Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetakiwa kurudia upya mchakato wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya kata, mkoa wa Dar es Salaam kwa madai kuwa, ulikuwa na kasoro nyingi. Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa jukwaa la wazi la semina ya jinsia na maendeleo (GDSS) linaloratibiwa na Mtandao wa Jinsia na Tanzania (TGNP), Badi Darusi, katika mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kutokana na hali iliyojitokeza ni dhahiri kuwa tume ilishindwa kusimamia ipasavyo kanuni na taratibu za uchaguzi kwa kuwaachia wanamaendeleo ya kata, ambao ni wanasiasa, yaani Madiwani na Wenyeviti wa Mitaa. Darusi alisema mchakato huo uligubikwa na vitendo vya kisiasa, rushwa, vitisho, unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia, hali iliyopelekea baadhi ya watu waliokuwa na sifa kuwa wajumbe wa mabaraza hayo kuenguliwa kimakosa kutokana na utashi pamoja na maslahi binafsi ya watu wachache.
“Tume ya Katiba ingalie hili suala kwa makini na ilifanyie kazi kwa kuwa kasoro hizo siyo nzuri hata kidogo kwani itapelekea kuwapo kwa katiba ya watu wachache wenye maslahi yao binafsi," alisema Darusi. Alifafanua kwamba Katiba inatakiwa kuwa ya watu wote bila ubaguzi wowote kama kisiasa au kijinsia. Aidha, aliitaka tume kufanya tathimini ya zoezi zima la upatikanaji wa wajumbe wapya katika mikoa yote ambayo kasoro zimebainika ili iweze kupata wajumbe halali wa mabaraza hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa GDSS, Janeth Mawinza aliitaka Tume hiyo kuwa makini kwa hatua zitakazofata ikiwamo zoezi la kuwapata wawakilishi wa Bunge la Katiba. Pia aliitaka Tume itambue mchango wa wanahabari katika mchakato mzima wa uundaji wa Katiba mpya na kuhahakikisha wanashirikishwa kikamilifu katika hatua za uundaji wa mabaraza ya Wilaya, Mkutano Mkuu wa katiba na kupewa nafasi katika Bunge maalum la katiba.
Chaguzi zilizotawaliwa na kasoro nyingi jijini Dar es Salaam ni katika Kata ya Mabibo ambako uchaguzi ulisitishwa na Kata ya Wazo Hill ambako uchaguzi ulifanyika katika mazingira ya kutatanisha.
Source: Ippmedia/Nipashe (April 2013). ''Uchaguzi mabaraza ya Katiba urudiwe'. Retrieved from Ippmedia/Nipashe

No comments:
Post a Comment