Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora

Wasiliana nasi : chademadiaspora@gmail.com -Fair and Balanced Platform- Twitter @ChademaDiaspora
----------------------WE THANK AND APPRECIATE YOU FOR VISITING CHADEMA DIASPORA BLOG. AGAIN, THANK YOU!-----------------------

Sunday, April 7, 2013

Lipumba aitangazia CCM kiama


CHAMA cha Wananchi (CUF), kimewataka Watanzania kuhakikisha wanabadilisha mfumo wa maisha kwa kutoipa kura Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kwani muda wa ubabaishaji umefikia kikomo. Akizungumza na wananchi wa tarafa ya Pingwe mkoani hapa jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuna mambo mengi ambayo yanachangia hali ngumu ya maisha ya wananchi na moja ya sababu kubwa ni CCM kuendelea kuwepo madarakani, licha ya kushindwa kutatua kero na changamoto zinazowakabili Watanzania. Alisema ni wakati mzuri wananchi kuweka msimamo kuwa ikifika wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu mwaka 2015, CCM haipati nafasi ya kushinda kwenye chaguzi hizo, ili CUF iweze kushika dola.

"Umefika wakati wa kusema ubabaishaji sasa basi, hatuwezi kuendelea kama wananchi mtaendelea kuikumbatia CCM. Ni jinamizi baya ambalo linakwamisha ukuaji wa maendeleo yetu. "Kuendelea kuiacha CCM madarakani, ni kuendelea kubaki masikini, tunajuana Watanzania kila ukienda sehemu watu wamechoka na wamekata tamaa ya maisha. Tumeamua kujipanga kwa ajili ya kuleta mabadiliko na bahati nzuri wananchi wa Tanga na mikoa mingine wanatuamini," alisema Profesa Lipumba.


Alisema maisha ya wananchi, yameendelea kuwa magumu kila kukicha na kutolea mfano huduma za jamii kuwa zimeendelea kuwa duni, hasa maeneo ya vijijini. Kuhusu sekta ya elimu, Profesa Lipumba alisema katika eneo hilo, hali imekuwa mbaya kwani Serikali imeshindwa kutafuta suluhu na sasa sekta hiyo imekosa mwelekeo.


"Tunatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora, ambayo itawasaidia katika maisha yao na taifa kwa ujumla…tusiangalie idadi ya wanafunzi iliyopo shuleni bila kujali ubora wa elimu inayotolewa. "Hakuna vitabu, hakuna walimu wa kutosha, hakuna vitendea kazi lakini kwa bahati mbaya wenzetu ambao wapo serikalini wameshindwa kufanya lolote na kuendelea kuwa kimya. CUF tunaguswa na hali mbaya iliyopo katika elimu na kwa hili tutaendelea kulieleza hadi hali iwe nzuri," alisema Profesa Lipumba. 


Wakati huo huo, Profesa Lipumba amesema Mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa maarufu kwa viwanda, lakini sasa hali ya kimaendeleo katika mkoa huo imekuwa mbaya, kwani viwanda vyote havifanyi kazi kwani vimekufa. Profesa Lipumba, alitoa kauli hiyo wakati akitoa mada inayohusu maendeleo ya uchumi ya Mkoa wa Tanga, katika kongamano lililoandaliwa na CUF, kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo ya Demokrasi kwa Vyama vya Siasa ya nchini Denmark (DIPD).


Alisema mkoa huo, umejaliwa kuwa na rasilimali nyingi, ikiwemo zao la mkonge ambalo kwa sasa limekosa msukumo. "Katika soko la dunia, inaonyesha Tanga ilikuwa ikizalisha tani 234,000 kwa mwaka, lakini sasa imeporomoka na kufikia tani 25,000 tu.


Source: Mtanzania (March 2013). Lipumba aitangazia CCM kiama. Retrieved from Mtanzania


No comments: