Lissu: Tusikilizane!! Naomba
tusilizane
Naomba kwa niaba ya timu Lwakatare
niwashukuru wote mliofika hapa kutuunga mkono na kumuunga mkono Kamanda wetu
Wilfred Muganyizi Lwakatare. Kama tulivyosema wakati kesi hii inafunguliwa ya
kwamba Lwakatare atapata utetezi wote unaostahili. Atapata utetezi wote
utakaothibitisha kwamba hana hatia yoyote. Tumetoka kusikiliza maombi
tuliyoleta Mahakama Kuu kuomba Mahakama kufuta mashauri yaliyofunguliwa dhidi
Wilfred Lwakatare.
Na niseme tu kwamba sisemi kesi itaamuliwaje, ila naomba
niseme hoja ambazo tumezizungumza mbele ya Jaji muda mfupi uliopita. Wilfred
Lwakatare alishitakiwa tarehe 18 na siku hiyo hiyo tukatoa hoja za kisheria
kwamba hayo mashtaka hayakuwa na mashiko, na upande wa washtaki wakajibu hoja
zetu, na mahakama ikaweka tareheya kutoa uamuzi wake juu ya hoja zetu. Lakini
badala ya kuiruhusu Mahakama itoe uamuzi, Waendesha mashtaka upande wa serikali
kesho yake wakafuta hati ya mashtaka waliyofungua tarehe 18, dakika hiyo hiyo
wakamkamata, dakika iliyofuta wakamfungulia mashtaka ya aina hiyohiyo
wakayapeleka kwa Hakimu mwingine; Na kwetu sisi huo ni mfano wa wazi wa
matumizi mabaya ya mamlaka ya Mwendesha mashtaka wa serikali wa mamlaka ya
kufuta mashtaka. Sheria zetu zinasema DPP anapofuta mashtaka lazima afanye
hivyo
1. Kwa lengo la kutenda haki
2. Kuzuia matumizi mabaya ya mfumo wa
Mahakama
3. Kwa manufaa ya Umma
Kufuta mashtaka na kuyafungua
yaleyale hakuna lengo la kutenda haki, kuzuia matumizi mabaya ya mfumo wa
Mahakama wala manufaa ya Umma, kwasababu hiyo basi tumeiomba Mahakama Kuu
iyafutilie mbali mashtaka dhidi ya Lwakatare. Lakini kuna jambo lingine; Kama
mlivyoona Wilfred Lwakatare ametoka hapa akiwa na pingu mkononi, ameshtakiwa
kwa makosa ya ugaidi, Sheria yetu ya ugaidi inasema mtu anayeshtakiwa kwa kosa
la kutenda mkutano wa kigaidi, huo mkutano wa kigaidi unatakiwa uwe na watu
watatu au zaidi. Lwakatare ameshtakiwa na mtu anaitwa Joseph Ludovick Lwezaura;
walikuwa wawili. Mkutano wa kigaidi sheria inasema uwe na watu watatu au zaidi,
“Hakukuwa na Mkutano wa kigaidi”. Na sheria hiyohiyo inasema kwamba mashtaka ya
kigaidi lazima hati ya mashtaka ionyeshe lengo la kigaidi, hati ya mashtaka
dhidi ya Lwakatare haionyeshi lengo la kigaidi. Kwa sababu hizo tumeiomba
Mahakama Kuu ifute mashtaka ya Kisutu, Wilfred Lwakatare arudi kwenye familia
yake na arudi kwenye Chama chake tuendeleze mapambano. Nawashukuruni sana.

No comments:
Post a Comment