ya
Mamlaka husika kutakiwa kuvunja jengo husika ili kuepuka madhara mengine
kutokea, kwa barua ya 5/04/2013,kutoka kwa Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji
, Bibi albina Bura ...katika muktadha ule ule wa baadhi ya watendaji
kujificha katika vivuli vyao..mpaka leo jengo husika bado halijavunjwa. Taarifa
zilizopo ni kwamba imebidi wakazi wa eneo hilo kwa gharma zao watelekeze nyumba
zao na kutafuta makazi mapya,nyumba ya ibada iliyokuwa inahudumia waumini
imefungwa, kituo cha afya nk..
Mheshimiwa Spika, Kambi ya
upinzani inatambua juhudi kubwa inayofanywa na kamati ya Bunge ya ardhi na
mazingira katika kushughulikia hili suala, licha ya kutokupata ushirikiano
kutoka kwa baadhi ya mawaziri!Kambi ya upinzani haitarajii kwamba Mhe. Waziri
mkuu, ambaye,wizara ambayo iko chini yake inahusika moja kwa moja na akiwa
kama kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni ataruhusu uzembe huu
uendelee: Tunaitaka serikali ichukue hatua zifuatazo :
i)
Hatua stahiki za kinidhamu za kisheria zichukuliwe kwa
wahusika wa maafa haya
ii)
Itoe Bungeni Taarifa ya uchunguzi ya kuanguka kwa magorofa Dar es salaam
ya mwaka 2006 na hatua zilizochukuliwa na baada ya ukaguzi nyumba ngapi
zilitakiwa kuvunjwa .Taarifa tulizonazo ile taarifa iko kwenye makabati,imejaa
vumbi!
iii)
Bodi zote zilizotajwa hapo juu ziwajibike ipasavyo kila moja katika eneo
lake iliyotakiwa kuwajibika kisheria
iv)
Ukaguzi ufanyike kwenye majengo yote yaliyojengwa na Ladha Construction LTD,
taarifa ambazo kambi ya upinzani inazo mbia amekuwa na mahusiano ya kikazi ya
muda mrefu na NHC na kuna nyumba alizozijenga ambazo kuna wapangaji ndani yake
v)
Takukuru ichunguze mchakato mzima wa utoaji wa vibali uliotawaliwa na ukiukwaji
wa sheria ili kujiridhisha kama hakukuna na harufu ya rushwa katika mchakato
mzima. Kamati zilizohusika na utoaji vibali zinahusika hapa.
vi)
Sheria ziangaliwe upya na ikiwezekana tuwe na chombo mamlaka mahsusi ya
ukaguzi (Inspection Authority ) inayosimamia majengo hususan
maghotofa ambayo itakuwa na wataalam wa fani zote kwa miji na majiji yetu
badala ya halmashauri zinazotoa vibali na kushindwa kusimamia kutokana
na ukosefu wa wataalamu.
vii)
Serikali iongeze idadi ya wataalam katika Halmashauri zetu ili waweze
kukidhi mahitaji na ukuaji wa kasi wa mji.
XXV. MSISITIZO KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI
• FIDIA ZA ARDHI
Mheshimiwa Spika; Mfano mwingine
wa mgogoro na madai ya muda mrefu ya fidia ni ya wananchi wa Kata ya Kwembe
hususan wanaoishi katika maeneo ya Mloganzila. Tarehe 1 Julai 2011 wakati Bunge
lilipokaa kama Kamati kupitia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya
Waziri Mkuu, Serikali iliulizwa kuhusu fidia ya wananchi wa eneo la Kwembe
Mlonganzila wanaopaswa kuhama kupisha ujenzi wa majengo ya Chuo cha Afya
Muhimbili (MUHAS). Serikali ilitoa majibu siku hiyo kuhusu wananchi
ambao walibaki baada ya wananchi 1919 kupewa fidia ya maendeleo na mimea. Hata
hivyo Serikali haikutoa majibu yoyote juu ya madai ya fidia ya ardhi ambao
wananchi hao walipewa.
Mheshimiwa Spika; Kambi Rasmi ya
Upinzani inaikumbusha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi izingatie
kwamba izingatie kwamba Rais Jakaya Kikwete aliahidi Julai, 2008 kuwa wananchi
wa eneo hilo wangelipwa fidia stahiki pamoja na kupewa viwanja mbadala (rejea Daily
News – 22 Julai, 2008). Aidha, Waziri Mkuu aliwahi kuandika barua kwa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya tarehe 21 Aprili, 2010 yenye
Kumb. Na. PM/P/1/569/29 ya kuelekeza mgogoro wa fidia ya ardhi umalizwe.
Mheshimiwa Spika; Ikumbukwe pia
kwamba Tarehe 22 Novemba, 2010 katika kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Serikali iliahidi kulipa fidia zote stahiki
ikiwemo fidia ya ardhi. Hii ni baada ya Wizara kuzingatia historia ya eneo
husika tangu wakati wa uhuru na uwepo wa hati ya kijiji cha Kwembe
kilichosajiliwa na kupewa hati No.DSM VC 40 ya tarehe 22 Februari, 1980.
Maeneo mengine yote yanayozunguka eneo hili yalipotwaliwa na mamlaka
mbalimbali yalilipwa fidia ya ardhi, mfano viwanja 600 Kwembe, Dampo
Kisopwa, ekari 200 za wasioona, na mji wa mdogo Luguruni.
Mheshimiwa Spika; Kambi Rasmi ya
Upinzani inayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikali hii inayojiita sikivu ya
CCM; ni sababu zipi zinazofanya mpaka sasa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na
Afya (MUHAS) pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
kutokulipa wananchi hao fidia ya ardhi mpaka hivi sasa kama Serikali
ilivyoahidi? Je, serikali hii inayojiita inajali inaona fahari gani kuwa na
wakimbizi wa ndani (internally displaced persons) wanaoishi baadhi katika
mahema katika eneo hilo na wengine wengi wakitangatanga katika maeneo mengine
baada ya kukosa walau kupewa viwanja mbadala kama Serikali ilivyowaahidi?
• VIWANJA VYA WAZI
Mheshimiwa Spika; Kwa nyakati
mbalimbali kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikihoji juu ya hatua
zilizochukuliwa kurejesha viwanja vya umma (public spaces) vilivyouzwa au
kubadilishwa matumizi kinyume cha sheria. Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa
na CHADEMA inaitaka Serikali kueleza ni lini hasa itakamilisha kuchukua hatua
na ni kwanini Serikali inashindwa kusimamia utawala wa sheria na hivyo kuachia
viwanja vingine zaidi kuvamiwa?
Mheshimiwa Spika; Itakumbukwa
kwamba Tarehe 1 Julai 2011 katika mkutano wa nne wa Bunge kikao cha kumi na
saba, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati akijibu maswali
bungeni aliahidi kuweka wazi kupitia kwa Manispaa za Dar Es Salaam taarifa ya
kamati ya uchunguzi ya mwaka 2010 iliyoundwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wakati
sasa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William
Lukuvi. Aidha, Waziri aliahidi kupitia kada ya askari wa ardhi (land rangers)
kuhakikisha maeneo hayo yanarejeswa na pia maeneo mengine mapya hayavamiwi.
Tangu wakati huo mpaka hivi mabango yamesimikwa katika baadhi ya maeneo mapya
yaliyovamiwa na wahusika kupewa notisi bila kuvunjika huku maeneo mengine mapya
yakiendelea kuvamiwa.
XXVIMUHSTASARI WA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAWAIDA NA
MAENDELEO
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2012/13 wizara
iliidhinishiwa jumla ya shilingi 101,731,722,000 , kati ya fedha
hizo shilingi 10,422,891,000 zilitengwa kwa ajili ya mishahara
shilingi 20,308,831,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi
71,000,000,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo… hadi februari
2013 wizara ilipokea jumla ya shilingi 30,991,919,144. Kati ya
fedha hizo shilingi 15,505,928,393 ni fedha za matumizi
mengineyo, shilingi 6,773,240,751 ni fedha za mishahara na shilingi
8,712,750,000 kwa ajili ya maendeleo..
Hata hivyo ,mpaka Februari 2013 ni shilingi 2,465,731,973
kwa ajili ya miradi ya maendeleo !
Mheshimiwa Spika, niliwahi kusema
hapa Bungeni, na ninarudia kusema; kama kuna eneo ambalo linaweza kutuletea
uvunjifu wa Amani,kama lisipofanyiwa kazi kwa umakini mkubwa ni ardhi .
Migogoro ya ardhi inachangiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu hakuna mipango
utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi!Wizara hii licha ya unyeti
wake ,ni kati ya wizara ambazo kwa miaka 5 mfululizo,mbali na kutengewa fedha
kidogo sana za miradi maendeleo,pamoja na ufinyu wa fedha husika zimekuwa
zikitolewa kidogo sana…wakati mwingine chini ya 20% ya fedha zote . Ni jukumu
letu wabunge kulisimamia hili.
Mheshimiwa Spika, baada ya
kusema hayo, kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inayoongozwa na
CHADEMA, naomba kuwasilisha.
____________________________________
Halima James
Mdee (Mb)
MSEMAJI MKUU WA
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
NA
WAZIRI KIVULI
WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Imesomwa leo, tarehe 27 Mei, 2013
No comments:
Post a Comment